Good, Natumai wabara watapata kujua mengi humu!Makala hii inakusudia kuonesha historia ya bendera nchini Zanzibar kwa miaka 44 iliyopita.
Una umri gani kijana? Nafikiri unaweza kujua ya ufisadi kwani hayo ndiyo unayoweza kuijuwa!Ama kweli hii nchi inaenda orjojo,bendere hiyo ilianzishwa lini maana ninavyoelewa kwa mujibu wa katiba yetu zanzibar siyo nchi,bali ni sehemu ya nchi ya Tanzania
Jaman hii bendera ya wenzetu visiwani ina rangi kadhaa ambazo kwazo binafsi sijafahamu zinawakili ni so naomba kujuzwa zinawakilisha nini?
Kabla hatujavamiwa na wajerumani, nchi yetu (Bara na Visiwa vya Zanzibar) ilitawaliwa na Sultan wa Zanzibar chini ya Sultan wa Oman. Bendera ya Sultani wa Zanzibar ilikuwa hii hapa chini.
Baada ya mikataba ya Carl Peters and Berlin conference, nchi yetu yote iliwekwa chini ya utawala wa Mjerumani. Mjerumani hakuwa na interest katika visiwa vya Zanzibar, hivyo akaingia deal na Uingereza. Walitaka Uingereza iwape visiwa vya Heligoland vilivyoko North Sea, wao watoe visiwa vya Zanzibar kwa Uingereza. Hivyo Zanzibar ikwa chini ya mweingereza, ambaye aliamua kumwacha sultan aendelee kuula. Bara ikaitwa Deutsch-Ostafrika (German East Africa). Bendera ya mjerumani hapa bara ilikuwa hii.
Kwa Zanzibar kulikuwa na bendera mbili. Ya kwanza ilikuwa ya mwingereza; ilikuwa na sura hii hapa:
Bendera ya pili huko Zanzibar ilikuwa ya Sultan ambaye alikuwa hana uhusiano na Sultani wa Oman tena kwa vile alikuwa chini ya waingereza. Bendara yake ilibadilishwa na kuwa ifuatavyo:
Baada ya ujerumani kupoteza makoloni yake kufuatia kushindwa vita ya dunia ya kwanza, sehemu ya bara iliwekwa chini ya mwingereza. Huyu ndiye aliita sehemu ya bara kuwa "Tanganyika" akimaanisha ili nyika iliyo nyuma ya Tanga. Bendera ya Tanga ilikuwa hii:
Katika kipindi cha utawala mwingereza, tulitumia bendera za aina kama tatu hivi lama ifuatavyo:
Gavana wa kiingereza yeye alikuwa akitumia bendera tofauti kama invyoonyeshwa hapa chini
Kunako May 1961 tulipata madaraka ya ndani chini ya Nyerere. Katika kipindi hicho tukawa tunatumia bendera ya kiingereza zilizoonyeshwa hapo juu na bendera ya madaraka ilikuwa kama ifuatavyo
hata hivyo inaaminika kuwa Nyerere alipendelea zaidi ile bendera ya TANU
Ilivyofika December 1961 tukapa uhuru na hivyo bendera ya mwingereza ikashushwa. Tukapandisha bendera ya kwanza ya Tanganyika iliyokuwa kama ifuatavyo:
hata hivyo baada ya uhuru, tuliendelea kubaki chini ya malkia aliyekuwa anawakilishwa na Governor General, Sir Richard Turnbull; bendera ya Governor General ilikuwa kama ifuatavyo:
Ilipofika December 1962 tukawa jamhuri na hivyo kuondokana kabisa na alama za kiingereza ispokuwa pesa (Siku nyingine nitatoa historia ya pesa zetu). Kwa bahati mbaya sikuweza kupata bendera ya rais mara baada ya kuwa Jamhuri
Kwa upande wa Zanzibar, waliendelea kuwa chini ya mwingereza na sultani hadi december mwaka 1963 ambao mwingereza aliamua kutoa uhuru kwa zanzibar chini ya Sultan. Bendera ya Zanzibar huru ( Sultanate of zanzibar) ilikuwa sura nyekunu na karafuu mbili. Sura halisi ya karafuu haijulikani sawasawa. Ila bendera hiyo ilionekana kama mojawapo ya hizi mbili:
hata hivyo serikali hii haikudumu zaidi ya siku 33, ikapinduliwa kwa nguvu na chama cha ASP. Baada ya mapinduzi, iliundwa serikali ya Jamhuri ya Zanzibar. Mwanzoni, bendera ya Jamhuri ya Zanzibar ilikuwa hii hapa chini
lakini baada ya muda mfupi ikabadilishwa na kuwa kama ifuatavyo huku ikiwa na rangi za bendera ya ASP
Katika kipindi kifupi sana wakati wa machafuko ya mapinduzi yale, Pemba ilijitangaza kuwa ni nchi huru ya jamhuri ya pemba, lakini nadhani walidhibitiwa haraka sana na majeshi ya ASP. bendera ya Jamhuri ya Pemba ilikuwa kama ifuatavyo:
Katika kipindi cha miezi mitatu baada ya mapinduzi, visiwa vya Zanzibar viliunganika tena na bara baada ya kutenganishwa kwa miaka ipatayo 80. Muungano huo ulijulikana kama jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuanzaia wakati huo, bendera ya Tanzania ni kama ifuatavyo:
Ile ya rais wa jamhuri ya muungano iko kama ifuatavyo:
Mwaka 2005, Zanzibar waliamua kuwa na bendera yao. bendera hiyo ni mchanganyiko wa bendera ya mwisho ya jamhuri ya zanzibar na ile ya jamhuriu ya muungano wa Tanzania. Inaonekana kama ilivyoonyeshwa hapa chini.
Rais wa Zanzibar naye akatengenezewa bendera yake ambayo inaonekana kama ifuatavyo hapa chini
Kama nimekosea sehemu yoyote katika mapitio yangu ya historia ya bendera nchini Tanzania, naomba marekebisho. Safari nyingine nitapitia historia ya fedha zetu; najua itakuwa ndefu sana lakini nitaigawa katika sehemu sita Kipingi cha Mjerumani, Kipindi cha mweingereza, Kipindi cha Nyerere, Kipindi cha Mwinyi na baada ya Mwinyi.