Historia ya crypto currency na safari yake huko mbeleni kwenye sarafu ya Bitcoin na nyingine

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,718
Habari zenu JF

mimi ni mmoja wa watumiaji wa sarafu za kidigital kwa jina crypto currency.

Nitapenda kutoa historia ya kwa nini kuanzishwa sarafu hizi ni ilikuwa kwa ajili ya nini na kwa sababu hipi.

Tuna fahamu tokea dunia kuanza mpaka kufika leo mifumo mingi ya malipo ilianza kwa kubadilishana vitu kwa vitu,madini kwa vitu mpaka kufikia njia za pesa tunazo zitumia mpaka leo.

Hila kutokana na dunia kubadilika na wakati leo tuna kitu kinaitwa mfumo wa kidigitali wa pesa ambao leo tuna tumia kwa njia kama za m-pesa,tigo pesa,airtel money, paypal na bank account mobile vyote hivi vina tuweka kwenye mfumo wa kumiliki pesa kidigitali.

Historia ya crypto currency:
Kutokana na watu kuumiza vichwa ni nini mbeleni dunia inataka kulingana na maendeleo yake tuje kwenye upande wa kipesa na malipo. Nchi nyingi pesa zao zinakuwa na nguvu kutokana na kitu kinaitwa Reserve currency(backup currency)

Reserve currency (backup currency):
ni sarafu ya kigeni ambayo inashikiliwa kwa kiasi kikubwa na benki kuu au mamlaka nyingine za fedha kama sehemu ya hifadhi zao za fedha za kigeni. Sarafu ya akiba inaweza kutumika katika shughuli za kimataifa, uwekezaji wa kimataifa na nyanja zote za uchumi wa dunia.

KIUFUPI:

Jambo ambalo limefanya kuanzishwa sarafu hizi za kidigitali ni kwa sababu ya kuunganisha dunia kuwa na mfumo wa mmoja ambao utakuwa na sarafu moja ambayo hiyo sarafu unaweza kutumia kokote duniani kulingana na thamani ya pesa ya nchi yako.

Sarafu ambazo zilianza kuingizwa ilikuwa ni bitcoin

Nini maana bitcoin
Ni mfumo wa malipo dijitali ambao unatumiwa na mamilioni ya watu bila msimamizi wa juu kama Benki Kuu ilivyo katika nchi mbalimbali. Sarafu hiyo huweza kutumika kwa kubadilishana na sarafu nyingine, bidhaa au huduma.

Bitcoin wakati inaanzishwa walitengeneza sarafu ambazo idadi yake ni milioni 21 na matarajio ya kutengeneza bitcoin nyengine mpya ifikapo mwaka 2114,ndio bitcoin zitaongezwa kuendeleza idadi ya bitcoin zilipo fikia.

Wamiliki wa bitocoin mpaka sasa idadi yao ni 18,903,837.5. na data zinavo sema kila siku wanunuaji wa bitcoin kwa siku zina nunuliwa bitcoin 900 kwa siku.

Mpaka mwaka 2021 idadi ya bitcoin ambazo azijanunuliwa ni milioni 2 makadilio.

Bitcoin ilianza kwa thamani ya dola 0.06 mwaka 2010 kwa bitcoin moja.ilikuwa ngumu watu kukubali aina mpya ya pesa hizi kwa sababu ilikuwa bado ijakubalika kufikia mwaka 2015 bitcoin ilianza kupanda kufikia bitcoin 1 =$190.
2016 1= $360
2017 1=$775
2018 1=$3,214
2019 1=$3,385
2020 1=$4,106
2021 1=$28,624

Na kipindi cha mwaka huu bitcoin 2021 ilifikia kupanda 1= $ 64000 ila kwa sasa imefikia usd 45000.

Wanufaika wa sarafu za kigeni ni wengi hata hapa nchini kwetu wapo vijana na wazee walioweza kuliona hili.

Sarafu za kigeni ndio njia mpya ya malipo kwa sasa ya kulipa na kulipwa na pia njia ambayo inatumika kama kuwekeza hisa ya baadae ya thamani ya sarafu.

Makampuni mengi sasa yameshaanza kukubali mifumo hii na moja wapo kama tanzania ili kukabiliana na soko la dunia katika sarafu za kidigitali.

Sarafu za kidigital kwa sasa zinakadiliwa zipo aina zaidi ya 10000 kuendelea na kila siku zinazalishwa aina mpya za sarafu.

Bitcoin ina kadiliwa kuwa inashikilia asilimia 40 ya sarafu zote kutokana na thamani yake kubwa.

Mimi nimeanza kuwekeza ili zikiisha bitcoin niwe nazo kama hisa

IMG_2970.jpg


IMG_2989.png

View attachment 2048335

IMG_2989.png
 
Wamiliki wa bitocoin mpaka sasa idadi yao ni 18,903,837.5. na data zinavo sema kila siku wanunuaji wa bitcoin kwa siku zina nunuliwa bitcoin 900 kwa siku.
I doubt kama hiyo 18.9M ni idadi ya wamiliki!

As far as I know, hiyo ni idadi ya bitcoins zilizopo kwenye mzunguko... yaani circulating supply out of 21M Total Supply.

Na uki-assume Circulating Supply = Holders, itakuwa una-assume kila mmiliki ana wastani wa 1 Bitcoin, jambo ambalo haliwezi kuwa sahihi kwa sababu majority wanamiliki a fraction of Bitcoin.

Kutokana na hilo, idadi ya wamiliki LAZIMA itakuwa maradufu kulinganisha na circulating supply!
 
Mkmi sielwei chochte kuhusu hii kitu.

Kama hutojali naomba unipe japo definition ya kiswahili crrptocurrency ni nini hasa kwa mtu ambae hajawahi kuiskia ?
 
Mkmi sielwei chochte kuhusu hii kitu.

Kama hutojali naomba unipe japo definition ya kiswahili crrptocurrency ni nini hasa kwa mtu ambae hajawahi kuiskia ?
 
Mkmi sielwei chochte kuhusu hii kitu.

Kama hutojali naomba unipe japo definition ya kiswahili crrptocurrency ni nini hasa kwa mtu ambae hajawahi kuiskia ?
Pitia hapa utapata mawili matatu ya kuanzia.

 
Level ya pili utapiga picha kitambulisho chako pamoja na live passport size.
Mkuu kwa ambao hawana passport size vipi wanaweza kufanya mining ?

Hii mining kwamba mfano mpaka kufikawezi wa 7 tufanye mtu amefanya mining mpaka zmefika 20coin.

Ao wanaweza kutangaza kwqmba coin moja ni sawa na labda dola 200 so mtu mwenye 20 coins atakuwa na 4000dollars,ndo itakuwa hivyo au ?
 
Mkuu kwa ambao hawana passport size vipi wanaweza kufanya mining ?

Hii mining kwamba mfano mpaka kufikawezi wa 7 tufanye mtu amefanya mining mpaka zmefika 20coin.

Ao wanaweza kutangaza kwqmba coin moja ni sawa na labda dola 200 so mtu mwenye 20 coins atakuwa na 4000dollars,ndo itakuwa hivyo au ?
Kitambilisho chochote tu kati ya kura, leseni au Nida. Ndio, idadi ya coin jumlisha thamani ya coin ndio utapata kiasi cha pesa.
 
Mkuu tutegemee renec moja kuuzwa bei gani hapo mwezi wa saba kwa uzoefu tu inaweza isipungue USD ngapi per one renec ?
Hakuna anayejua kwa uhakika mkuu. Itategemea na nguvu ya soko. Inaweza kuwa $10, $50 au hata $100
 
Weka akiba ya maneno na nitakuja kukumbusha

Haya mambo ya crypto waachieni wenyewe nyie wakina pangu pakavu fanyeni biashara ya mananasi!! Hao vijana wanaofanya udalali wa hii biashara hata wao hawaijui vizuri!
 
Back
Top Bottom