Historia ya Inspekta mkuu wa polisi (IGP) tokea tupate Uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Historia ya Inspekta mkuu wa polisi (IGP) tokea tupate Uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Julius Kaisari, Sep 3, 2012.

 1. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Ndugu wakuu, Maveterani wa kitambo,na wote wenye ufahamu,Salaam.

  Ninapenda kufahamu juu ya Wakuu wa "Jeshi" la Police, IGPs tangu Tanganyika huru na baadae Tanzania,na rekodi zao , walau zinazokumbukwa.

  Nimefikia hatua hii ya kuleta hapa jambo hili hasa wakati huu ambapo Ma-polisi wanaonekana miungu watu,watoa Roho za raia,pasipo kuulizwa,na wanatokeza kifua mbele kutuaminisha hadithi zao za uongo,kama vile wote sisi ni mazuzu.

  Pia Leo katika kipindi cha Jenerali on monday, nimemsikia Jaji Mihayo akichukulia mfano mmojawapo wa Kufutwa kazi kwa Inspector Aziz, nadhani wakati wa Jemedari Mwl J.K Nyerere..kwa kosa la Kugonga mtu barabarani (TRAFFIC CASE) na akachelewa ku-report kituo cha Polisi despite ya ukuu wake...Mwalim Nyerere alimtimua.!!

  Sasa naomba labda tupate historia zaidi na mikasa zaidi hasa kwa ajili ya "Ilmu".

  Natumaini wadau kina JokaKuu, Kichuguu , Mzee Mwanakijiji na wengineo mtakuwa na habari zaidi.

  Samahani kama ilishaongelewa hapa.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  nachukua siti a mbele, nisikie.
   
 3. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hujalipia umezamia wewe, tutaika "kamuhanda" hapa
   
 4. king kan

  king kan JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,267
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Mi namkumbuka alwatan Mahita.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Usiwe na wasiwasi, nitakusimulia kadri ya kumbukumbu yangu, halafu nitawaachia wengine nao waendeleza. Ngoja nimalize kwanza kazi zinazonipa ugali, halafu nitarudi na rekodi ninayofahamu.
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mie member jamani.

   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ukwelikitugani,

  ..kwanza inabidi uwajue wakuu wa polisi tangu tupate uhuru.

  ..niliwahi kupitia website ya jeshi la polisi ambapo niliona taarifa za ma-IGP na miaka waliyotumikia.

  ..kwa kumbukumbu zangu wakuu wa Polisi ni hawa wafuatao: Elengwa Shaidi, Hamza Aziz, Samwel Pundugu, Philemon Mgaya, Solomon Liani, Harun Mahundi, Omar Mahita, na Said Mwema.

  ..Hamza Aziz alikuwa na kesi ya kukanyaga mtu na gari. sina details zaidi za kesi yake lakini inasemekana iliisha kiajabu-ajabu na baadaye Mwalimu akampeleka ubalozini USA.

  ..Philemon Mgaya alistaafishwa na Mwalimu Nyerere kwa manufaa ya umma. Miaka hiyo that was all the information that was given to the public. Nategemea watajitokeza wachangiaji kueleza ni nini kilisababisha Philemon Mgaya akastafishwa kwa manufaa ya umma.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mimi kwa uelewa wangu mdogo wa hili jeshi letu ni kama hivi

  Tulianza na Eli Shaidi (1964-1970 ) akaja Hamza Azizi ndo huyo anayezungumziwa hapa aliwahi kugonga tena akiwa amelewa (1970-1973 ) then Samson Pandugu (1973-1975 ) huyu sina taarifa zake nyingi ila inasemekana katika ma IGP waliotoka wakiwa masikini wa kutupwa huyu ni mmoja wapo. Halafu kuna Mgaya miaka ya 1975-1980 huyu nadhani bado yupo hai mpaka leo na ni bonge la mfanyabiashara na kuna Liani huyu alifanya miaka ya80 mpaka mwalimu alivyostaafu akaondoka nae, kulikua kuna tetesi kuwa hakua raia pia kama mwenzake aliyemfuatia Mahita ila huyu jamaa alikua ana connections kali Ikulu wakati huo na alitoka akiwa tajiri wa kutosha tu, pia ni katika watu wa mwanzoni mwanzoni mwa miaka ya 90 kufa kwa ikimwi( tetesi) lakini ilikua ni open secret! Akaja Mahundi kipindi chote cha Rais Mwinyi 1985 to 96 I think ndio kwa mara ya kwanza yule msomali akapandishwa cheo kutoka uRPC Kilimanjaro hadi kuwa IGP baada ya kazi nzuri ya kudhibiti nguvu ya Mrema kule, tunajua aliyoyafanya Mahita ikiwemo sekeseke za Mwembechai, Zanzibar alivyowadhibiti CUF kule na kupelekea Tanzania kutoa wakimbizi kwa mara ya kwanza, tunajua kesi ya kuzaa na mfanyakazi wa ndani na alipostaafu kuna tetesi kuwa alitaka kugombea ubunge kule kwao Moro! Wakati wa Kikwete ndo akatuletea huyu shemeji yake kutoka Interpol kuanzia 2006 mpaka sasa hivi.....

  Niko open kwa masahihisho, nimejaribu kuweka historia kadri ninavyoifahamu mimi, aidha kwa masimulizi au kutokana na kusoma sehemu mbalimbali
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Eh eh ehe! ehe! endeleeeeni basi
   
 10. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ngojawaje wajuvi ndugu yangu acha haraka, hapa ndo Great thinkers....
   
 11. MTEWELE G.

  MTEWELE G. Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka sometimes muwe mnawaacha wakapumzika bcoz hata mkiwachambua bado kama kuna uovu hautafutika, na kama kuna mema mbona hamuweki wazi? Ni mtazamo tu
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  1. Kwa Kwanza alikuwa anaitwa Elangwa Shaidi, huyu alistaafu kutokana na umri. Sina uhakika alikuwa na umri gani.

  2. Aliyefuatia ni Hamza Azizi ambaye aligonga mtu na gari la serikali akiwa amelewa. Hata hivyo kwa vile alikuwa ni mtoto wa Mzee Aziz Dosa, ambaye alikuwa ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa Nyerere wakati wa Uhuru, Nyerere akaamua kumhifadhi kwa kumhamishia kwenye ubalozi wa Tanzania huko USA. Kuna binti yake ambaye leo naye ni balozi huko foreign affairs.

  3. Samson Pundugu alistaafishwa na Nyerere ikiwa ni pamoja na Ali Hassani Mwinyi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wakati huo. Hiyo ilikuwa ni response kutokana na mauaji ya wachawi huko Shinyanga. Watu wengi sana alistaafishwa kazi ndani ya jeshi la polisi na wizara nzima ya mambo ya ndani.

  4. Philemon Mgaya nimepoteza kumbukumbu kidogo, ila nadhani aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora au mkuu wa polisi wa Tabora. Nilisoma na mmoja wa watoto wake, na sikumbuki kama alitoka Tabora ndipo akawa IGP au alitoka IGP ndiyo akaenda Tabora. Ila tetesi zilizokuwapo ni ama alipokea au aliomba rushwa ili kutoa kibali cha kuendesha biashara ya ulinzi kwa kampuni y Group 4 Security wakati huo.
   
 13. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Halafu mkuu Kichuguu, sijui kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, huyu Mgaya kuna kipindi alishawahi kuwa ADC wa mwalimu? Najua kuna kipindi fulani Rais alikua na Aide de Camp kutoka Polisi na sio JWTZ kama sasa hivi, embu nikumbushe hapo, as in timeline! Ni kujifunza tu, thanks in advance
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  Kichuguu, gobore,

  ..nadhani Philemon Mgaya alikuwa aide de camp wa Mwalimu, halafu RPC Tabora, na baadaye IGP.

  ..ni kweli kuna kipindi aide de camp wa Mwalimu Nyerere walikuwa ni maofisa wa jeshi la polisi.

  ..kuna ADC[jina limenitoka] wa Mwalimu toka Polisi ambaye baadaye alikwenda kufundisha jeshi la polisi la Zimbabwe.

  NB:

  ..nimesoma kwenye daily news kwamba Col.Makwaia aliyepata kuwa adc wa Mwalimu na Mzee Mwinyi amefariki dunia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ni Kweli, nadhani ilikuwa ni kipindi ambacho mwandishi wa Nyerere alipokuwa ni Hashim Mbita.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
 17. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Hivi Tryphone Maji anaingia wapi kwen ye hiyo list?, ama yeye hakuwai kuwa IGP, ama alikuwa Mkuu wa Police Mkoa wa DAr?
   
 18. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Naona thread imedorora kidogo
  Bwana mkubwa huyu Maji hajawahi kuwa IGP alikkua ni RPC wa DSM tu, tena alikua fisadi wa kutosha nasikia alisettle maeneo ya Kibaha baada ya kustaafu ana bonge la Ranchi la mifugo pale

  Asante JokaKuu kwa linki hiyo imekua useful na nadhani muanzisha mada atakua amepata angalau mwangaza wa alichokua anakitaka! Just kwa kuongeEa ongezea huyo IGP mmoja Liani ndo alikuwa incharge wakat wa ishu ya uhaini ya 80s na alihusishwa na namna kina Hatty walivyotoroka Ukonga wenye data zaidi wataendelea kushusha
  ukwelikitugani gonga hata like mkubwa kama post zimekua useful...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Absolutely, very useful. Ona sasa umeongeza mshawasha kwenye "mnakasha" huu..Hii habari ya "IGP mmoja Liani ndo alikuwa incharge wakat wa ishu ya uhaini ya 80s na alihusishwa na namna kina Hatty walivyotoroka Ukonga " Inavuta hisia sana. Nadhani kama haijapewa airtime jamvini basi ni muda muafaka Jemedari wangu gobole..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  Kituko,

  ..Tryphon Maji alikuwa RPC wa D'Salaam miaka ya 90.

  ..kuna tajiri wa kihindi alikamatwa na kuwekwa ndani central police. sina uhakika aliwekwa ndani kwa amri ya nani. lakini Tryphon Maji na Silvano Adel[katibu mkuu mambo ya ndani] walikwenda central police na kumtoa mhindi mahabusu. habari hiyo ilimfikia Augustino Mrema, waziri wa mambo ya ndani, na yeye akaripoti Ikulu, na kupelekea vibarua vya Maji na Adel vikaota majani.

  ..Tryphon Maji na Silvano Adel wametangulia ktk haki miaka ya hivi karibuni.


  ukwelikitugani, gobore, Kichuguu,

  ..Solomon Liani aliteuliwa na Mwalimu Nyerere, na alitumikia mpaka wakati wa Raisi Mwinyi, ambaye ndiyo alimteua IGP Harun Guido Mahundi, aliyekuwa RPC Arusha.

  ..ukiangalia timeline ya matukio, nadhani wahaini walikamatwa na kutoroka wakati Solomon Liani akiwa IGP. sina uhakika kuhusu wahusika waliochukuliwa hatua za kinidhamu.

  ..kuna kipindi fulani ambapo waziri wa mambo ya ndani, pamoja na mkuu wa magereza walilazimika kujiuzulu. sasa sina uhakika kama walijiuzulu kutokana na kutoroka kwa wahaini, au kutokana na kutoroka kwa majambazi sugu karibia 21 toka gereza/mahabusu ya ukonga.

  ..naomba mwenye kumbukumbu nzuri watusaidie kuhusu lile tukio la majambazi sugu kama Hamisi "nyau", Leloo, na wenzao kutoroka gerezani/mahabusu ilikuwa ni mwaka gani na kama kuna hatua zozote zile zilichukuliwa dhidi ya IGP, waziri wa mambo ya ndani, na mkuu wa magereza.
   
Loading...