Historia ya hospitali ya rufaa ya mtakatifu Fransisco

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
Ifuatayo ni historia ya hospitali ya Mt. Francisco, hospitali teule ya wilayaambayo ilianzishwa mwaka 1921. Mwaka 1921 waliwasili masista wa kwanza wa “Baldegg” kutoka Uswiss(Switzerland) ambapo shirika la Msalaba Mwekundu lilipoanzishwa. Mwaka 1927 ilifunguliwa zahanati yaani Dispensari ya zamani inatumika kama maktaba. Mwaka 1931 ilinguliwa kwa hospitali ya Mtakatifu Fransisco ikiwa na vitanda 30 tu vya kulaza wagonjwa.

Mwaka 1937 ilijengwa wodi ya wazazi. Mwaka 1951 Daktari mmisionari anaanza rasmi kazi yake huko Ifakara. Mwaka 1953 daktari bingwa wa upasuaji kutoka Austria Zams, Dr. Karl Schöpf anakuja Tanganyika na familia yake na anakuwa daktari mpya mmisionari. Mwaka 1955 Ujenzi wa hospitali mpya ya Mtakatifu Fansisco ulianza rasmi.

Mwaka 1957 kilifunguliwa kituo cha utafiti kutoka Uswiss chenye taasisi ya magonjwa ya ukanda wa kitropiki. Mwaka 1960 hospitali mpya ya Mtakatifu Fransisco anafunguliwa rasmi. Mwaka 1961 Tanganyika inakuwa huru chini ya Julius Kambarage Nyerere kama rais wa kwanza. Kwa kuungana na Zanzibar nchi inaitwa TANZANIA. Hospitali ya wakoma "Nazareti" imekuwa makao ya walemavu wengi na waliokuwa zamani wagonjwa wa ukoma.

Mwaka 1967 ilifunguliwa hospitali ya wakoma ijulikanayo “Nazareti” iliyobuniwa na Mhandisi Norbert Heltschl kutoka Tyroler. Ilifadhiliwa na jimbo la Innsbruck chini ya Askofu Dr. Paulus Rusch. Katika mwaka huo huo Rais Julius K. Nyerere alitangaza “Azimio la Arusha”.

Mwaka 1969 Dr. Schöpf anahitimisha kazi yake Tanzania na kurejea Zams. Katika miaka iliyofuata wataalam mbalimbali wa tiba kutoka Uswiss na Ujerumani walichukua nafasi ya ukurugenzi wa hospitali.

Mwaka 1976 hospitali inakuwa chini ya serikali na hivyo kuwa hospitali ya wilaya za Kilombero na Ulanga,mmiliki akibakia kuwa jimbo katholiki la Mahenge Mwaka1993 Dr. Patience L. Kibatala anachukua nafasi zote mbili ya ukurugenzi wa hospitali na ukuu wa idara ya upasuaji akiwa Mtanzania wa kwanza. Mwaka1995 unakuwa mwanzo wa ushirikiano kati ya hospitali ya Zams na hospitali ya Mt. Fransisco.

Mwaka 2004 unanzishwa "Ushirika wa marafiki wa Ifakara" Kama una kumbukumbu nyingine ongezea hapo chini.
 
Gharama juu sana,huduma haziko poa,hawataki kuajiri qualified personnel,wao ni mwendo wa cheap labour tu....
No retention mechanisms hata kwa wale wanaoajiriwa....
 
Gharama juu sana,huduma haziko poa,hawataki kuajiri qualified personnel,wao ni mwendo wa cheap labour tu....
No retention mechanisms hata kwa wale wanaoajiriwa....



Mimi mara ya mwisho kwenda kwenye ile hospitali ilikuwa ni mwaka 2003 nilivunjika mkono nilienda kupiga X ray nilikuwa na miaka 6 mpaka leo cjatia mguu tena pale
 
Back
Top Bottom