Historia ya BITCOIN: Uliza chochote nitajitahidi kukujibu

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
7,341
4,045
ku-xlarge.jpg
 
Ndiyo mkuu inauhusika nani? Embu nitoe ukungu ambao upo machoni mwangu.

Mkuu, Bitcoin ni virtual currency, yaani ni pesa katika hali ya soft copy, unaweza kuihifadhi kwenye flash disk au kwenye online wallet, na unaweza kuitumia kama pesa nyingine kulipia huduma na kununua bidhaa hasa mtandaoni. Pia baadhi ya nchi zinapatikana ATM za Bitcoin ambazo unaweza kubadili bitcoins zako na kuwa cash!
 
my question is nawezaje kuzipata bitcoins...???

i heard recently zimepanda sana thamani 1 bitcoin is equal to 1200 usd's kama sikosei

Mkuu, kuna sehem nyingi za kununua Bitcoins, unaweza kununua kwa kutumia debit card yako, lakini mara nyingi ukitumia credit card au debit card inachukua siku nyingi mpaka uje kupata bitcoins zako, njia rahisi kama unataka kununua ingia localbitcoins.com utakuta wauzaji wengi, bei tofauti na njia mbalimbali za malipo, mimi huwa nalipia kwa westernunion ndani ya dakika 20 muuzaji ananipatia coins zangu. Bei inabadilika siku hadi siku, juzi ilipanda mpaka $1300 kwa BTC moja, leo imesimamia $950 kwa hiyo unaponunua kuwa mwangalifu, nunua siku unapoona imeshuka kama hivi, mimi huwa nanunua wakati wa crisis na kuuza inapopanda.
 
toka umeanza hii biashara faida yako inaendaje?? af how can you trap international customers...??
 
Hiii pesa ina uzuri mmoja mkubwa sana, it is untraceable. Yaani ukilipwa au ukilipa hakuna anayeweza kujua amemlipwa au amemlipa nani! Wewe unalipa au kulipwa kupitia anuani ya wallet tuu ambayo haihitaji chochote cha kujitambulisha.
Mfano hii ni anuani 1Mx3kd4WTQu7chDM9qKqttbL6fh9rdzzG5
Akiangalia websites nyingi sasa wanapokea michango kwa kutumia hii pesa ambapo wanaweka anuani yao kwenye ukurasa wa mwanzo.
 
toka umeanza hii biashara faida yako inaendaje?? af how can you trap international customers...??

Biashara inakwenda vizuri mkuu, kuna oportunity nyingi sana kama mtu anafahamu wapi pa kuangalia na pia uwe tayari kurisk. Pia sijawahi kumuuliza mteja wangu wapi anatoka, lakini nina uhakika 99.9% hawatoki Tanzania.
 
Mkuu, kuna sehem nyingi za kununua Bitcoins, unaweza kununua kwa kutumia debit card yako, lakini mara nyingi ukitumia credit card au debit card inachukua siku nyingi mpaka uje kupata bitcoins zako, njia rahisi kama unataka kununua ingia localbitcoins.com utakuta wauzaji wengi, bei tofauti na njia mbalimbali za malipo, mimi huwa nalipia kwa westernunion ndani ya dakika 20 muuzaji ananipatia coins zangu. Bei inabadilika siku hadi siku, juzi ilipanda mpaka $1300 kwa BTC moja, leo imesimamia $950 kwa hiyo unaponunua kuwa mwangalifu, nunua siku unapoona imeshuka kama hivi, mimi huwa nanunua wakati wa crisis na kuuza inapopanda.

Nashukukuru mkuu kwa ufafanuzi wako.
Sasa wewe unanufaika vipi na biashara hiyo?

Embu tupe mchanganuo wa kutosha ili tupate kufahamu.
 
Nashukukuru mkuu kwa ufafanuzi wako.
Sasa wewe unanufaika vipi na biashara hiyo?

Embu tupe mchanganuo wa kutosha ili tupate kufahamu.

Hahahaa, mkuu mbona kila kitu kiko wazi.....kwa mfano nikinunua btc kwa bei ya leo $950 nikauza kesho kwa $1200 hauoni napata faida!! BTW theory ni hiyo, lakini mimi nadeal zaidi na soko lisiloonekana, halitabiriki, haliaminiki lakini ndiyo linalipa!
 
Upatikanaji wa wateja upo kwa kiwango kikubwa?
 
Back
Top Bottom