Historia moja imebaki intact; hakuna Rais aliyefanikiwa kurithisha kiti cha Urais kwa amtakaye

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,842
Katika historia ya Tz, jambo moja limekuwa linatokea mara kwa mara.

Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kumuweka anaemtaka anapoondoka.

Wengi walihisi Magufuli atatuwekea mtu wake akimaliza mda wake but haikutokea.

Nyerere alimtaka Salim, akatokea Mwinyi.

Mwinyi akamtaka Malecela, akaibuka Mkapa.

Mkapa akamtaka Kigoda, akashindwa na mtandao wa Kikwete.

Kikwete akamtaka Membe, akaibuka Magufuli.

Magufuli hatujui alikuwa na nani kampanga kichwani mwake Ila now tuna Samia.

Nna uhakika hata chaguo la Samia halitapita; ataibuka mwingine dakika za mwisho.

Hii ndo Tanzania. Ukipanga hivi the 'ancestors' wanapangua.
 
Back
Top Bottom