Historia ni Mwalimu Mzuri: Siku Profesa Kighoma Ali Malima alipoondoka CCM...

mmmh nimejaribu kurudia kusoma ila bado sijaelewa lengo hasa la andiko lako ni nini!

anyway labda uelewa wangu mdogo
Hapana hauko peke yako mi pia sijaelewa...nimetoka kapa!labda ndo kama ulivyosema uelewa wetu....
 
Ndugu yangu Mjengwa, nyakati zote hizo ccm ilikuwa kitu kimoja na hakukuwa na chuki KUBWA miongoni mwa wanachama. Wanachama walijionea fahari kuitwa wanaccm, tofauti kabisa na enzi hii ya msukuma.
You are absolutely right
 
mmmh nimejaribu kurudia kusoma ila bado sijaelewa lengo hasa la andiko lako ni nini!

anyway labda uelewa wangu mdogo
Kumponda nyalandu ndiyo order of the day kwa lumumba fc!!ila ndiyo hivyo tena wanaponda kiuoga uoga maana hata hawajiamini!
 
Ndugu zangu,

Nimekumbushia hilo mara nyingi, kwamba historia ni Mwalimu Mzuri. Hata kama wengine mlikuwa hamjazaliwa, lakini, hakuna marufuku ya kusoma historia.

Tunapochambua haya yanayotokea sasa wengine wetu tunaitazama historia.

Ni ukweli wa kihistoria, kuwa CCM ni zaidi ya Chama, ni taasisi kubwa yenye kugusa maisha ya kila mmoja wetu, hata akiwa nje ya CCM.

Sio tu kwa kusoma historia, nina bahati ya kushuhudia miongo minne ya matukio makubwa ya kisiasa katika nchi hii nikiwa na ufahamu na kiu ya kujifunza.

Nimesoma matukio ya TANU kutikiswa kisiasa, zama za Mwalimu. Nimeshuhudia matukio ya CCM kutikiswa kisiasa, zama za Mzee Mwinyi. Vivyo hivyo kwenye zama za Mkapa na juzi tu Jakaya Kikwete.

Katika wote waliohama CCM na waliotarajiwa wangeitikisa CCM ikayumba sana ni Profesa Kighoma Ali Malima. Huyu alikuwa Waziri mwenye dhamana ya Hazina. Alikuwa msomi na mwenye ushawishi ndani ya Chama chake. Haya ya sasa, ingelikuwa enzi zile, Lazaro Nyalandu ingelikuwa ni jina maarufu kwenye vijiwe vya mtaani tu, wala si jina la kutisha ndani ya CCM.

Kwenye Daily News, Julai 17, 1995, iliripotiwa kama ifuatavyo:
" Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Viwanda, Kighoma Ali Malima, ameondoka CCM na kujiunga na Chama chake kipya cha National Reconstruction Alliance ( NRA).

Malima alitangaza hayo kwenye mkutano mjini Tabora, na anatarajiwa kuwa mgombea Urais kupitia NRA." - Daily News, Julai 17, 1995.

Siku ya pili yake, Julai 18, 1995, Kwenye Daily News, Katibu Mwenezi wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alilipotiwa akitoa kauli juu ya hatua hiyo ya Malima, kwa kutamka.

" Alichofanya Malima hakina maana yeyote kwa CCM!"

Ni nani anayejiuliza leo mchango wa Mzee Kingunge kwenye kutufikisha hapa?

Naam, historia ni Mwalimu Mzuri.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52 ( Whatsapp)
Ni wewe Maggid ndio umeandika hizi pumba au ni wale machotara wako umewaachia hii ID?

Kama ni wewe soma upya thread yako kuna ombwe kubwa la uandishi na uchambuzi.

Mimi nilikuwa secondary school nakumbuka vizuri Malima alikuwa ni mdini tu na hakuwa na impact yoyote zaidi ya kwa wale radical muslims wenzake tu, na baada ya kifo chake wafuasi wake ndio waliivamia CUF na kuipa mlengo wa kidini.

Kama uchambuzi ndio huu basi hata mimi nisiye kwenye tasnia ya habari naweza kuandika makala magazetini.

Hovyoo kabisa.
 
Hapana hauko peke yako mi pia sijaelewa...nimetoka kapa!labda ndo kama ulivyosema uelewa wetu....
Utaelewa vipi wakati wamepewa pesa za kuandika propaganda mitandaoni lakini wamejikuta wapo babeli.

Hizi ndio alama za Mungu anapotaka kuungamiza utawala dhalimu hata watumie mbinu gani huwa haisadii.

Ona mtu mzima kama huyu Majjid Mjengwa leo anavyohadhirika hapa kwenye jukwaa la manguli.

Cc: paskal Mayalla, Mzee Mwanakijiji
 
Katika wote waliohama CCM na waliotarajiwa wangeitikisa CCM ikayumba sana ni Profesa Kighoma Ali Malima. Huyu alikuwa Waziri mwenye dhamana ya Hazina. Alikuwa msomi na mwenye ushawishi ndani ya Chama chake.
Profesa Kigoma Malima=Horace Kolimba=Vifo vya utata. Anayeweza kuelezea zaidi atueleze.
 
Naukumbuka sana huo mwaka ambao Malima aliondoka ccm, nina kumbuka sana hata maneno alio yasema Malima wakati anatoka ccm lakini pia ninakumbuka sana sababu ilio mfanya Malima kutoka ccm na pia kumbukumbu zangu bado zipo vizuri sana za sababu ya Malima kuachia nafasi yake ya uwaziri wa fedha na pia bado nina kumbuka hata mara baada ya kupata habari za kifo chake kule London, nilikua mwanafunzi A level na ulikua mwaka wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Tanzania na nchi jirani yaani Malawi na Zambia walikua wamechagua upinzani kuongoza nchi zao miaka michache kabla yetu. Malima na Mrema waliondoka mwaka mmoja huko ccm, Malima hakutikisa kabisa ccm ila Mrema. Nakumbuka Mrema alivyo gombewa pia kuingia chama kipi; Chadema walimtaka (wakati huo Chadema wala haikua maarufu sana), UMD cha chief Fundikila walimtaka but NCCR-Magezu ikiwa imesheheni wasomi ndio walimpata Mrema baada ya kukubaliana terms and conditions. Malima unampa sifa za BURE, hakua tishio nje ya ccm. Malima aliondoka kwenye uwaziri kwa shinikizo while Mrema aliondolewa uwaziri kwa kosa ambalo ni la kitaalamu tu (alivunja siri za baraza la mawaziri na pia ile ya uwajibikaji wa pamoja) kimsingi hayo mambo walikua wanayajua wasomi tu. Malima Kighoma Ali hakua maarufu zaidi ya uswahiba wake na raia namba 1 wa wakati huo.
 
Hakuna asiyejua upande wako Maggid

Pia usifananishe CCM ya miaka hiyo mpaka Kingunge akatamka hivyo na CCM ya awamu hii

CCM ya awamu hii kwanza iko vipande vipande pili iko hoi kisauti , mwenye sauti ni Mmoja tu.

Wanachama wengi sasahivi Hamna sauti mnagugumia kimya kimya.

maggid yuko sahihi

nyalandu hana impact kwa ccm, au haujaelewa?
 
Naukumbuka sana huo mwaka ambao Malima aliondoka ccm, nina kumbuka sana hata maneno alio yasema Malima wakati anatoka ccm lakini pia ninakumbuka sana sababu ilio mfanya Malima kutoka ccm na pia kumbukumbu zangu bado zipo vizuri sana za sababu ya Malima kuachia nafasi yake ya uwaziri wa fedha na pia bado nina kumbuka hata mara baada ya kupata habari za kifo chake kule London, nilikua mwanafunzi A level na ulikua mwaka wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Tanzania na nchi jirani yaani Malawi na Zambia walikua wamechagua upinzani kuongoza nchi zao miaka michache kabla yetu. Malima na Mrema waliondoka mwaka mmoja huko ccm, Malima hakutikisa kabisa ccm ila Mrema. Nakumbuka Mrema alivyo gombewa pia kuingia chama kipi; Chadema walimtaka (wakati huo Chadema wala haikua maarufu sana), UMD cha bwana Mtikila walimtaka but NCCR-Magezu ikiwa imesheheni wasomi ndio walimpata Mrema baada ya kukubaliana terms and conditions. Malima unampa sifa za BURE, hakua tishio nje ya ccm. MAlima aliondoka kwenye uwaziri kwa shinikizo while Mrema aliondolewa uwaziri kwa kosa ambalo ni la kitaalamu tu (alivunja siri za baraza la mawaziri na pia ile ya uwajibikaji wa pamoja) kimsingi hayo mambo walikua wanayajua wasomi tu. Malima Kighoma Ali hakua maarufu zaidi ya uswahiba wake na raia namba 1 wa wakati huo.
Asante kwa ufafanuzi makini, tulimezeshwa matango pori.
 
Mfundishe historia hajui uyo mtoto mdogo anataka makubwa
 
maggid yuko sahihi

nyalandu hana impact kwa ccm, au haujaelewa?

Ndugu zangu,

Sababu alizotaja Nyalandu zote zinajadilika na haziwezi kuwa za msingi kuhama chama wakati Nyalandu mwenyewe kwa miaka 20 yuko Bungeni kwa tiketi ya CCM, yawezekana kabisa CCM ilipoteza dira Nyalandu akiwa Waziri. Alibaki huko kwa vile alikuwa Mbunge na Waziri na hata fursa ya kugombea urais aliipata. Ningemwona mkweli na shujaa kama wakati ule CCM ikipoteza dira angeng'atuka ubunge na uwaziri wake wa utalii na maliasili.
Naomba kuwasilisha.
 
Kaka Majid ni kweli historia ni mwalimu nzuri,lakini sifa kuu ya historia ni "kila tukio lina Zama zake,na sababu zake"
Ukitaka kujielimisha soma "philosophies and methodologies of studying history"

Umri wa CCM kihistoria bado ni mdogo sana ukilinganisha na uhalisia wa historia za vyama vya siasa Africa..soma historia ya "The true whig party of Liberia" Then rudisha majibu historia imekufundisha nini.

CCM ya sasa haina maana hata Kingunge analijua hilo.
CCM ya Kingunge na Vingunge haipo tena!!

Kile chama cha mapinduzi cha Julius Kambarage Nyerere na Kingunge Ngombale Mwiru,chama cha wakulima na wafanyakazi hakipo Tena CCM ya Leo ni ya Magufuli!!

CCM ya Leo inanunua wanachama!!!!
CCM ya Leo vingunge wanahama!!!
CCM ya Leo ni kama kampuni.

Isingekuwa nguvu ya Dola hakika udhaifu wa CCM ni mkubwa mnooo,upo dhahiri hata watoto wangeuona.

Nimalizie kwa kusema hoja ya kutumia historia kuficha ukweli na udhaifu wa CCM kwa kupuuza vigogo wanaokihama chama ni kujidanganya!!
 
maggid yuko sahihi

nyalandu hana impact kwa ccm, au haujaelewa?
Naamini ana impact na ndio maana mnahangaika sana kufungua threads za "kusema hana impact"

Mtu ambaye hana impact huwa anapuuzwa.

Leo Maggid katoka porini kaja huku kwasababu ya Nyalandu, asingekuwa Nyalandu tusingemuona hapa!

Acheni kujipa Tumaini fake, Chama lenu linawafia.
 
Back
Top Bottom