Huwezi kupambana na ccm hata siku moja, hata wanaohama wanajuaNdugu zangu,
Nimekumbushia hilo mara nyingi, kwamba historia ni Mwalimu Mzuri. Hata kama wengine mlikuwa hamjazaliwa, lakini, hakuna marufuku ya kusoma historia.
Tunapochambua haya yanayotokea sasa wengine wetu tunaitazama historia.
Ni ukweli wa kihistoria, kuwa CCM ni zaidi ya Chama, ni taasisi kubwa yenye kugusa maisha ya kila mmoja wetu, hata akiwa nje ya CCM.
Sio tu kwa kusoma historia, nina bahati ya kushuhudia miongo minne ya matukio makubwa ya kisiasa katika nchi hii nikiwa na ufahamu na kiu ya kujifunza.
Nimesoma matukio ya TANU kutikiswa kisiasa, zama za Mwalimu. Nimeshuhudia matukio ya CCM kutikiswa kisiasa, zama za Mzee Mwinyi. Vivyo hivyo kwenye zama za Mkapa na juzi tu Jakaya Kikwete.
Katika wote waliohama CCM na waliotarajiwa wangeitikisa CCM ikayumba sana ni Profesa Kighoma Ali Malima. Huyu alikuwa Waziri mwenye dhamana ya Hazina. Alikuwa msomi na mwenye ushawishi ndani ya Chama chake. Haya ya sasa, ingelikuwa enzi zile, Lazaro Nyalandu ingelikuwa ni jina maarufu kwenye vijiwe vya mtaani tu, wala si jina la kutisha ndani ya CCM.
Kwenye Daily News, Julai 17, 1995, iliripotiwa kama ifuatavyo:
" Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Viwanda, Kighoma Ali Malima, ameondoka CCM na kujiunga na Chama chake kipya cha National Reconstruction Alliance ( NRA).
Malima alitangaza hayo kwenye mkutano mjini Tabora, na anatarajiwa kuwa mgombea Urais kupitia NRA." - Daily News, Julai 17, 1995.
Siku ya pili yake, Julai 18, 1995, Kwenye Daily News, Katibu Mwenezi wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alilipotiwa akitoa kauli juu ya hatua hiyo ya Malima, kwa kutamka.
" Alichofanya Malima hakina maana yeyote kwa CCM!"
Ni nani anayejiuliza leo mchango wa Mzee Kingunge kwenye kutufikisha hapa?
Naam, historia ni Mwalimu Mzuri.
Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)