Historia ya Aziz Ali

Mkuu Maalim asante kwa simulizi hizi murua, nilikuwa napasikia tuu Mtoni kwa Aziz Ali, sikupata kumjua wala kumsikia mzee huyu!.

Tutafutie na habari za Musa Hassan wa jila la Msasani, na wazee wengine waliolipa jiji letu majina.

P
Halafu amini usiamini; babangu alikuwa anasema amesoma na Azizi Ally wakati hata hiyo 1950 yenyewe alikuwa hajaliona hata jua!!

Najua wazee wetu ni wahongo kishenzi lakini babangu mimi kazidi aisee, dah!

Mkuu malcolm Lumumba, eti mzee wako alisoma na Kwame Nkhurumah na Bi. Mkubwa alikuwa shoga ake na Bibi Titi?!
 
Mkuu Maalim asante kwa simulizi hizi murua, nilikuwa napasikia tuu Mtoni kwa Aziz Ali, sikupata kumjua wala kumsikia mzee huyu!.

Tutafutie na habari za Musa Hassan wa jila la Msasani, na wazee wengine waliolipa jiji letu majina.

P

Na wewe hebu endelea kuunganisha dots za Hamza Aziz na Rose Aziz mpaka kuwa na mgodi wa dhahabu
 
Mtoni mtogani kwa Azizi Ally kumbe kuna Historia mzuri lakn TV na RADIO zetu huwezi kukuta wameandaa documentary ili vizazi na vizazi vifaidike.Make watoto wanaokua sa hv wanamuona DIAMOND NA ZARI Kama wapigania UHURU
Tatizo lako unaskiliza wasafi fm lini utasikia. TBC mbona wanaandaa sana hivi vipindi
 
Utangulizi

Aziz Ali alifariki mwaka wa 1950 miezi michache baada ya kutoka kuhiji Makka. Hata kwa mbali katika maisha yake haikumpitikia kuwa mali aliyoacha nyuma itakuja kutumika katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwanza fedha zake zikitumika wakati wa TAA kisha TANU kupitia mwanae wa kwanza Dossa Aziz. Itoshe kusema tu gari alilomnunulia mwanae Nairobi mwaka wa 1947 kama kiliwazo baada ya kukataliwa katika masomo ya urubani kwa kuwa ni mtu mweusi, ndilo Dossa alilitoa kwa TANU mwaka wa 1954 kwa ajili ya kumsaidia Mwalimu Nyerere kufanya kazi zake kwa wepesi.

Aziz Ali

Aziz Ali amekuja Dar es Salaam mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918) akiwa askari katika jeshi la Wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na Goa mmoja.

Mwajiri wake alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi ndizo alizokuwa akifanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya ujenzi akaajiri mafundi.

Aziz Ali akiwa kijana

Kwa hakika jina lake hasa ni Ali Kidonyo.
Hili ndilo jina lake alilojulikana akiwa mtoto na kisha kijana kwao Tanga.

Hili Aziz alipewa na watu wa Dar es Salaam kwa hisani na wema wake.

Yeye alikuwa akitoa fursa kwa watu kumpa pesa kidogo kidogo kama malipo ya nyumba alizokuwa anawajengea na alikuwa mtu akishindwa kulipa akimpa muda hadi atakapoweza.

Nyumbani kwake mwezi Mtukufu wa Ramadhani alikuwa akitandika nje majamvi na kufuturisha hadi watu 100 asiowajua wakija wanafuturu na kuondoka.

Ndipo wakamwita "Aziz" yaani "Mpenzi." Ikawa wakimtaja jina wanatanguliza "Aziz," yaani "Kipenzi chetu Ali."

Kidonyo jina hili la kwao Tanga likafa kabisa.
Aziz Ali alikuwa mcha Mungu sana.

Alikataa kumwanzisha shule mwanae mkubwa Waziri maarufu kwa jina la Dossa hadi kwanza ahitimu Qur'an.

Hii ikapelekea Dossa kuanza shule darasa la kwanza akiwa na miaka 14 akawa darasa moja na Abbas Sykes mdogo wa tatu kwa rafiki yake Abdulwahid Sykes.
Yuuu wabeja sana paasi,nimejifunza historia nzuri!
 
Paskali, Mussa Hassan "Mgosi" yule wa Simba na Coastal Union?
No ni Mzee Mussa Hassan aliyekuwa akiishi Mikoroshini, Wamakonde wakashindwa kutamka Musa Hassan, wakatamka Mucha Achani ndipo ikageuka Msasani. Beach yake ilikuwa na nyumba 6 tuu, ya Nyerere, Kambona, Bert Shackland, Simbeye, Naburi not uwanja tupu wa Tewa Said Tewa. Mbele ya Mikoroshini kulikuwa na miti ya mikoche ndio asili ya Mikocheni.

Umesahau nyumba ya Sir George Kahama.
 
Halafu amini usiamini; babangu alikuwa anasema amesoma na Azizi Ally wakati hata hiyo 1950 yenyewe alikuwa hajaliona hata jua!!

Najua wazee wetu ni wahongo kishenzi lakini babangu mimi kazidi aisee, dah!
Inawezakana kweli Azi Ali ana mtoto wa kiume nae anaitwa Aziz Ali
 
Ilipoishia story ya mtoa mada inatosha kumuweka Ali ktk kundi la mashujaa kama ulivyosema?au atasemwa tu na wale wanaomjua kua yeye ni shujaa?any way na wewe utupe madini,ushujaa wa Aziz Ali unatokana na nini?
Ardhini kumemeza mashujaa wengi mnoo .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom