Historia Tamu ya Timu Ya Mbao fc aka Wood fc.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Mbao fc aka wood fc Vijana kutoka Mwanza aka Rock city kwanza niwape hongera kwa kuleta changamoto kwenye soka la bongo tulishazoea Fainali nyingi ni Yanga,Simba au Azam ila leo Mmeonyesha kuwa mnaweza japo ndo matokeo ya mchezo lazima mshindi apatikane.

Mbao fc wana historia ya Kuvutia sana Kwanza Ligi kuu walipanda kibahati tu,Walikua kundi C katika ligi daraja la kwanza(Startimes league) na timu za Geita gold mines,Polisi Tabora,Jkt oljoro na Jkt kanembwe.
Timu zote nne zilikutwa na hatia ya Kupanga matokeo isipokuwa mbao fc hivyo wakashushwa daraja na Mbao fc wakapanda.

Mchezo wa Mwisho wa ligi kuu Vodacom Wangefungwa na Yanga tu wangerudi walipotoka ligi daraja la kwanza matokeo yake wakakomoa na Kuichapa Yanga goli 1-0

Na leo hii kidogo tu wangeandika Historia tena ndani ya nchi hii,msife moyo Mzidi kupambana.
 
kilichonifurahisha Mimi ni wale watoto wa ombaomba fc...(Toto fc)...kushuka daraja...wanajifanya kumkomalia MNYAMA wanasahau mechi zingine..

halafu kizuri zaidi aliewashusha ni omba omba nwenyewe...aka vyura fc..
 
kilichonifurahisha Mimi ni wale watoto wa ombaomba fc...(Toto fc)...kushuka daraja...wanajifanya kumkomalia MNYAMA wanasahau mechi zingine..

halafu kizuri zaidi aliewashusha ni omba omba nwenyewe...aka vyura fc..
Hahahaa aya bana Fifa fc aka Dhl fc
 
  • Thanks
Reactions: GUI
Back
Top Bottom