Historia na mbinu za ushawishi za kueneza ushoga kupitia makundi yenye nguvu ya fedha na intelijensia dunia.

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,779
2,000
Historia ya Ushoga

Historia: Kwa ufupi tu, mapenzi yaJinsia moja hasa jinsia ya kiume yamekuwa yakipigwa vita miaka nenda miaka rudi katika maeneo mbalimbali duniani. Tamaduni, sheria na dini zimekuwa zikipingana na ushoga kwa sababu sio jambo la asili. Mnamo karne ya 12, kanisa katoliki lilipiga marufuku waumini wake kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga). Kabla ya hapo, ushoga haukuwa kitu cha kujadili, ulipuuzwa. Lakini marufuku za kidini na kisheria zilianza kuwekwa pale ushoga ulipoanza kuota mizizi katika jamii.
Wataalamu wa tiba mbalimbali, madaktari na wanasaikolojia wamekuwa wakishindana kufanya tafiti juu ya ushoga; sababu, chanzo na tiba. Baadhi ya wataalamu wameona kuwa ushoga sio jambo la asili, huku wengine kama Dr. Sigmund Freud wakiona kuwa ushoga ni jambo la asili na hakuna sababu ya kutafuta tiba wala kuwatungia sheria za kuwakataza watu kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Hata hivyo kwa kipindi kirefu ushoga uliwekwa kwenye kundi la maradhi ya akili (psychological disorders).

Ilipofika mwaka 1973, taasisi ya magonjwa ya akili ya Marekani (American Psychiatrist Association) iliondoa ushoga kwenye kundi la maradhi ya akili, hii ilifuatiwa pia na ushirika wa saikolojia wa hukohuko marekani (American Psychology Association) ulipouondoa ushoga kwenye kundi la matatizo ya kisaikolojia mwaka 1975. Kwa hiyo katika marekani, ushoga ukatolewa kwenye maradhi ya akili, na vilevile kwenye matatizo ya kisaikolojia. Uamuzi huu haukufanywa kwa sababu za kitafiti kama taaluma za kitabibu zinavyoelekeza bali kwa ushawishi wa kilaghai (lobying) na mashinikizo kutoka makundi ya mashoga huko marekani.

Mnamo mwaka 1990, shirika la afya duniani, WHO nalo likafuata mkondo wa kuondoa ushoga kwenye kundi la maradhi ya akili.

Dunia na ushoga.

Katika kitabu chake cha Conspirators Hierarchy, mwana intelijensia Dr. John Coleman anaeleza kwa kifupi tu namna serikali za marekani na uingereza zinavyofanyakazi kwa mashinikizo ya makundi ya siri, yakiwemo makundi ya mashoga. (Homosexuals). Makundi hayo ya (homosexuals) wamejiingiza katika makundi maengine ya siri kama vile, Order of st John of Jerusalem, Bachofen, Royal Institute for International Affairs (RIILA), Illuminati, Bilderbelgers, Trialterals, Freemasonry, Round Table, Cini foundation, Club of Rome, The Fabianist (waanglikana), Council of Foreign Relations (CFR), Zionist, Hellfire clubs, The Venetian Black Nobility, The Mont Pelerin Society, Bolshevism-Rosicrucianism, Rothchildren of Europe. Nk.

Yapo makundi mengi yenye nguvu ya fedha na intelijensia. Nimependa kunakili orodha hiyo ili ifahamike kuwa sio kitu rahisi tunapozugumzia ushawishi wa makundi haya katika serikali kubwa za dunia. Tunaweza pia kuwaongeza Jesuits Fathers (wakatoliki) ambao hawakutajwa na Dr. Coleman. Ni makundi ambayo serikali za dunia ya tatu hazifui dafu kupambana nayo. Mara nyingi sisi watu wadogo tunanufaika na/au kuathirika pale makundi haya yanapokinzana au yanapoafikiana katika kazi zao, ndio pale unapoona sasa kanisa la Anglican linakubali ushoga, na katika kuliingilia kanisa katoliki tunaona papa Benedict anajiuzulu na anaingia papa Francis na kuweka rekodi ya kuwa 'Mjesuits' wa kwanza kushika wadhifa wa upapa. Ni mapambano tu.

Sasa; ushoga ulianza kwanza kukubalika (acceptable), maana yake katika mataifa hayo ushoga ulikubalika na kuwa sehemu ya maisha ya kawaida. Pili ukatungiwa sheria (legal), maana yake hutakiwi kuwapinga, la! Utahukumiwa. Lakini si hivyo tu, sasa hivi unatangazwa na kuhamasishwa kupitia vyombo mbali mbali vya magharibi. Mbinu kadhaa zinatumika kuhamasisha ushoga, Moja! Kupitia filamu na muziki, mbili kupitia vitabu vya nchi za magharibi na kuzuia vitabu vya nchi za Asia ya Kati (Arabia, Armaic) au 'semitic books'. Tatu kupitia dini (anglican church) kwa udhanio wa uratibu wa "The Fabianists". Nne kupitia wataalamu wa tiba (madaktari na wanasaikolojia), tano kutumia intelijensia ya habari, sita kutumia tasisi za misaada

Kushugulikia suala la ushoga linahitaji mashirikiano ya vyombo na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali na kwa umakini wa hali ya juu sana kutokana na miingiliano ya sheria mbalimbali mfano sheria zinazohusu faragha,usiri,haki za binadamu,uhuru wa mtu na zingine nyingi tu

Suala hili si la kutamka tu kirahisi rahisi tu katika majukwaa mbalimbali bali ni suala kuzisoma tafiti mbalimbali zilizofanyika kuhusu ushoga nini ni hitisho la hizo tafiti na uwezo wetu kupitia taasisi mbalimbali kushughulika na suala la ushoga na namna gani kama nchi kuweza kupunguza na kama si kumaliza kabisa suala la ushoga nchini
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,533
2,000
Mwanadamu kamwe hawezi kubaki salama kwa kukidhi kila hitaji la nafsi yake.....

Mwanadamu hawezi kubaki salama kwa kutoka nje ya njia za aliyemuumba!!.....

Kila kitu kilichoundwa kina maelekezo ya jinsi ya kukitumia...kwenda kinyume na maelekezo hayo ni kuharibu hicho kitu......

Hata Muumba alipomuumba mwanadamu alimpa na maelekezo ya namna ya kuishi!!!....

Hilo jambo halipo kwenye utaratibu wowote wa maisha hapa duniani....si kwa wanyama wala wanadamu!!!!....hivyo basi wanaofanya hivyo na wanaoshabikia hilo ni kwa utashi wa nafsi zao.....lakini kwenye jamii ya waungwana ni kwamba wapo kwenye kiza cha upotovu na madhara yake watayaona!!...hata kabla ya Mungu kuwahukumu!!.....

NB:
Mungu hamkatazi mwanadamu jambo isipokuwa lenye madhara kwake!!....
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,394
2,000
Tatizo la ushoga ni kuwa linaua vizazi, yaani unakuta hakuna watoto watao zaliwa kutokana na ushoga, na Mungu aliuumba ulimwengu ili kujazana. Sasa hao mashoga hata kama mtu anawatetea je watoto wa kurithi vizazi watatoka wapi?
 

Lucky Star

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,020
2,000
Nasikia kuna wanyama jamii ya ngedere tangu kuzaliwa kwao hadi kufa hafanyi kosa la kuingiza kiungo chake cha SIRI kwenye kiungo cha mwenzie kisichoruhusiwa kwa kuzaliana.

Leo binadamu tunayeambiwa amejaliwa utashi na ufahamu kuliko viumbe wengine anafanya haya.

Watafiti(siyo wale uchwara) wanatakiwa kurejea tafiti zao
 

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
4,056
2,000
Labda wale " monks" waliokuwa wanajifungia kwa kusali . Fanya utafiti huenda mambo yalianzia pale .
 

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
4,056
2,000
Hao jamii ya ngedere wangekuwa na utashi wangejaribu ili waone kuna nini . Binadamu kwa kutumia utashi wao walijaribu wakaona kuna joto la ziada . Basi ni chaguo la mtu kuchagua aina ya starehe wanayotaka .

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom