Historia tunayofundishwa Watanzania ina makosa makubwa

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,389
2,000
Juzi niliona makala moja katika mtandao wa BBC ikisema " Katika nchi zilizoendelea watu wasio na elimu ndiyo wenye vitambi lakini katika nchi zetu za kiafrika wasomi ndiyo wenye vitambi"

niliitafakari sana makala hii ina maana gani hasa kwetu sisi wasomi na nilichokigundua ni kwamba waafrika tuna vyeti lakini uelewa wetu ni sawa na watu wasiosoma katika nchi zilizoendelea.

Sio jambo jepesi kukubali kutoka na ile "pride" tunayoipenda kuilinda lakini ni bora tugundue tatizo na tulitatue kuliko kujifanya halipo ili kulinda heshima kumbe ndiyo tunajidhalilisha.

nikajaribu kutazama historia yetu tunayofundishwa mashuleni je inatujengeaje maarifa?

nilichokiona ni hadithi za mwaka fulani kulitokea tukio fulani basi.

mfano walikuja wakoloni afrika na wakatutawala na tukaelezwa mambo mengi waliyotufanyia lakini jambo moja la kujiuliza ambalo historia haisemi, hivi waliokuja kutoka ulaya na kututawala walikuwa watu wangapi?

Yawezekana walipokuja wakoloni wawili, watatu walipofika kwetu kuna ndugu zetu walikaa upande wa wakoloni na kuwasaidia wakoloni kututawala. Hivyo fundisho kubwa ambalo jamii zetu zilitakiwa kujifunza ni adui wa kwanza aliyesababisha sisi tutawaliwe ni mgawanyiko katika jamii zetu na ili tusitawaliwe tena katika maisha yajayo ni kuwaeleza watoto wetu jinsi ndugu zetu walivyoshiriki kuwakoloni ndugu zao na sio kwa kupata faida kubwa bali kupata vitu vidogo ambavyo walijiona wako juu ya watu wengine.

mpaka leo tumejikuta waafrika tunapoteza rasilimali zetu kwa mtindo ule ule wa baadhi yetu kugawa mali zetu kwa wageni na tunaendelea kwa staili ile ile ya kulaumu wageni tu.

Bado ukija katika historia ya vyama tunaelezwa huko nyuma tulishawahi kuwa na vyama vingi na baadae tukavifuta na kuwa na chama kimoja na baadae tukavifuta mfumo wa chama kimoja na kurudi kwenye vyama vingi.

Hatuwaelezi watoto wetu kwa nini hasa tulikuwa tukifanya maamuzi haya? Je ni changamoto gani tulizokutana nazo ambazo zilikuwa zikitushawishi kubadili mifumo. Matokeo yake tumejikuta tunaenda tunarudia rudia makosa yale yale, changamoto zilezile. Ninaamini kama tungekuwa tukiwafundisha watoto wetu kuwa mwaka fulani tulikuwa na mfumo wa vyama vingi lakini katika utekelezaji wa siasa za mfumo huu tulikumbana na changamoto moja, mbili tatu... na ilipofika mwaka fulani tukaamua kufuta vyama vingi.

tumekaaa na mfumo huu kwa mda huu lakini tukakumbana na changamoto moja mbili tatu na hivyo tukaamua kurudi kule.

Ninaamini historia yetu ingekuwa na mafunzo ambayo watoto wetu wasingerudia makosa waliyofanya watu wa zamani maana wangekuwa wamekuzwa wakielezwa ubaya wa kufanya vile. Historia yetu imebaki ya kutaja matukio, kukalili majina na viongozi, walipozaliwa, walipata utawala lini mpaka lini basi lakini hakuna maarifa zaidi ya kukalili matukio.
 

Masanva Aya

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
448
1,000
Hiyo ni kwa sababu kila kiongozi anataka kuacha historia yake binafsi. Mfano hai , kila waziri akiingia kwenye wizara anafanya mambo yake kama yeye, hivyo hivyo kwa Rais ndo maana nchi haiendi, hakuna malengo ya baadae kama Taifa ila kuna utawala kwenye Taifa. Mfano wizara ya elimu, aisee unachoka, akija waziri huyu anafuata umitashumita , akija mwingine anarudisha umitashumita yaani.....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom