Historia ya Katiba ya Tanzania na mabadiliko 14 ya Katiba tokea Uhuru mpaka sasa

Wazo Kuu

Member
Oct 21, 2018
80
400

Katiba ya nchi ni muafaka wa kitaifa unaoanisha namna taifa linavyohitaji kujitawala katika mambo yote na kuendesha mambo yake. Hivyo basi, Katiba ya nchi ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali pia huanisha haki za msingi za wananchi.

Katiba ya nchi hutungwa na wananchi wenyewe kama watu huru ili kupata muafaka wa taifa lao na namna gani wangependa kujitawala.

Kwa kifupi, Katiba sio chombo cha wanazuoni wachache bali ni chombo kinachoonyosha umiliki wa nchi na rasilimali ya wananchi, nafasi ya wananchi katika utawala na namna gani wangependa kuweka utawala wa nchi yao na hivyo kutengeneza muundo wa serikali yao.

Kwa hiyo; Katiba ya nchi ni waraka wa kitaifa unaoweka bayana, pamoja na mambo mengine, mfumo wa haki za msingi kwa wananchi wake, mihimili yake ya dola, namna ya kuweka utawala katika ngazi

zote, muundo wa serikali yao na namna ya usimamizi wa mapato na matumizi ya rasilimali yote ya kitaifa bila ukandamizaji wa aina yeyote kwa jinsia zote.

Tunapoizungumzia Katiba ya Tanzania hatuna budi kukumbuka Azimio la Tabora (Busara) 1958 ambapo wazalendo watanganyika walimuunga mkono Mwalimu Nyerere kutumia busara na singuvu kudai Uhuru wa Tanganyika. Historia inatuambia wakoloni walimshitaki Mwalimu Nyerere kwa kile walichokiita kuwa ni Uchochezi na kutakiwa kulipafaini shilingi elfu tatu ama kenda jela miezi sita, lakini wazalendo walichanga nakumnusuru Mwalimu Nyerere kwenda jela, mbio na harakati za busara zikasonga mbele hata kuleta uhuru tarehe 09 Disemba 1961.

consti-pic.jpg

Tukio hili la uhuru wa Tanganyika liliweka mazingira ya kipindi cha mpito kutokana na mabadilikoya kiutawala toka kwa Wakoloni Waingereza kwenda kwa Wazalendo waTanganyika hasa kupitia tamko rasmi la serikali ya kikoloni -

Tanganyika constitution Order in Council of 1960, ambalo ndilo lililoidhinisha kuwepo kwa serikali huru ya Tanganyika na Katiba yake (the Independence Constitution) mnamo mwezi Disemba, 1961. Kwa jinsi hiyo, kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 kulileta fursa ya kipekee ya mabadiliko ya baadae ya katiba, hasa kutokana na ulazima wa kuweka mambo na hatima ya Taifa huru la Tanganyika chini ya utawala huru wa Watanganyika. Hata hivyo, umuhimu wa mabadiliko ya kikatiba baada ya uhuruhaukuwa umefichika. Kwa wakati ule, katiba iliyoleta uhuru (yaani the Independence Constitution) ilikuwa na muundo uliofuata mfumo wa Ki-ingereza (Westminster).

Katika mfumo huu Malkia wa Uingereza bado anabakia mtawala ila si mtendaji mkuu. Waziri mkuu ndiye anayeunda serikali na kuwa mtendaji mkuu. Kwa hali hiyo Tanganyika ilikuwa bado nakivuli cha Malkia kwa mbali. Kwa upande wa siasa za vyama, kimsingi, katiba hii ya kwanza ya Tanganyika ilikuwa ni ya vyama vingi. Hata hivyo, kwa vile Katiba hii ilitengenezwa na kupewa Tanganyika chini ya Serikali ya Malkia wa Uingereza enzi hizo, wataalamu wa mambo ya katiba wanatanabaisha kwamba, katiba hii, ilikuwa ni ya namnatu ya kuleta makubaliano au maridhiano kati ya wakoloni na wazalendo wa Kitanganyika lengo hasa likiwa ni kutoa hakikisho la kuwepo dola huru la Tanganyika.

Chini ya Katiba hii ya uhuru, dhana kubwa ya bunge kuwa chombo chenye mamlaka ya juu (supremacy of the parliament) ilijikita ndani yakepamoja na ile ya kuhakikisha kuwepo kwa uhuru wa mahakama (independence of the judiciary.)

Uwepo wa dhana hizi muhimu katika katibaya uhuru lilikuwa jambo lisiloepukika hasa kutokana na msisimko mkubwa ambao wapigania uhuru walikuwa nao na hivyo serikali ya kikoloniisingependa kuona mabadiliko yatakayo leta madhara hasa kwa maslahi yaobaada ya uhuru. Maslahi yoyote yanalindwa dhidi ya ukandamizi wa serikalikama bunge na mahakama zikiwa huru na zikitenda kazi zake ipasavyo. Hivyoserikali ya kikoloni ililiona jambo hilo na kuliweka ndani ya katiba hata kamawao hawakuwatendea hivyo Watanganyika kipindi cha ukoloni.)


Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika 1962.

Kipindi cha pili kilicholeta mazingira mbadala yaliyohitaji mabadiliko yakatiba Tanzania (Tanganyika) kilikuja mwaka 1962. Mwaka kushika hatamu ikaneemeka zaidi. Kwa hali hii ni dhahiri kuwa hata Katibatuliyo nayo hivi leo haikuwashirikisha wananchi wote kwani si wotewaliokuwa wanachama wa chama tawala. Hivyo utaratibu wa kutunga Katiba mpya kwa kuitisha kongamano la Katiba (constitutional conference) haujawahi kufanyika wala kuwa sehemu ya desturi nchini Tanzania hadi leo.

MABADILIKO NA MABORESHO KATIKA KATIBA YAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 1977 (AMENDMENTS).

I. Mabadiliko ya Kwanza 1979

Mabadiliko ya kwanza katika Katiba ya mwaka 1977 yalifanyika mwaka 1979 yakilenga hasa kwa ukuu kuanzishwa kwa mahakama ya rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye mamlaka katika pande zote za Muungano. Hii ilichangiwa pia na kuanguka kwa jumuiya ya Afrika Mashariki ya 1967 hivyomifumo yote ikiwemo ya kimahakama kurudi kwa dola husika.

II. Mabadiliko ya Pili ya 1980
Mabadiliko ya pili yalifanyika mwaka 1980 yakilenga kutatua kero mbalimbali zaMuungano hasa kwa upande wa Zanzibar. Hata hivyo mabadiliko haya hayakutatuakero hizo kama ilivyotarajiwa.

III. Mabadiliko ya Tatu 1980
Mwaka huo huo yalikuja tena mabadiliko mengine, yawezekena hii ilitokana naubovu wa Katiba ama uchanga wa Taifa na ukuaji wake uliohitaji mtazamo shirikishikwa watu wa Tanzania, na hilo halikufanyika ipasavyo. Katiba iliyoshirkisha watuhuwa madhubuti na imara yenye kuhimiri mabadiliko ya kiuchumi, siasa na jamiimaana hulenga vizazi vyote.

IV. Mabadiliko ya Nne 1982
Mabadiliko ya nne ya Katiba ya 1977 yalikusudia kuboresha taratibu za kuteua wakuuwa mikoa na wilaya, hata hivyo mabadiliko haya hayakuweka bayana uwajibikaji wawakuu hawa.

V. Mabadiliko ya Tano 1984
Mabadiliko ya tano yalifuatia mahitaji ya watanzania kuwepo na ustawi na uangaliziwa haki za binadamu katika Katiba na hivyo kuingiza tamko la haki za binadamukatika Katiba. Sehemu ya tatu ya Katiba hii inajumuisha tamko la haki za binadamu.

VI. Mabadiliko ya Sita 1990
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilianzishwa na mabadiliko haya ya mwaka 1990yakiwa ni mabadiliko ya sita katika Katiba ya mwaka 1977. Kabla ya tume hiimasuala ya uchaguzi yalikuwa chini ya uangalizi wa Chama (CCM). Lengo lakuanzisha tume ilikuwa kusimamia uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa 1995.

VII. Mabadiliko ya Saba 1990
Ndani ya mwaka huu yalikuja mabadiliko mengine tena yakilenga kuweka utaratibuwa kuwa na mgombea mmoja wa urais upande wa Zanzibar kuundoa utaratibu waawali ambao ulilalamikiwa.


VIII. Mabadiliko ya Nane 1992
Mantiki ya mabadiliko ya mwaka 1992 ilikuwa ni kuruhusu tena mfumo wa vyamavingi nchini. Hii ilitokana na mwelekeo wa magharibi na msukumo wa wakubwa wadunia waliotaka demokrasia ijikite katika vyama vingi vya siasa. Hata mfumo waBunge pia ulibadilika kwa kuruhusu viti maalumu kwa wanawake kwa asilimia 15 naviti vitano kwa baraza la wawakilishi ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania.

IX. Mabadiliko ya Tisa 1992
Muda mfupi tu mara baada ya mabadiliko ya nane, yalitokea tena mabadilko ya tisayakirekebisha taratibu za chaguzi za Rais wa Muungano, tamko kwamba Rais anaweza kuondolewa kwa kura ya Bunge kwa kukosa imani nae na kuanzisha nafasiya Waziri Mkuu kikatiba.

X. Mabadiliko ya Kumi 1993
Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoanzishwa katika mabadiliko ya sita ya mwaka 1990ilipewa mamlaka kikatiba kusimamia chaguzi za madiwani na hivyo chaguzi hizokufanyika pamoja na uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge.

XI. Mabadiliko ya Kumi na Moja 1994
Mabadiliko haya yalileta utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza kwa nafasi yaUrais ambaye huwa makamu wa Rais mara baada kushinda uchaguzi mkuu. Na kwamantiki hii basi mabadiliko haya yaliweka ukomo kwa Rais wa Zanzibar kuwaMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

XII. Mabadiliko ya Kumi na Mbili 1995
Kiapo kwa Rais, makamu wake, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar kuulindaMuungano wa Tanganyika na Zanzibar kiliwekwa na mabadilko haya. Na ukomo waRais kuwa vipindi viwili tu ulianzishwa na mabadilko haya.

XIII. Mabadiliko ya Kumi na Tatu 2000
Hapa mfumo wa kumpata mshindi katika kinyang’anyiro cha Urais kwa kupata kuranyingi zaidi ya wapinzani wake. Kabla ya mabadiliko haya Rais alipatikana kwakupata walau asilimia 51 ya kura zote. Kadhalika Rais alipewa mamlaka kikatibakuteua watu kumi kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kadhalika Viti maalumu vya wanawake bungeni viliongezwa kufika asilimia 20.

XIV. Mabadiliko ya Kumi na Nne 2005
Hapa viti maalumu vya wanawake bungeni viliongezwa tena mpaka asilimia 30. Lakini pia uhuru wa kuabudu, uhuru wa kushiriki na watu wengine, uhuru wa maonina kujieleza viliwekwa bayana na kuondoa vizuizi vyote vilivyokuwepo kwenye Katiba. Kadhalika wabunge wa viti maalumu wanateuliwa sasa kwa uwiano wa ushindi wa kila chama majimboni.

Hivyo watanzania wanawajibu wa kuisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu inatosha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom