Historia inatuambia mauaji hayakuwahi zima mapinduzi Ila yalichochea mapinduzi ya kijamii

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,184
11,201
Historia inatukumbusha Kuwa mauwaji ya Wana harakati hayakuwahi zima mapinduzi ya kisiasa ktk jamii Ila yalichochea mapinduzi makubwa na umwagaji mkubwa wa dam na mwisho ushindi.

Mauwaji ya kikatili Kwa wana wa Taifa la Israel na kutaka kuwaondosha juu ya uso wa dunia yalizaa Taifa lenye nguvu na akili ktk USO wa dunia kiasi hata maadui zao walijifunza toka kwao.

Huko Marekani mauwaji na manyanyaso ya MTU mweusi yalifika tamati Kwa MTU Mmoja Martin Luther kufanya hotuba ambazo mwisho ziliwafanya Kuwa huru ktk Taifa Lao na mwisho Marekani kuongozwa na MTU mweusi.

SA watu weusi waliuwawa kama mbwa na kuteswa kiasi hata Yule alikuwa akiwatetea alifungwa maisha Ila mwisho alitoka na Kuwa Rais wa Taifa Hilo.

Libya Taifa tuna ambiwa watu wake walilipwa hata pasipo kufanya KAZI Ila dhuluma na Kuwa Tesa wale walisema vibaya serikali hasa watu kupotea kulifanya jamii ya watu kujikisanya nakujiuliza nini kinatula na ndipo wakagundua serikali Yao ndio inawatafuna kupitia specia unity chini ya Ghadafi. Jambo Baya kabisa undugu na ukabila ndani ya serikali ukaligawa Taifa watu wakasema potelea pote Bora tulale msituni kuliko Kuwa na kiongoz anaye tuchinja kama kuku ktk Banda lake. Na hivyo ndivyo serikali ya Libya ilivyo anguka na kumaliza kiongoz wao Kwa mikono Yao.

Historia ina tuambia hata baada ya miaka mingi SASA kupita kule Kongo Patric Lumumba ambaye hata kaburi halionekani Ila cheche za mapinduzi zinalipuka mpaka leo.

Rwanda ni darasa la chuki ndani ya Raia Kwa miongo kadhaa ilifanya siku moja wa hutu na Watusi kuchinjana kama kuku pasipojuwa nini kimewakumba. Hadi Leo cheche za mauwaji Yale zina litesa Taifa pamoja na kamati za maridhiano Ila bado watu wanayao mioyoni. Chuki haijawahi Jenga Taifa Ila kuliangamiza Taifa.

Huko Syria nchi imegeuka magofu Kwa tamaa ya MTU Mmoja kukitaka kiti milele. Hali sii hali.

Iraq Sadam Hussein akijipa KAZI yakutoa roho wanao pinga au kusema vibaya utawala kuliwaweka ma elfu ya wa Kurd Kuwa kuku wa kafara Ila mwisho naye akanyongwa sokoni. Dam inatabia yakulipiza na dam inatabia yakumfanya MTU Kuwa Hana akili zake za mwanzo kukosa rafiki na mwisho kutanga tanga ktk USO wa dunia.

Dhambi ya kumwaga dam humfanya MTU Kuwa anaona maluwe luwe ndio maana Mungu akamtokea Kaini na kumeambia Dam ya ndugu yako ina ni lilia ardhini. Kumbe unapo uwa zile roho hazilali mpaka haki Yao ipatikane.
Ndipo mwenyez Mungu akasema Usiuwe au kumwaga dam isio na hatia. Asante
 
Maneno ya binadamu dhaifu, wewe ni kiumbe dhaifu mno, unaishi kwa misemo na kutoa mifano hata usioielewa, a real man fights na haishi kwa misemo ya kingesengese, huo ni udhaifu, ....
 
Japo nimkumbuka Ben Saanane nashikwa hasira na wewe lakini kwa somo la leo naomba umueleeze jiwe kwasababu upo karibu nae na bado anashupaza shingo wakati wewe kijana wake umeshabadilika
 
Back
Top Bottom