Historia ya BITCOIN: Uliza chochote nitajitahidi kukujibu

Kama unafahamu kiingereza nikutumie kitabu soft copy cha Bitcoin For Dummies, kinaelezea kila kitu na hutasita kununua bitcoin, unaweza kupokea bitcoin zako had I kwenye mpesa.....hahahahaha woga wako ndio adui yako.
Ntumie mm bab n PM then tusaidiana
 
Kama unafahamu kiingereza nikutumie kitabu soft copy cha Bitcoin For Dummies, kinaelezea kila kitu na hutasita kununua bitcoin, unaweza kupokea bitcoin zako had I kwenye mpesa.....hahahahaha woga wako ndio adui yako.
Ntumie mm bab n PM then tusaidiana
 
WIZI MTUPU.........mara bitcoin mara onecoin, mara sijui D9...... WIZI MTUPU
cryptocurrency zipo nyingi mkuu inayoongoza kwa market capitalization kubwa ni bitcoin zipo nyingine kama ethreum na nk,D9 ni mchezo wa upatu ambao kwa kifupi ni ponzi scheme.
 
Ndugu zangu, siku hizi tunasoma uzi nyingi kuhusu forex, bitcoins, na kadhalika. Naona watu wengi hawaelewi vizuri, wengine wanadanganywa, na wengine wanakataa kabisa hata kujaribu kuelewa kwa kuhofia kwamba ni kitu kigeni sana.

Nimeamua basi nijaribu kueleza eleza zaidi kuhusu topics hizi. Zote ni njia ya kuwekeza na kupata au kupoteza pesa kadhiri ya unapooperate mwenyewe. Pia ni muundo mpya wa biashara na wa kuelewa maisha wa jamii.

Kwanza forex. Nampongeza Bwana Ontario na uzi zake za Forex. Nimemfuatilia sana na sijawahi kuona kwamba anasema uwongo hata mara moja. Anawashauri wengi na wanaolalamika ni wale hawaelewi bado au wanakuwa na tama ya kutajirika haraka. Forex njia nzuri ya kuwekeza pesa, ukiwa unafuata kanuni muhimu kama kuwekeza kwenye plattform halali, kujielimisha kwa kusoma na kuoperate, kufuata akili na si Tamaa ya moyo, na kadhalika.

Bitcoin. Kwa kweli, hapa tunaingia kweye muundo mwingine kabisa. Cryptoeconomy au cryptocoins na hata cryptotokens. Cryptoeconomy imeanza na blockchain, teknolojia mpya ya kidijital 2008. Ndiyo wameitumia kwa ajili ya kuunda Bitcoin, kama pesa ya mtandao. Kwa muda mdefu wengi wameiona kwamba ni mchezo tu, mpaka ghafla wafanyabiashara na matajiri wamegundua wanaweza kuitumia kwa uwekezaji na kwa kutumia kwa jailli ya kununua na kuuza, kama system ya transactions, nk. Ndiyo maana tumefika leo Bitcoin ndiye sarafu ya kidijitali yenye uwezo kubwa (asilimia 48% ya sarafu ya kidijital ni Bitcoin). Zipo zaidi ya sarafu 1300 ya kijidijital, Sarafu ya pili inaitwa Ethereum. Ethereum ni sarafu inaitumika sana kama sarafu ya kidijitali kama Bitcoin na kama sarafu ya kidijitali makampuni ya Blockchain na fintech wanaitumia wakati wanatumia teknolojia ya Blockchain. Hata hivi leo mtu yeyote anaweza pia kununua kuuza na kuwekeza pia kwa Ethereum na cryptocoins tofauti tofauti. Thamani zao unaweza kuziona www.coinmarketcap.com

Nimesoma hapa Jamiiforums watu wengi walipoteza pesa kwa kuwekeza kwenye kampuni za wajanja wanaoahidi faida kubwa na ya baraka. Kwa Kweli hatuhitaji kampuni kwa kuwekeza, tunachohitaji ni kuelewa tunachofanya na wapi kuzifungua crypto wallets na kutumia crypto plattform gani bila kuwapa pesa yetu kwa wajanja. Tunachohitaji ni akili na kusoma na kuelewa biashara hii. Kwanza Kabisa tusiweke pesa yetu ya kuendesha maisha ya kila siks kwenye biashara hii. Tukiweka nyumba au gari au ada ya shule ya watoto, ni kosa kubwa sana. Tumia pesa unaoweza kuifanyia Kazi, kwa kutumaini utaipata faida, lakini kwa kuelewa daima hakuna uhakika asilimia mia kwenye uwekezaji wowote. La pili kwa kununua au kuwekeza kweye sarafu za kidjitali njia za kawaida ni rahisi.

Hatua ya kwanza ni kupata crypto coin electronic wallet kama BTC wallet au ETH wallet. Hizo ni private wallets. Hizo wallets zina password refu sana (encrypted key) na ni ya pekee. Ukipoteza umepoteza kila kitu maana hakuna mwingine anayeijua zaidi ya wewe. Andika popote, na usimpe mtu yeyote kwa sababu yeyote. Uhifadhi. La pili ujiunge na cryptocoin exchange yeyote. Zipo soko mbalimbali na inabidi ufanye Kazi kwanza ya kuelewa ipi inakufaa sababu nyingine ndiyo wanakuwa na experience Africa ya Mashariki na wanakuwa na fees tofauti, na muundo tofauti ya kulipa au kulipwa na credit card, au debit card, au Mpesa au nini..

Exchange places watakupa public wallet. Hapa unaweza kufanya transactions, kununua na kuuza, na kadhalika. Inashauriwa sana cryptocoins zako zihifadhiwe ndani ya private wallet, na uziweke kwenye public wallet yako unachohitaji kwa ajili ya transaction tu, kwa usalama zaidi. Daima bitcoin au crypto coin zako utazihifadhi Katika private wallet yako.

Hata hivi uchumi wa crypto (cryptoeconomy) inakuwa na msingi moja unaoitwa Blockchain. Ukitaka kujua zaidi kuhusu Blockchain na cryptocoins, soma kwenye mtandao. Mimi natumia sana www.blockchaincompany.info kwa habari. Kwanza sababu ya Maelezo mazuri, pia wanarushia Bloomberg Live, na ukiwa member wanakupa Tokens za kampuni bure, na hizo tokens zitakuwa pia kwenye token exchange (cryptotoken) karibuni na utakuwa na faidha kwa baadaye. Pia tovuti ya www.coinmarketcap.com kwa kuangalia soko la kila siku. Tujielimishe. Kwa mfano, tupo wengi tunalalamika benki zetu hawataki kutupatia mikopo yenye masharti nafuu (ingawa ni kweli wengi wanakuja kuomba mikopo benki zetu bila hata business plan!!). Kwa uchumi wa blockchain utaweza kuweka pesa kwenye start up yako kwa kutumia ICOs (Initial Coin Offering) haraka ukiwa umeitayarisha vizuri, bila kuwategemea mabenki…. Soma utaelewa, jifunze ili milango zifunguliwe, jitayarishe kwa mapinduzi wa blockchain katika uchumi na jamii... uwe tayari kwa Blockchain Africa, na cryptocoins za Africa....
 
Iv na wew n mtz

Watu ka wew na Ontario mnanipa shida sana kujua uraia wenu


MNA akili sana

I will follow u
 
de play boy , pengine sijajieleza vizuri kwa hiyo samahani. Mada si uraia wa Ontario au wangu au wake, na akili zetu, haha, mada ni kujaribu kutoa Maelezo zaidi kuhusu muundo mpya wa Blockchain na cryptcoins. Weka mawazo yako hapa kuhusu mada kwanza ili wore tuwe na akili. Tafuta google blockchain Africa na cryptocoin Africa. Iwe wazi lakini kwamba simjui Ontario zaidi ya kusoma uzi zake hapa jamiiforums. Unisaidie napokosea na tuendelee kujenga. Tupo pamoja.

structuralist umeuliza vizuri sana. Katika harakati zangu nimeona asilimia 99 ya watu duniani ingawa wamesikia neno Bitcoin wanashindwa kuelewa ni kitu gani. Na ukiongea kuhusu teknolojia iliopo nyuma ya Bitcoin, maana yake Blockchain, ndiyo kabisaaa wengi sana hawaelewi. Mwenyewe nimetumia kama miezi mitatu mpaka niseme niliweza kujisikia naelewa na naweza pia kuongea kuhusu bitcoin na coins Nyingine za kidijitali, na Blockchain.

Bitcoin ni, kwanza, kama sarafu ya kawaida lakini ya dijitali. Inakaa tu kwenye mtandao na msingi wake ni trust. Trust maana yake jamii tunakubaliana kwamba kitu fulani kina thamani fulani. Tunatumaini karatasi fulani nyekundu ina thamani ya tsh10000 si kwa sababu benki kuu inasema hivo tu ila pia kwa sababu jamii tunakubaliana hayo. Hapo trust palitoweka (Zimbawe miaka za nyuma) thamani ya fedha ilikuwa tofauti ya thamani ya vitu... basi Bitcoin ni sawa na euro au usd au pound au Tsh. Na bitcoin ina usalama kwa sababu ya teknolojia ya blockchain, blockchain ni kama benki kuu tuseme. Inatumikaje?Je naweza kununua kitu dukani na bitcoin? Kwa Kweli bado, ila itafika situ utaweza kutumia. Kwa sasa ni sarafu kwa ajili ya speculation, maana kwa ajili ya uwekezaji sawa na forex, lakini kwenye soko la kidijitali (coinmarketcap.com). Ina maana ukiwekeza unaweza eida kupata fedha zaidi au kupoteza pesa pia. Ina hatari sababu ni speculation maana yake unafikiri itapanda juu au itashuka chini kwa hiyo unaamua kununua au kuuza, na kama uamuzi wako ni maya unaweza kupoteza pesa.

Hata hivi kwa sasa soko la bitcoin ni bullish maana yake inapanda na inapanda. inaweza kushuka, lakini itapanda tena. Unanunua bitcoin (au vipande vya bitcoin) na unaiacha thamani yake ikue siku hadi siku. Mfano... miezi miwili zilizopita imefika mpaka 5000, na imeshuka ghafla mpaka 3500 usd... wengi wamenunua kwa 3500... jana imefika 6000, na leo wengine wameamua kuuza kidogo kidogo ili kurudisha investment Yao kwa hiyo imeshuka mpaka 5848 saizi. Nafikiri itabaki hapa kidogo baada ya muda kidogo itaruka juu ya 6000 tena. Uzuri ni kwamba si lazima uwekeze usd5848, unaweza kuwekeza hata usd 100 ukitaka na utapata asilimia fulani ya bitcoin moja, na faida yako itaongezeka (au itashuka kama btcoin inashuka). Mimi siwezi kukushauri uwekeze au la. Hayo ni kila mmoja bada ya kusoma na kujielimisha na kuelewa. ila mimi binafsi nawekeza kwa sababu nafikiri itapanda na itapanda.

UKIELEWA BITCOIN PIA UTAELEWA KWAMBA UNAWEZA KUWEKEZA BAADAYE KWENYE SARAFU YA KIDIJITALI NYINGINE KaMA ETHEREUM, LITE, RIPPLE, NK. Mimi binafsi lakini nigependa zaidi watanzania wajifunze kuhusu Blockchain na namna gani Blockchain inaweza kusadia nchi ya Tanzania na Serikali yake kupata maendeleo. Nitajaribu niandike kesho kuhusu Blockchain na use cases zake. Asanteni.
 
Sielewi vizuri kwa nini to merge uzi wangu na uzi mwingine kuhusu bitcoin. Kwanza si nia yangu kuongea kuhusu Bitcoin. Nia yangu ni kufafanua namna gani Blockchain economy na mtandao wa cryptocoin inaweza kuwa mapinduzi wa muundo wote wa uchumi duniani kwa kujenga network wa uchumi yenye usalama zaidi na unayepinga rushwa na upotevu wa pesa katika mikono ya wajanja. Pia namna gani wafanyabiashara wanaweza kutumia Blockchain kwa ajii ya kuboresha biashara zao (kuanzia watu wa logistics mpaka wa Bima, benki, n.k.). Naona moderators wanafikiri kila kitu ni Bitcoin.... hata sielewi kama nitaendelea hapa au nitaanza uzi mpya. Basi tu.
 
Mwaka huu baona ndio mwaka mungu kaniandikia nitoke kimaisha ... Nimepata kujua Forex na Leo nakutatana na miujiza mingine ya cryptocurrency.
 
Jee unaweza vipi kufahamu kwamba unalipia fair value pindi unaponunua? pili, kwenye stock market naweza kuthaminisha thamani ya kampuni, nikitaka kuwekeza kwenye fixed deposit naweza kuangalia trend ya interest rate, nikiwekeza kwenye kilimo naweza angalia price trend ya mazao, nikiweza kwenye coca cola naweza ona thamani ya biashara. Sasa hii bitcoin how do i know kwamba nawekeza kwa thamani halisi ya soko?
 
Back
Top Bottom