Historia ya Kiswahili

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Historia ya Kiswahili



Maeneo penye wasemaji wa Kiswahili​





Historia ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani la Afrika ya Mashariki.
Neno Swahili ni neno la asili ya Kiarabu Sahil lenye maana ya pwani; sawahil ’’as-sawāhilī’’ (السواحلي) ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni wa eneo la pwani.

Kiswahili kilianza kama lugha ya miji na mabandari ya biashara ya kimataifa kwenye pwani la Afrika ya mashariki. Tuna historia jinsi gani miji kama vile Kilwa, Lamu na mingine kadhaa ilianzishwa na wafanyabiashara Waarabu au Wajemi waliooa wenyeji. Idadi ya wahamiaji kutoka Uarabuni haikuwa kubwa sana hivyo lugha ya wenyeji ilitumika kila mahali ila tu maneno mengi yameingia kutoka Kiarabu. Kwa ujumla Kiswahili ina maneno ya asili ya Kiarabu kati ya 30-40%, hali inayolingana na kiasi cha maneno ya asili ya Kilatini au Kifaransa katika lugha ya Kiingereza. Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu. Hivyo Kiswahili kilizaliwa kuwa lugha ya Kibantu kilichopokea maneno mengi ya asili ya nje.




Mwanzo katika miji ya pwani


Lugha imeandikwa kwa herufi za Kiarabu tangu karne ya 13 BK. Kwa bahati mbaya hatuna maandiko ya kale sana kutokana na hali ya hewa kwenye pwani isiyosaidia kutunza karatasi za kurasa zenyewe zinaweza kuoza kutokana na unyevu hewani pamoja na wadudu wengi walioko

katika mazingira ya pwani. Lakini maandiko ya kale yanayopatikana kutoka karne ya 17 BK huonyesha ya kwamba tenzi na shairi zinafuata muundo inayotangulia maandiko yenyewe kwa karne kadhaa. Sehemu kubwa ya maandiko ya kale ni tenzi yaani mashairi yenye aya maelfu.

Tenzi ndefu kabisa inahusu kifo cha Mtume Muhamad ikiwa na aya 45,000.
Kiswahili kimepokelewa kirahisi na wenyeji kwa sababu wenyeji walikosa lugha ya pamoja kati yao, lugha za Kibantu ziko karibu sana na athira ya

Kiarabu ilikuwa kilekile kote pwani. Haya yote yalisaidia kujenga umoja wa Kiswahili katika eneo kubwa la pwani la Afrika ya Mashariki.
Kufika kwa Wareno Afrika ya Mashariki kuanzia mwaka 1500 kulileta athira mpya ikiwa maneno kadhaa ya Kireno yameingia katika Kiswahili kama vile "bendera" na "meza". Kuwepo kwa wafanyabiashara Wahindi katika miji mikubwa ya pwani kuliingiza pia maneno ya asili ya Kihindi katika lugha kama vile "lakhi", "gunia" n.k. Athira ya lugha za Kihindi iliongezeka kiasi baada ya Waingereza kutumia Wahindi wengi kujenga reli ya Uganda.

Kiswahili kilitumika katika kanda ndefu sana kutoka Somalia hadi Msumbiji wa Kaskazini. Wafanyabiashara Waswahili waliendesha biashara ya misafara hadi Kongo. Kiswahili kiliendelea kuenea kwenye njia za misafara hii. Kila msafara kilihitaji watu mamia hadi maelfu wa kubeba mizigo ya biashara kutoka pwani hadi pale msafara ulipolenga hata Ziwa Tanganyika. Watu hawa wote walisambaza matumizi ya Kiswahili katika sehemu za ndani. Lakini katika maeneo fulani biashara hii ilijenga pia kizuizi. Watu kama Waganda waliona Kiswahili ni lugha ya Waislamu tena lugha ya biashara ya watumwa hadi leo ni wagumu kukubali Kiswahili. kkiswahili kilitumika kama lugha ya biashara baina ya watu wa pwani na bara.

Kiswahili wakati wa ukoloni


Karne ya 19 BK ilileta utawala wa kikoloni. Wakoloni walitangulia kufika katika mabandari ya pwani wakatumia mara nyingi makarani, askari na watumishi kutoka eneo la pwani wakijenga vituo vyao barani. Watu hawa walipeleka Kiswahili katika pembe za bara.
Wajerumani waliamua kutumia Kiswahili kama lugha ya utawala katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapo waliweza kutumia kazi ya

Wamisionari
wakristo wa awali hasa Ludwig Krapf waliowahi kufanya utafiti wa lugha na kutunga kamusi na sarufi za kwanza pamoja na kuunda mfumo wa kuandika Kiswahili kwa herufi za Kilatini.
Utawala wa kikoloni ulirahisisha mawasiliano kati ya wenyeji. Reli zilijengwa na wafanyakazi kutoka makabila mbalimbali walishirikiana. Waafrika

walilazimishwa kulipa kodi kwa wakoloni hivyo walitafuta kazi ya ajira. Hasa katika mashamba makubwa yaliyolima mazao ya biashara pia katika migodi ya Kongo watu wa makabila mengi walichanganya wakitumia hasa Kiswahili kati yao. Kwa namna hiyo lugha ilienea zaidi.

Waingereza baada ya kuchukua Tanganyika kutoka kwa Wajerumani waliendela kutumia Kiswahili kama lugha ya utawala. Kuanzia mwaka 1930 waliunda kamati yenye shabaha ya kuunganisha lahaja mbalimbali na kuunda Kiswahili cha pamoja kwa ajili ya Afrika ya Mashariki (Inter-territorial Language (Swahili) committee for the East African Dependencies). Mwenyekiti alikuwa Frederick Johnson, makatibu R.K. Watts, P.Mzaba na Seyyid Majid Khalid Barghash. Kamati hii iliamua kutumia lahaja ya Kiunguja kuwa msingi wa Kiswahili cha pamoja kilichoendela kufundishwa

mashuleni. Leo hii ni Kiswahili rasmi kinachojifunzwa na wanafunzi na kuandikwa magazetini na vitabuni.
Miaka ya ukoloni ilisababisha pia kupokelewa kwa maneno mapya katika Kiswahili. Kijerumani kiliacha maneno machache kama "shule" (Kijer.

Schule) na "hela" (Kijer. Heller) lakini maneno mengi sana ya asili ya Kiingereza yalipokelewa. Kiswahili kimeonyesha uwezo mkubwa wa kupokea maneno kutoka lugha tofauti sana kikitumia maneno haya kufuatana na sarufi ya Kibantu ya Kiswahili.kiswahili ni kibantu kwa kutumia hoja za kiisimu na kihistoria.kiisimu ni hoja za kisayansi ambazo huonyesha kila neno la kiswahili lina mzizi wa lugha za kibantu na mzizi ni shina la neno kwa kiingereza tunasema (stem)

Kiswahili leo


Katika Tanzania Kiswahili kimekuwa lugha rasmi ya serikali na taifa. Shule za msingi hutumia Kiswahili lakini shule za sekondari na vyuo bado zinaendelea kufundisha kwa Kiingereza.
Kenya imetangaza Kiswahili kuwa lugha ya taifa lakini inaendelea kutumia Kiingereza katika shughuli za serikali. Watu wa tabaka za juu mara nyingi hupendela kutumia Kiingereza wakiona ni lugha bora. Lakini tangu 1986 wanafunzi wote wanatakiwa kujifunza Kiswahili katika shule za

sekondari. Tatizo mojawapo ni kuwepo wa makabila makubwa kama Wakikuyuau Waluo wenye wasemaji wengi sana katika eneo moja hali isiyosaidia kujifunza lugha tofauti. Pia kaskazini na magharibi ya Kenya wenyeji wengi si wasemaji wa lugha za Kibantu ambao hawaoni Kiswahili ni lugha rahisi.

Uganda
inatumia Kiswahili kama lugha ya polisi na jeshi hali ambayo haikuongeza upendo wa Wauganda kwa lugha kutokana na historia ya Uganda ya kuwa na vita na serikali za kijeshi. Lakini kinasikika pia kama lugha ya biashara masokoni. Pamoja na kwamba Waganda walikichukulia Kiswahili kama lugha ya kitumwa lakini pia lugha hii ilionekana kuwa na ustaarabu wa kiarabu zaidi yaani Uislamu. Lugha ya Kiswahili ilitumika katika kueneza dini hiyo ambayo Waganda hawakuipenda.

Mashariki mwa Kongo Kiswahili kimeenea sana ni moja kati ya lugha nne za kitaifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwenye visiwa vya Ngazija ni lahaja mbalimbali za Kiswahili zinazotumika na wananchi.

Kumbe Lugha ya Kiswahili ni Tamu kuliko Lugha zote za Afrika?
 
Kwa upande wa congo hilo eneo lime expand zaidi... Na uganda sio wengi wanao ongea kiswahili. hata north western kenya pia... hii ramani sio sahihi I am affraid
 
Kwa upande wa congo hilo eneo lime expand zaidi... Na uganda sio wengi wanao ongea kiswahili. hata north western kenya pia... hii ramani sio sahihi I am affraid

kuna baàdhi ya maeneo ya kongo yanatumia lugha ya kisw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom