Historia ni Mwalimu Mzuri: Siku Profesa Kighoma Ali Malima alipoondoka CCM...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Nimekumbushia hilo mara nyingi, kwamba historia ni Mwalimu Mzuri. Hata kama wengine mlikuwa hamjazaliwa, lakini, hakuna marufuku ya kusoma historia.

Tunapochambua haya yanayotokea sasa wengine wetu tunaitazama historia.

Ni ukweli wa kihistoria, kuwa CCM ni zaidi ya Chama, ni taasisi kubwa yenye kugusa maisha ya kila mmoja wetu, hata akiwa nje ya CCM.

Sio tu kwa kusoma historia, nina bahati ya kushuhudia miongo minne ya matukio makubwa ya kisiasa katika nchi hii nikiwa na ufahamu na kiu ya kujifunza.

Nimesoma matukio ya TANU kutikiswa kisiasa, zama za Mwalimu. Nimeshuhudia matukio ya CCM kutikiswa kisiasa, zama za Mzee Mwinyi. Vivyo hivyo kwenye zama za Mkapa na juzi tu Jakaya Kikwete.

Katika wote waliohama CCM na waliotarajiwa wangeitikisa CCM ikayumba sana ni Profesa Kighoma Ali Malima. Huyu alikuwa Waziri mwenye dhamana ya Hazina. Alikuwa msomi na mwenye ushawishi ndani ya Chama chake. Haya ya sasa, ingelikuwa enzi zile, Lazaro Nyalandu ingelikuwa ni jina maarufu kwenye vijiwe vya mtaani tu, wala si jina la kutisha ndani ya CCM.

Kwenye Daily News, Julai 17, 1995, iliripotiwa kama ifuatavyo:
" Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Viwanda, Kighoma Ali Malima, ameondoka CCM na kujiunga na Chama chake kipya cha National Reconstruction Alliance ( NRA).

Malima alitangaza hayo kwenye mkutano mjini Tabora, na anatarajiwa kuwa mgombea Urais kupitia NRA." - Daily News, Julai 17, 1995.

Siku ya pili yake, Julai 18, 1995, Kwenye Daily News, Katibu Mwenezi wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alilipotiwa akitoa kauli juu ya hatua hiyo ya Malima, kwa kutamka.

" Alichofanya Malima hakina maana yeyote kwa CCM!"

Ni nani anayejiuliza leo mchango wa Mzee Kingunge kwenye kutufikisha hapa?

Naam, historia ni Mwalimu Mzuri.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52 ( Whatsapp)
 
Ni ukweli wa kihistoria, kuwa CCM ni zaidi ya Chama, ni taasisi kubwa yenye kugusa maisha ya kila mmoja wetu, hata akiwa nje ya CCM.
Kwa hiyo unakubaliana na wale wanaosema kuwa hiki sio chama cha siasa tena bali wana 'shughuli' zingine!?
Sasa hayo majipu na uvundo anayotumbua JPM yalitengenezwa na chama gani na kuna ubaya gani kwa walioyaona mapema na kuamua kukiacha chama badala ya kusubiri ujio wa mwenyekiti wa sasa ambaye naye alitokea kibahati!
 
Hakuna asiyejua upande wako Maggid

Pia usifananishe CCM ya miaka hiyo mpaka Kingunge akatamka hivyo na CCM ya awamu hii

CCM ya awamu hii kwanza iko vipande vipande pili iko hoi kisauti , mwenye sauti ni Mmoja tu.

Wanachama wengi sasahivi Hamna sauti mnagugumia kimya kimya.
 
Hakuna asiyejua upande wako Maggid

Pia usifananishe CCM ya miaka hiyo mpaka Kingunge akatamka hivyo na CCM ya awamu.

CCM ya awamu hii kwanza iko vipande vipande pili iko hoi kisauti , mwenye sauti ni Mmoja tu.

Ndugu yangu, The Businessman,

sifa moja ya ukweli ni pale unapowekwa mezani kwa mara ya kwanza; Hukataliwa. Na hufika siku hujitokeza, na uhalali wake huanzia tangu siku ile ulipokataliwa. Nimesema ukweli wangu, nikiamini ni ukweli wa kihistoria.
 
Kwa hiyo alichokifanya Nyalandu hakina maana yoyote kwa CCM? (kwa mujibu wa ukweli wa kihistoria )

Kuondoka kwa Nyalandu kwa CCM hii ni tofauti na kuondoka kwa Malima kwa CCM ya wakati ule.
 
Ndugu yangu Mjengwa, nyakati zote hizo ccm ilikuwa kitu kimoja na hakukuwa na chuki KUBWA miongoni mwa wanachama. Wanachama walijionea fahari kuitwa wanaccm, tofauti kabisa na enzi hii ya msukuma.
 
Ni jambo la kusikitisha kweli hata wale walipewa akili na Mungu wanazitumia vibaya tena kwa kuwanukuu wasiostahili hata kunukuliwa na watu wenye akili timamu.
Kwanini watu wanataka tuamini kuwa kila anayehama CCM lengo lake ni KUITIKISA CCM? Kwanini watu wasisimamie dhamira ya mhamaji?
Visa vya hawa watu wote wanaotajwa sijaona hata sehemu moja wakisema wanahama kuitikisa CCM, Nyarandu na wengine wamesema wazi malengo yao ya kuhama CCM, kati ya hayo malengo hakuna hata moja la kuitikisa ccm ife zaidi ya dhamira zao za kuachana na ccm.
Nyalandu na Watanzania walio wengi wanajua kabisa kuondoka kwao ccm hakutakuwa na mtikisiko kwasababu ccm yenyewe imekataa kutoa chance ya kushindana kwa hoja ila nguvu.
CCM mnayosema haitikisiki muwe mnasema ni katika ubira upi huo, hapa mngesema kweli kuwa ccm haitikisiki kwasababu kuna nguvu ya dola nyuma yake, ila kama ni hoja na uwanja ukawa na refa mzuri mbona hata CCM wenyewe wanajua kuwa wangetikisika.
Kama mna chama kinachoruhusiwa kufanya mikutano yake popote pale bila bughudha, mna viongozi karibia nchi nzima wanaitunikia ccm tena kwa malipo ya kodi za Watanzania wote, halafu kuna vyama vingine haziruhusiwi hata kusema wanachokiamini ila kile ccm inachokipenda kukisikia, hebu tuambieni huo mtikisiko utakuwepo hata Kikwete akihama kesho?
Mkitaka mjue ccm inatikisika futeni vyeo vya makada watiifu na kuweka utaratibu mzuri wa kuwapata RC, DC na wakurugenzi kwa ushindani na sio zawadi.
 
Kwa hiyo unakubaliana na wale wanaosema kuwa hiki sio chama cha siasa tena bali wana 'shughuli' zingine!?
Sasa hayo majipu na uvundo anayotumbua JPM yalitengenezwa na chama gani na kuna ubaya gani kwa walioyaona mapema na kuamua kukiacha chama badala ya kusubiri ujio wa mwenyekiti wa sasa ambaye naye alitokea kibahati!
Zaidi ya chama maana yake kinainjinia mpaka kazi za watu wasiojulikana.
 
hakina maana kwasababu wao wanajua uchaguzi wataiba na ndo maana hawashituki
 
Ndugu yangu, The Businessman,

sifa moja ya ukweli ni pale unapowekwa mezani kwa mara ya kwanza; Hukataliwa. Na hufika siku hujitokeza, na uhalali wake huanzia tangu siku ile ulipokataliwa. Nimesema ukweli wangu, nikiamini ni ukweli wa kihistoria.
[HASHTAG]#maggid[/HASHTAG].
Tunajua sana nini kilimtokea mzee malima baada ya hapo,si yeye tu wako wengi hayati Kolimba mzee Sita na CCJ yake na nini kilitokea baadae nguvu ya taasisi maalumu iliingilia.
Kama ulivyosema wakati ni mwalimu na hali kadharika historia, lakini pia ukweli uliokataliwa ukidhihiri hutamaraki toka siku ulipozaliwa.
Safari ya vyama vya upinzani kama taasisi imekuwa ngumu kwani imekumbana dhahiri na taasisi imara ya CCM ikisaidiwa na taasisi za dola, huko nyuma haya yalifanyika kwa siri kubwa bila raia wa kawaida kumjua adui wao wa kweli katika demokrasia ndio maana mikakati yao ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Raia wa leo na vyama vya leo wameshalitambua hili ndio maana CCM imepata taabu sana kuiua CHADEMA,ingawa imefanikiwa kuviua vingi tu huko nyuma.
Matumizi ya mabavu yanayofanyika sasa yameongeza chuki kwa raia huku vyama vikizidi kuchukua tahadhari na kuboresha mbinu za kupambana na hicho chama dola, kikubwa na cha kushangaza kadili siku zinavyokwenda ndivyo taasisi dola CCM inavyozidi kuishiwa mbinu na kufanya matendo yasiyokubarika.
2015 ulikuwa mwaka mzuri sana kwa taasisi dola kujifunza lakini ninavyoona haijajifunza chochote bado inaamini katika matumizi ya nguvu na sio ushawishi.
kitendo kile cha juzi pale Dodoma kimewakera raia matokeo yake yatafuata punde ni hayo tu mheshimiwa kwa sasa nisikuchoshe.
 
Ndugu yangu, The Businessman,

sifa moja ya ukweli ni pale unapowekwa mezani kwa mara ya kwanza; Hukataliwa. Na hufika siku hujitokeza, na uhalali wake huanzia tangu siku ile ulipokataliwa. Nimesema ukweli wangu, nikiamini ni ukweli wa kihistoria.

Kwa hiyo kwenye hoja za Nyalandu kuachana na CCM hakuna ukweli?! Ama nawe unaukataa u kweli ama unajituma kwenye korido za waajiri wako kama overtime tu?!
 
Hakuna asiyejua upande wako Maggid

Pia usifananishe CCM ya miaka hiyo mpaka Kingunge akatamka hivyo na CCM ya awamu hii

CCM ya awamu hii kwanza iko vipande vipande pili iko hoi kisauti , mwenye sauti ni Mmoja tu.

Wanachama wengi sasahivi Hamna sauti mnagugumia kimya kimya.

Mkuu CCM ni zaidi ya uijuavyo wamepita maraisi wengi na chama kinaendelea hata BWANA YULE nae atapita na CCM itabaki kuwepo kama ilivyokuwepo, Muda ni muamuzi mzuri sana.
 
Back
Top Bottom