Historia ya Inspekta mkuu wa polisi (IGP) tokea tupate Uhuru

Kaka JokaKuu, ...............................Umenikumbusha mbali sana kuhusu Hamisi Nyau, miaka ya nyuma palikuwa na story nyingi sana zikimuhusu huyo jamaa, ujambazi na ushirikina...................tunaweza pata kumbukumbu nzuri sana humu
 
Kituko,

..Tryphon Maji alikuwa RPC wa D'Salaam miaka ya 90.

..kuna tajiri wa kihindi alikamatwa na kuwekwa ndani central police. sina uhakika aliwekwa ndani kwa amri ya nani. lakini Tryphon Maji na Silvano Adel[katibu mkuu mambo ya ndani] walikwenda central police na kumtoa mhindi mahabusu. habari hiyo ilimfikia Augustino Mrema, waziri wa mambo ya ndani, na yeye akaripoti Ikulu, na kupelekea vibarua vya Maji na Adel vikaota majani.

..Tryphon Maji na Silvano Adel wametangulia ktk haki miaka ya hivi karibuni.

ukwelikitugani, gobore, Kichuguu,

..Solomon Liani aliteuliwa na Mwalimu Nyerere, na alitumikia mpaka wakati wa Raisi Mwinyi, ambaye ndiyo alimteua IGP Harun Guido Mahundi, aliyekuwa RPC Arusha.

..ukiangalia timeline ya matukio, nadhani wahaini walikamatwa na kutoroka wakati Solomon Liani akiwa IGP. sina uhakika kuhusu wahusika waliochukuliwa hatua za kinidhamu.

..kuna kipindi fulani ambapo waziri wa mambo ya ndani, pamoja na mkuu wa magereza walilazimika kujiuzulu. sasa sina uhakika kama walijiuzulu kutokana na kutoroka kwa wahaini, au kutokana na kutoroka kwa majambazi sugu karibia 21 toka gereza/mahabusu ya ukonga.

..naomba mwenye kumbukumbu nzuri watusaidie kuhusu lile tukio la majambazi sugu kama Hamisi "nyau", Leloo, na wenzao kutoroka gerezani/mahabusu ilikuwa ni mwaka gani na kama kuna hatua zozote zile zilichukuliwa dhidi ya IGP, waziri wa mambo ya ndani, na mkuu wa magereza.

Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo alikuwa Abdallah Natepe.
 
gobore,

..asante kwa marekebisho yako.

..ndiyo uzuri wa JF kwamba tunarekebishana.

..sasa naomba isomeke kwamba mkuu wa magereza aliyejiuzulu ni Geneya Gabriel, na siyo Mwanguku.
 
Last edited by a moderator:
gobore,

..asante kwa marekebisho yako.

..ndiyo uzuri wa JF kwamba tunarekebishana.

..sasa naomba isomeke kwamba mkuu wa magereza aliyejiuzulu ni Geneya Gabriel, na siyo Mwanguku.

Ngoja nijaribu kuweka timeline kama kumbukumbu yangu ilivyo kwa hawa Makamishna wa Magereza,wanaojua zaidi watanisahihihisha makamishna wa magereza waliopata kuongoza ni

Obadia Rugimbana(62-66) huyu ni baba yakemzazi Jordan Rugimbana Dc Kinondoni,Ramadhani Nyamka(67-77),Gabriel Ganja Geneya (77- 83 or 82),Simon Mwanguku,Jumanne Mangara,Ornel Mallisa( Benno Mallisa dad...tetesi am not sure),Nicas Banzi 2001-2007( Huyu ndo alitoka kwa aibupamoja na waziri wake Omari Mapuri baada yakupiga waandishi wa habari) halafu Agustino Nanyaro 2007 mpaka 2012 kamuachia Fidelis Mboya anayekaimu kuanzia May

Note:
..........kuanzia Uhuru jeshi liliongozwa na Commisioner of Prisons ila muundo ulikuja kubadilishwa mwaka 1974 na mkuu kuwa Commisioner General of Prisons na hivyo basi kumfanya RamadhaniNyamka kuwa mtanzaniawa kwanza kushika cheo hicho

.........graduate wa kwanza(Degree holder) kwenye majeshi yote ya Tanzania alitokea Magereza, Commisioner Ganja Geneya

Pamoja
 
Baada ya Natepe, Waziri aliemfuata alikuwa na General Kimario, na nadhani huyu ndiye aliyekumbwa na skendo ya majambazi kutoroka, kama kumbukumbu yangu ni sahihi. Brigedia Natepe alipoondoka alipongezwa sana na wabunge wote lakini General Kimaryo alipoondoka ilikuwa ni kimya kimya tu; nadhani alitupwa kuwa mkuu wa mkoa fulani badala yake.
 
1. Kwa Kwanza alikuwa anaitwa Elangwa Shaidi, huyu alistaafu kutokana na umri. Sina uhakika alikuwa na umri gani.

2. Aliyefuatia ni Hamza Azizi ambaye aligonga mtu na gari la serikali akiwa amelewa. Hata hivyo kwa vile alikuwa ni mtoto wa Mzee Aziz Dosa, ambaye alikuwa ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa Nyerere wakati wa Uhuru, Nyerere akaamua kumhifadhi kwa kumhamishia kwenye ubalozi wa Tanzania huko USA. Kuna binti yake ambaye leo naye ni balozi huko foreign affairs.

3. Samson Pundugu alistaafishwa na Nyerere ikiwa ni pamoja na Ali Hassani Mwinyi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wakati huo. Hiyo ilikuwa ni response kutokana na mauaji ya wachawi huko Shinyanga. Watu wengi sana alistaafishwa kazi ndani ya jeshi la polisi na wizara nzima ya mambo ya ndani.

4. Philemon Mgaya nimepoteza kumbukumbu kidogo, ila nadhani aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora au mkuu wa polisi wa Tabora. Nilisoma na mmoja wa watoto wake, na sikumbuki kama alitoka Tabora ndipo akawa IGP au alitoka IGP ndiyo akaenda Tabora. Ila tetesi zilizokuwapo ni ama alipokea au aliomba rushwa ili kutoa kibali cha kuendesha biashara ya ulinzi kwa kampuni y Group 4 Security wakati huo.
Kwani wewe ulikuwa Tabora mwaka gani . Mimi nilisoma tabora katiya mwaka 1978 na 1980 namkumbuka mtoto wa mzee Mgaya yeyealikuwa Milambo Sekondari O level
 
Mkuu naomba kujua huyu Marehemu Mzee Michael Mgema ambaye baadae alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza hakuwahi kuwa IGP?
 
Wakuu naomba kujua huyu Marehemu Mzee Michael Mgema ambaye baadae alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza hakuwahi kuwa IGP?
 
Kwani wewe ulikuwa Tabora mwaka gani . Mimi nilisoma tabora katiya mwaka 1978 na 1980 namkumbuka mtoto wa mzee Mgaya yeyealikuwa Milambo Sekondari O level
Huenda ndiye huyo huyo; alikuwa anatumikia sana kwenye ibada za kanisa katoliki.

Vipi wewe ulisoma kwa miaka mitatu tu?
 
Wakuu naomba kujua huyu Marehemu Mzee Michael Mgema ambaye baadae alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza hakuwahi kuwa IGP?
Mkuu , Mtemi Michael Mjema hakuwahi kuwa IGP, alivyotoka kuwa RPC Dodoma yeye na wake zake zake alihamia DSM na kuwa mkuu wa kitengo kile cha Afande Tossi, kisha baada ya hapo na wake zake alistahafu na hatimae kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza
 
WAKURUGENZI WA IDARA YA UPELELEZI (CID) TANGU 1960 HADI LEO.
spacer.gif
spacer.gif
17/9/1960-1/9/1961 M. J. McKinlay ACP.
1/9/1961-19/7/1962 K.F.J. Flood SSP.
19/7/1962-6/12/1962 R. T. L. Egan ACP.
6/12/1962-2/8/1967 E. E. Akena ACP.
2/81967-13/11/1967 R.S. Kaswende ACP.
13/11/1967-4/6/1968 N.G.M. Sawaya SACP.
4/6/1968-2/9/1968 A.R.Shungu SACP.
2/9/1968-23/9/1970 N.G.M. Sawaya SACP
23/9/1970-21/5/1973 S.H.Pundugu CP.
21/5/1973-28/5/1975 B.M. Omari CP.
28/5/1975-14/8/1975 F.M. Mtono SACP.
14/8/1975-15/2/1977 H.M.Lyimo CP.
12/2/1977-21/5/1981 M.Mwingira CP.
21/5/1981-6/3/1985 J.M.Lemomo CP.
7/3/1985-30/6/1992 A.A.B.Mwaitenda CP.
22/10/1992-3/5/1996 E.A.Man CP.
4/5/1996-2/3/2006 Adadi Rajab CP.
3/3/2006 Hadi sasa R.S. Manumba CP.

VIONGOZI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA UKOLONI HADI UHURU.
spacer.gif
spacer.gif
1916 – 1920 Major S.T. Davis.
1920 – 1929 E.F. Brown.
1929 – 1933 G.H. Kiram.
1933 – 1942 F.A.B. Nicholl.
1942 – 1949 E.B. Birthray.
1949 – 1951 W.A. Muller.
1951 – 1958 R.E. Fouler.
1958 – 1962 G.S. Wilson.
1962 – 1964 E.N. Shaidi.
spacer.gif
spacer.gif
INSPEKTA JENERALI WA POLISI TANGU MUUNGANO HADI LEO.
img_pol2.jpg
1964 – 1970
1970 – 1973
Elangwa N. Shaidi Hamza Azizi.
7/8/1973 – Aug 1975 8/8/1975 – Nov 1980
Samweli H. Pundugu. Philemon N. Mgaya.
2/11/1980 – 30/11/1984 1/12/1984 – 3/5/1996
Solomoni Liani. Harun G. Mahundi.
4/5/1996 – 2/3/2006 3/3/2006 Hadi sasa
Omar I. Mahita. Saidi A. Mwema.
 
HISTORIA YA JESHI LA POLISI – TANZANIA
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
1885 Wajerumani walifika Tanganyika ili kutawala, waliunda kikundi cha watu kilichofanya kazi ya Polisi.
spacer.gif
spacer.gif
1916 Vita kuu ya kwanza ikiendelea Ulaya na Afrika, kundi la Maafisa 31 (NCO) kutoka Afrika Kusini wakiwa na silaha (Rifle) walifika Tanganyika kufanya kazi za Polisi.
spacer.gif
spacer.gif
1919 Tarehe 25 August 1919 Serikali ya Kiingereza ilitangaza katika Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kuwa Jeshi la Polisi Tanganyika limeanzishwa rasmi. Makao Makuu ya Jeshi hilo yalikuwa Wilayani Lushoto chini ya uongozi wa Major S.T DAVIS.
spacer.gif
spacer.gif
1921 Kundi lingine la Wakaguzi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika kuanzisha shule ya Mafunzo ya Polisi huko Morogoro.
spacer.gif
spacer.gif
1925 Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa Tingatinga kwenye machimbo ya dhahabu Chunya.
spacer.gif
spacer.gif
1930 Makao Makuu ya Polisi yalihamishwa kutoka Lushoto kuja Dar es Salaam.
spacer.gif
spacer.gif
1949 Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini kurejesha amani penye vurugu.
spacer.gif
spacer.gif
1949 Vijana mbalimbali wa Kiafrika toka shule mbalimbali za Sekondari Nchini walichaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi chini ya uangalizi (Probation Inspectors).
spacer.gif
spacer.gif
1952 Kikosi cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwa katika Polisi bila kutumia nyaya za simu.
spacer.gif
spacer.gif
1958 Askari wa Polisi wa Kikie (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Miss. Payee.
spacer.gif
spacer.gif
1961 Tarehe 9 Desemba, 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake. Baada ya uhuru, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo toka katika kutumikia Wakoloni na Walengwa wakawa ni Wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali ya Wananchi.
spacer.gif
spacer.gif
1962 Kwa mara ya kwanza nafasi ya Kamishna wa Polisi aliyekuwa Mzungu Mr. M.S Wilson – C.P, ilichukuliwa na Mwafrika
Mr. Elangwa Shaidi – C.P.
spacer.gif
spacer.gif
1962 Maafisa 10 Waafrika waliteuliwa kuchukua nafasi za wakuu wa Polisi wa Mikoa (Regional Police Commanders).
spacer.gif
spacer.gif
1964 Tarehe 26/04/1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na hivyo kuunda Tanzania. Kwa hiyo Mr. Elangwa Shaidi alipandishwa cheo nakuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP).
Alisaidiwa na Makamishna watatu wa Polisi ambao ni:-
1. Mr Edington Kisasi Kamishna wa Polisi Zanzibar.
2. Mr. Hamza Azizi Kamishna wa Polisi Bara.
3. Mr. Akena Kamishna wa Polisi CID.
spacer.gif
 
1. Kwa Kwanza alikuwa anaitwa Elangwa Shaidi, huyu alistaafu kutokana na umri. Sina uhakika alikuwa na umri gani.

2. Aliyefuatia ni Hamza Azizi ambaye aligonga mtu na gari la serikali akiwa amelewa. Hata hivyo kwa vile alikuwa ni mtoto wa Mzee Aziz Dosa, ambaye alikuwa ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa Nyerere wakati wa Uhuru, Nyerere akaamua kumhifadhi kwa kumhamishia kwenye ubalozi wa Tanzania huko USA. Kuna binti yake ambaye leo naye ni balozi huko foreign affairs.

3. Samson Pundugu alistaafishwa na Nyerere ikiwa ni pamoja na Ali Hassani Mwinyi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wakati huo. Hiyo ilikuwa ni response kutokana na mauaji ya wachawi huko Shinyanga. Watu wengi sana alistaafishwa kazi ndani ya jeshi la polisi na wizara nzima ya mambo ya ndani.

4. Philemon Mgaya nimepoteza kumbukumbu kidogo, ila nadhani aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora au mkuu wa polisi wa Tabora. Nilisoma na mmoja wa watoto wake, na sikumbuki kama alitoka Tabora ndipo akawa IGP au alitoka IGP ndiyo akaenda Tabora. Ila tetesi zilizokuwapo ni ama alipokea au aliomba rushwa ili kutoa kibali cha kuendesha biashara ya ulinzi kwa kampuni y Group 4 Security wakati huo.

Kama sikosei Solomon Liani naye aliwahi kuwa IGP.
 
Ngoja nijaribu kuweka timeline kama kumbukumbu yangu ilivyo kwa hawa Makamishna wa Magereza,wanaojua zaidi watanisahihihisha makamishna wa magereza waliopata kuongoza ni

Obadia Rugimbana(62-66) huyu ni baba yakemzazi Jordan Rugimbana Dc Kinondoni,Ramadhani Nyamka(67-77),Gabriel Ganja Geneya (77- 83 or 82),Simon Mwanguku,Jumanne Mangara,Ornel Mallisa( Benno Mallisa dad...tetesi am not sure),Nicas Banzi 2001-2007( Huyu ndo alitoka kwa aibupamoja na waziri wake Omari Mapuri baada yakupiga waandishi wa habari) halafu Agustino Nanyaro 2007 mpaka 2012 kamuachia Fidelis Mboya anayekaimu kuanzia May

Note:
..........kuanzia Uhuru jeshi liliongozwa na Commisioner of Prisons ila muundo ulikuja kubadilishwa mwaka 1974 na mkuu kuwa Commisioner General of Prisons na hivyo basi kumfanya RamadhaniNyamka kuwa mtanzaniawa kwanza kushika cheo hicho

.........graduate wa kwanza(Degree holder) kwenye majeshi yote ya Tanzania alitokea Magereza, Commisioner Ganja Geneya

Pamoja

Mbona naona kama wengi ni watu wa kaskazi samahani lakini sioni wa Nyanda za Juuu kusini kama kule kwetu Namanyere
 
Back
Top Bottom