Historia ya Hayati Luteni Jenerali Silas Mayunga, Mti Mkavu (1940-2011)

Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi amina.kwa hakika makanda mlikuwa nyie bahati mbaya tumebakia na makamanda jina tu,wengi wao sasa hivi wanajihusisha na ufisadi wa kutisha huwezi amini wameingia hata kwenye uuzaji wa matrecta na kuwa na akauti nje ya nchi trilion 3na kuwata wanajeshi makato yasiyo na kichwa wala miguu watu kama hawa watapiganisha vita kama ulivyofanya wewe na makamanda wenzio kwenye vita ya kagera!!!makamanda wapenda pesa watajali hata kuwapa mafunzo ya kivita vijana wetu!!pesa hiyo watapeleka kwenye akaunti nje ya nchi,sio kama mlivyofanya ninyi,pengo uliloacha ni vigumu sana kuzibika.
 
ufisadi hauna itikadi wala ukakamavu,jamaa walikomboa nchi,walipopewa nafasi nyingine tu wakaharibu.


fisadi mkubwa ni kiwelu, alivuta mkwanja kahama mining akawafukia wachimbaji wadogo wadogo akiwa mkuu wa mkoa wa shinyanga na pia aliuza vita ya kagera mpka akahamishwa kutoka mstari wa mbele na kuwa mkuu wa chuo cha monduli , sababu ya kumhamisha ilitajwa itasemwa baadaye lkn hajiwahi tajwa mpka leo
 
RIP Mayunga, <br />
<br />
poleni watanzania wote kwa kuondokewa na shujaa wa ukweli wa nchi yetu, aliyeulinda uhuru wetu kwa vitendo pale nduli amini alipotaka kutupokonya. kazi yako ilikuwa njema na nakuombea pumziko la amani lenye rehema juu ya rehema<br />
<br />
Jina la Bwana libarikiwe!
<br />
<br />

RIP Major Gen. Silas Mayunga. Vijana wengi wa Mabibo watakosa ucheshi wako.

Mtumishi Miss Judith kama hakuomba rehema akiwa hai huu si wakati wa kuombewa rehema!
 
Wakuu taarifa za uhakika nilizopata kutoka nchini India kuwa mpiganaji wetu shupavu na kiongozi mwadirifu, Meja Gerenali Silas Mayunga (Kushoto pichani akiwa na Gen. Musuguri) hatuko naye tena, amefariki leo katika hospitali ya Apollo New Delhi, India ambako alikuwa amelazwa tangu mwezi, Julai 2011.

Generali Mayunga atakumbukwa kwa mengi kwa jinsi alivyotumikia Taifa letu kwa utumishi uliotukuka, atakumbukwa daima kwa jinsi alivyoongoza mapambano ya vita vya Kagera kumng'oa Nduli Idd Amin.

M/Mungu ailaze roho yake mahali pema. RIP.

289661_241658155864685_187334827963685_807048_6957622_o.jpg


(Picha kutoka Mroki Mroki)

Salute!! I shall always treasure his mighty deeds!!!
 
inasikitisha kuna utitiri wa sikukuu ambazo taifa huacha kufanya kazi kuzitukuza, lakini sio sikukuu ya mashujaa waliotoa roho zao au kuhatarisha maisha yao (kama akina Major General Mayunga) lakini taifa halisimami japo kwa siku moja kuwakumbuka. tufute sikukuu kama za sabasaba, easter monday, boxing day, idd pili nk turudishe sikukuu ya mashujaa.

Rest in Peace Major General Mti Mkavu...ulikuwa juu sana na Idd Amin hatokusahau
 
Mungu awape nguvu hasa hiki kipindi kigumu cha majoz ndg wa malehemu pia watanzania wote mana mchango wako tutaukumbuka daima na yale mazuri uliyo tuachia tutayaenzi.ULALE MAHALA PEMA AMINA
 
KATI ya viongozi ambao nilipenda kusikia kauli zao kuhusu Luteni Jenerali Silas Mayunga, aliyefariki wiki iliyopita, Agosti 5, nchini India, ni Waziri wa zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali (mstaafu) Abdulrahman Kinana.

Kwa nini Kinana? Kwa sababu anajua masuala ya jeshi katika sura mbili. Kwanza kama mwanajeshi; pili Waziri wa Ulinzi. Lakini kubwa zaidi, anafahamiana kwa karibu na Mayunga.

Itakumbukwa Novemba mosi, 1978, majeshi ya aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin yalivamia Mkoa wa Kagera. Uvamizi huo ulimsukuma Mwalimu Nyerere kuashiria ushindi kabla vita kuanza.

Nyerere aliashiria ushindi kabla vita kuanza akisema; "sababu ya kumpiga tunayo, nia ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao." Hakika, kauli hii ilihitaji si tu risasi za kutosha, mizinga au makombora na silaha za kila aina kuisimamia, bali mashujaa wa mstari wa mbele vitani.

Ilikuwa kazi kubwa, na kwa kweli ilikuwa ni juu ya makamanda wa mstari wa mbele kuamua kuivunjia hadhi kauli hiyo ya Amiri Jeshi Mkuu au kuisimamia kufa au kupona ili ibaki kuwa ya ukweli.

Hivyo basi, ni kauli au hotuba iliyopaswa kutetewa, kupiganiwa kufa au kupona ili kuuthibitishia ulimwengu; Amiri Jeshi Mkuu -Rais Nyerere alikuwa sahihi kutangaza uwezo, nia na sababu za kumpiga Amin upo.

Ingawa makamanda wa mstari wa mbele walikuwa na zana za kivita, lakini hotuba ya Mwalimu iliwaongezea silaha ya ziada ambayo ni uzalendo.

Miongoni mwa wapiganaji waliotwikwa dhima hiyo nzito ni pamoja na Luteni Jenerali Silas Mayunga, sambamba na wapiganaji wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Watanzania kwa ujumla, waliotoa ng'ombe hata kuku kulisha wapiganaji uwanja wa mapambano.

Mstari wa mbele katika uwanja wa vita, Luteni Jenerali Silas Mayunga na wenzake, kazi ilikuwa moja tu-kufa au kupona ili kulinda si tu hadhi ya Tanzania, heshima ya wapenda haki duniani.

Ni vita hii ya Kagera ndiyo inayotajwa kumtambulisha zaidi Luteni Jenerali Mayunga ndani ya JWTZ na Jeshi la Uganda. Vita hiyo ilimpambanua ni mpiganaji wa aina gani akiwa mstari wa mbele.

Luteni Jenerali Mayunga ni nani?

Kama ilivyo kwa watu wengi mashuhuri dunia, haikuwa rahisi kumtabiria mtoto mdogo aliyezaliwa Maswa, Shinyanga, mwaka 1940; eti siku moja ataipigania nchi yake kufa au kupona, akiwa katika uwanja wa mapambano ya risasi, mizinga na makombora mazito.

Bila shaka, hata alipokuwa shuleni Bwiru Sekondari, Mwanza, walimu na wanafunzi wenzake hawakujua unyeti wa Silas Mayunga nchini, miaka kadhaa iliyofuatia.

Pengine hata naye hakujua uzito wa uamuzi wake wa kuanza maisha mapya ya kijeshi alipojiunga, na kwa mara ya kwanza na Jeshi la kikoloni, (Tanganyika Rifles) Januari 10, mwaka 1963.

Safari yake kijeshi imegusa nchi za Israel na Canada, akihitimu mafunzo ya kijeshi Julai 26, mwaka 1963 nchini Israeli na miaka 10 baadaye (1973), akafuzu kozi ya unadhimu na ukamanda wa jeshi nchini Canada. Kozi ya Ukamanda wa Juu wa Jeshi alihitimu mwaka 1974 nchini.

Juni 21, mwaka 1995, ni siku ambayo Mayunga alijiwekea rekodi binafsi ya kushika cheo cha juu jeshini, akipandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali na miezi sita baadaye (Desemba 31, 1995) alistaafu.

Mti mkavu akiwa jeshini

Mayunga ni kamanda kiongozi. Amekuwa Mkurugenzi wa Mafunzo makao makuu ya jeshi, Kamanda wa Brigedi ya 202 ya Tabora, na Kamanda wa Divisheni za 20 na 30 za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Huwezi kuzungumzia Operesheni Chakaza wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Idi Amin bila kumtaja kiongozi wa operesheni hiyo ambaye ni Luteni Jenerali Mayunga.

Katika Operesheni Chakaza, Mayunga ndiye aliyekuwa Kamanda wa Brigedi ya 206. Ndani ya Jeshi la Uganda Mayunga ana historia muhimu. Amekuwa Kamanda wa Kikosi Maalumu cha JWTZ nchini Uganda kati ya 1979 na 1980.

Lakini ukiondoa pilikapilika za kijeshi, Mayunga amekuwa Mkuu wa Mkoa Singida mwaka 1977 &#8211; 1978, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria mwaka 1989 hadi 1998 na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) 1998 na 2002, alipostaafu.

Kinana na Mayunga Liberia

Kama nilivyoeleza awali, nimezungumza na Kinana. Amekumbuka mengi kuanzia pilikapilika za kivita za Mayunga akiongoza sekta ya Mbarara, sambamba na jukumu zito la kufundisha majeshi ya Uganda ili si tu kusafisha masalia ya Idi Amin; bali kuliweka upya jeshi la Uganda.

"Wakati ule (vita ya Kagera) kulikuwa na sekta mbili. Sekta ya Masaka ikiongozwa na Musuguri na sekta ya Mbarara akiongoza Mayunga,"

"Anazo sifa nyingi muhimu kama kiongozi. Kwanza, uwezo wa kujichanganya na watu wote. Wanajeshi wote walimpenda kama kiongozi, akiwa anaongoza vikosi vyote sekta ya Mbarara na makao yao makuu yakiwa mji wa Mbarara -Uganda, hapo alikuwa akifundisha majeshi ya Uganda.

"Nakumbuka pia mwaka 1994, nikiwa Waziri wa Ulinzi naye akiwa Balozi wetu katika nchi zote za Afrika Magharibi, Umoja wa Mataifa ulituomba kupeleka wanajeshi wa kulinda amani Liberia.

"Tulipeleka wanajeshi 1,000, nikiwa na Mayunga tuliwatembelea wanajeshi wetu kwa kweli aliwapa hotuba nzuri sana ya kuhimiza uzalendo, wanajeshi wetu walifurahi kumwona na kuzungumza na Mayunga wakitambua sifa yake ndani ya jeshi, akiwa vitani Uganda,"

"Tulikuwa pale siku tano, lakini kikubwa zaidi niligundua kuwa aliweza kuwa karibu sana na watu wa hizo nchi alizokuwa akiiwakilisha Tanzania na hiyo ndiyo sifa yake kuu. Ni mtu wa kuchanganyika na watu wote," anaeleza Kinana.

Mayunga

Nimebahatika kuzungumza na baadhi ya wapiganaji walioshiriki vita ya Kagera. Kwao, Mayunga ni mti mkavu usiochimbwa dawa. Kwa mujibu wa simulizi zao, Mayunga alikuwa akiwajaza uzalendo, ujasiri na kuwaondolea uchovu kila walipokuwa wakisonga mbele kumkabili adui.

Kwa maelezo yao, Mayunga ni mpiganaji aliyedhihirisha kuwa ushindi wa kivita hautokani na kigezo cha silaha bora pekee, bali ni wapiganaji jasiri, wazalendo na hodari katika kupiga hatua kusonga mbele na si hatua za kurudi nyuma-kumkimbia adui.

Huyo ndiye Mayunga ambaye hakufa akiwa uwanja wa mapambano akihangaika kuikomboa nchi yake dhidi ya adui. Ndiyo, hakufa kwa risasi, mizinga wala makombora ya adui vitani.

Pamoja naye, tunawaenzi makamanda wetu waliofia vitani na waliorudi hai, walimsogeza adui nyuma na kuyapa ushindi majeshi ya Tanzania na Watanzania.

Wapiganaji wote kuanzia vikosi vya nchi kavu, maji, anga na intelijensia ya kijeshi (military intelligence) katika JWTZ na nchi kwa ujumla, hatuna budi kusema; ingawa tumepoteza kamanda mwingine aliyesonga mbele mstari wa mbele vitani, mwaka 1978 lakini tunaridhika ametimiza wajibu wake kwetu, raia wenzake.

Ameishi kwa kutii mamlaka ya nchi. Ameishi kwa kutii raia wenzake, ameishi kwa mujibu wa tamaduni za Kitanzania. Huyu si kamanda wa kijeshi pekee, bali ni mpigania haki duniani.

Ingwa tunamlilia lakini tunaridhika, tunashukuru na kujipongeza kwa kugonganisha &#8216;glass' tukisema imewezekana, ametimiza wajibu.

Ewe Luteni Jenerali Mayunga, hakufa kwa risasi, mizinga wala milipuko yoyote pengine kama familia yako ilivyohofia ukiwa vitani lakini sasa umekufa ukiwa kitandani ukitibiwa. Buriani Kamanda Mayunga. Tunasikitika kwa kifo, lakini tunafurahi umetimiza wajibu.


Raia Mwema
 
KWA kuwa sala husaidia, ni bora nikamuombea pepo ya heri kwa mwenyezi Mungu ili Luteni Jenerali Silas Mayunga &#8216;Mti Mkavu' apumzike kwa amani baada ya utumishi wake uliotukuka kwa taifa hili.

Kazi ya Mungu haina makosa. Hili naliamini na wala sipingani na Muumba kuhusu kuwepo kwa kanuni ya siku ya kuzaliwa na ya kufa. Ndiyo maana nimepokea kifo cha shujaa huyo kwa mikono miwili, ila nikitafakari mchango wa heshima wa Mti Mkavu kwa Watanzania nabaini kasoro.

Sote tunafahamu Jenerali Mayunga enzi zake aliweka rehani uhai wake, akatanguliza uzalendo kwa taifa lake, akawa tayari kusimamia oparesheni ngumu zaidi ya kijeshi iliyopewa jina la Chakaza ili kumng'oa nduli Idd Amin wa Uganda aliyewatusi Watanzania na kutaka kudhulumu ardhi yao mwaka 1979.

Nawaza, mtu kama huyu ambaye licha ya kuwa mtumishi mtiifu jeshini na amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Jamhuri ya Kongo, amekufa katika hali gani?

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba mpaka Mti Mkavu anapelekwa nchini India kwa matibabu, mzee huyu alikuwa akiishi maisha ya dhiki sana ambayo kusema kweli ukilinganisha na mchango wake kwa taifa, haulingani hata kidogo.

Watu wenye huruma kama mimi wanaweza kujiuliza, kosa la Jenerali Mayunga kwenye serikali hii lilikuwa ni nini? Je, ni kutumikia taifa kwa uaminifu na moyo wa uzalendo ndiyo dhambi iliyomfanya amalizie vibaya maisha yake au alizubaa kuhujumu mali za umma ndiyo maana alipuuzwa?

Fikra nyepesi zinaonyesha kuwa, serikali imekosa shukrani kwa mashujaa wake, ikitafutwa tafsiri nyingi itakuwa ni kuichosha akili kwa vitu vilivyokuwa wazi. Mti Mkavu hakupewa shukrani kwa mchango wake, inatosha kusema hivyo.

Moja kati ya mifumo mibaya iliyojengwa kwenye nchi hii ni ya kutothamini michango ya kizalendo wa Watanzania kwa ngazi zote, maana ukiachilia mbali Mti Mkavu ambaye amefariki dunia akiwa mwaminifu, kuna wastaafu wengine wameachwa wakiteseka bila msaada wala heshima yo yote.

Hivi karibuni tumewasikia baadhi ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma wakilalamika kupata mafao hafifu, mmoja wapo ni mkuu wa zamani Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mirisho Sarakikya ambaye alisema pensheni ya shilingi 50,000 wanayopewa haitoshi kuendesha maisha.

Inawezekana kwa tafsiri za juujuu mtu asione hasara ya kuwepo kasumba hii mbaya ya kuwatelekeza watu waliotetea taifa na kujitolea utu wao kwa manufaa ya jamii kama wafanyavyo viongozi wa nchi hii, lakini ukweli unabaki kwamba tabia hii inaua moyo wa uzalendo kwa Watanzania.

Somo la utumishi uliotukuka na uamanifu wa mali za umma ambalo serikali inatamani liwaingie Watanzania haliwezi kueleweka kwa vijana wanaoingia jeshini leo huku wakiambiwa au kumuona mkuu wa majeshi wa zamani akikata mitaa na kandambili miguuni.

Wimbi la ufisadi na uhujumu uchumi linalotikisa nchi yetu sasa hivi linatokana na wananchi kushindwa kufahamu faida za uaminifu ni zipi, ikiwa akina Mti Mkavu walioweka heshima ya nchi wameachwa katika hali duni mpaka wanakufa.

Taswira ya Watanzania wengi imewafikisha mahali pa kuamini kwamba nafasi za uongozi na vyeo kama si utumishi wa umma kwa ujumla wake zinaweza kuwa na maana kwao kama watajitajirisha mapema kwa wizi kuliko kusubiri bila mafanikio kuheshimiwa na serikali.

Kwenye nchi hii mafisadi wana heshima kubwa kuliko wazalendo wa kweli. Utajiri usiokuwa na vyanzo una ramani ya utukufu machoni pa watu, kuliko umasikini unaolinda rasilimali za taifa. Jambo hili ni la ajabu sana.

Ukipata fursa ya kufuatilia mifumo ya nchi nyingine zinazoheshimu zana ya uzalendo utabaini kuwa, heshima haiendi kwa watu wasiofuata misingi na sheria za nchi. Ndiyo maana ukienda Marekani kwa mfano, waliokuwa wafungwa wa Vita ya Pili ya Dunia wanavaa beji maalumu za utambulisho zenye nembo ya POW (Prisoners Of War).

Beji hizo za POW zinawawezesha watu hao kujulikana na jamii imekuwa ikiwapa heshima.

Kwa Tanzania, tumeshindwa nini kutambua mchango wa mashujaa wetu na kuwapa beji zitakazowafanya waheshimike kwa kupewa kipaumbele wanapokwenda kwenye foleni za kununua Luku za umeme au hata kwenye zamu za kuingia kumuona daktari, ili waone fahari ya kuwa waaminifu kwa taifa?

Natoa mwito kwa serikali na hasa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ahakikishe kwamba mashujaa wetu, nikimaasha watu wote wanaotoa michango mizuri inayoliletea heshima taifa, wanathaminiwa na si kupuuzwa.

Nashindwa kusema mengi, ila KALALE PEMA JENERALI MTI MKAVU, nitaenzi uzalendo wako!

 
View attachment 244504
Hayati Luteni Jenerali Mayunga Mti Mkavu

Wakuu taarifa za uhakika nilizopata kutoka nchini India kuwa mpiganaji wetu shupavu na kiongozi mwadirifu, Meja Gerenali Silas Mayunga (Kushoto pichani akiwa na Gen. Musuguri) hatuko naye tena, amefariki leo katika hospitali ya Apollo New Delhi, India ambako alikuwa amelazwa tangu mwezi, Julai 2011.

Generali Mayunga atakumbukwa kwa mengi kwa jinsi alivyotumikia Taifa letu kwa utumishi uliotukuka, atakumbukwa daima kwa jinsi alivyoongoza mapambano ya vita vya Kagera kumng'oa Nduli Idd Amin.

M/Mungu ailaze roho yake mahali pema.


KATIKA KUMBUKUMBU :MJUWE KAMANDA LUTENI JENERALI MAYUNGA

View attachment 244492
Musuguri (Kulia) akiwa na Silas Mayunga.Picha hii ilipigwa kipindi walipowasili nchini kutoka Vita vya Kagera

Itakumbukwa Novemba mosi, 1978, majeshi ya aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin yalivamia Mkoa wa Kagera. Uvamizi huo ulimsukuma Mwalimu Nyerere kuashiria ushindi kabla vita kuanza.

Nyerere aliashiria ushindi kabla vita kuanza akisema; "sababu ya kumpiga tunayo, nia ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao." Hakika, kauli hii ilihitaji si tu risasi za kutosha, mizinga au makombora na silaha za kila aina kuisimamia, bali mashujaa wa mstari wa mbele vitani.

Miongoni mwa wapiganaji waliotwikwa dhima hiyo nzito ni pamoja na Luteni Jenerali Silas Mayunga, sambamba na wapiganaji wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Watanzania kwa ujumla, waliotoa ng'ombe hata kuku kulisha wapiganaji uwanja wa mapambano.

Mstari wa mbele katika uwanja wa vita, Luteni Jenerali Silas Mayunga na wenzake, kazi ilikuwa moja tu-kufa au kupona ili kulinda si tu hadhi ya Tanzania, heshima ya wapenda haki duniani.

Ni vita hii ya Kagera ndiyo inayotajwa kumtambulisha zaidi Luteni Jenerali Mayunga ndani ya JWTZ na Jeshi la Uganda. Vita hiyo ilimpambanua ni mpiganaji wa aina gani akiwa mstari wa mbele.

MAYUNGA;Safari yake kijeshi imegusa nchi za Israel na Canada, akihitimu mafunzo ya kijeshi Julai 26, mwaka 1963 nchini Israeli na miaka 10 baadaye (1973), akafuzu kozi ya unadhimu na ukamanda wa jeshi nchini Canada. Kozi ya Ukamanda wa Juu wa Jeshi alihitimu mwaka 1974 nchini.

Juni 21, mwaka 1995, ni siku ambayo Mayunga alijiwekea rekodi binafsi ya kushika cheo cha juu jeshini, akipandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali na miezi sita baadaye (Desemba 31, 1995) alistaafu.
Mti mkavu akiwa jeshini

Mayunga ni kamanda kiongozi. Amekuwa Mkurugenzi wa Mafunzo makao makuu ya jeshi, Kamanda wa Brigedi ya 202 ya Tabora, na Kamanda wa Divisheni za 20 na 30 za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Huwezi kuzungumzia Operesheni Chakaza wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Idi Amin bila kumtaja kiongozi wa operesheni hiyo ambaye ni Luteni Jenerali Mayunga.

Katika Operesheni Chakaza, Mayunga ndiye aliyekuwa Kamanda wa Brigedi ya 206. Ndani ya Jeshi la Uganda Mayunga ana historia muhimu. Amekuwa Kamanda wa Kikosi Maalumu cha JWTZ nchini Uganda kati ya 1979 na 1980.

Lakini ukiondoa pilikapilika za kijeshi, Mayunga amekuwa Mkuu wa Mkoa Singida mwaka 1977 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1978, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria mwaka 1989 hadi 1998 na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) 1998 na 2002, alipostaafu.

View attachment 244493
Mwili wa Lt. Gen Silas Mayunga ukiwa kwenye Jeneza.
View attachment 244496
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka Shada kwenye kaburi la Lt. Gen Mayunga

Luteni Jenerali Silas Mayunga, alifariki Agosti 5, 2011 nchini India,hakufa kwa risasi, mizinga wala milipuko yoyote pengine kama familia yake ilivyohofia kipindi yupo vitani bali alikufa akiwa kitandani wakati wa matibabu.

Ewe Kamanda Mayunga tunakulia ,tunasikitika kwa kifo, lakini tunafurahi umetimiza wajibu.
Walijitoa kwa damu na nyama kuwapigania watoto na wakimama wa watanzania walioteswa na majeshi ya Amin....Gen Mayunga Mti mkavu
 
Back
Top Bottom