Historia ya Algeria na jinsi waarabu walivyowalazimishia watu uislamu afrika ya kazkazini

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Historia ya Algeria
Historia ya Algeria inahusu eneo la Afrika Kaskazini ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Algeria.

Historia ya kale ya Algeria

Historia inayojulikana ilianza na Waberber ambao wametokana na mchanganyiko wa wakazi asilia.

Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye pwani ya Mediteranea. Muhimu zaidi kati ya miji yao ulikuwa Karthago uliopanua utawala wake hadi Hispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini).

Kumbe Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania.

Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walisimama upande wa Roma, hivyo wakapata uhuru wao kwa muda kidogo, lakini wakati wa karne ya 1 KK Roma ilianza kutawala eneo la Algeria moja kwa moja.

Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia zililimwa huko.

Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wa Algeria na Dola la Roma lililoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu katikati ya karne ya 7.

Utawala wa Roma ulivurugika baada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja.

Jeshi la Kaisari Justiniani I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katika karne ya 7 uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.

Uvamizi wa Waarabu karne ya 7

Kuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini, baada ya uhamisho wa serikali ya makhalifa kutoka Medina kwenda Dameski, Waumawiya walikaza jitihada huko Afrika ya kaskazini.

Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu ulikuwa kitovu cha uenezaji. Walipoenea katika Algeria ya leo walirudishwa na Waberber Wakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka 711 Afrika ya kaskazini yote (maana yake nchi za leo za Tunisia, Algeria na Moroko) zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Hapo sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu.

Matokeo hayo yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu, maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu
 
acha chuki haitokusaidia ..........mwenyezi MUNGU ANATUAMBIA KTK KITABU CHAKE KITUKUFUU ( NA WASILAZIMISHWE KUINGIA KWENYE DINI) weka chuki zako mfukoni.
 
Ni hivi nchi za Africa Kaskazini zilikuwa na imani ya ukristo na hata mapapa wa mwanzo walitoka huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom