Historia inapiga king’ora kwa suala la Wamachinga duniani, nani anasikia?

Mkuu THE LOST,
Hawa jamaa wako smart, kwasababu wanajuwa yanayoweza kuwakuta kwa mfumo walioujenga ambao siyo rafiki kwa wanyonge ambao ndiyo wengi, tayari waliishajiandaa zamani kwa kutengeneza mfumo mwingine (wameuficha kwenye madroo) ambao utatumika endapo Wamachinga watafanya mapinduzi ya pili ya Marxism. Mfumo huo mpya wameutambulisha kwa jina la NEW WORLD ORDER, wewe unadhihirisha kwa mchango wako huo kuwa ni Mwanazuoni mzuri sana, hivyo fuatilia hiyo New World Order, ni hatari kuliko mfumo tulio nao hivi sasa ambao wanyonge hawana chao wala sauti. Wakati fulani nakubaliana na wewe kuwa dawa inaweza kuwa ni WW tu.
Tunakaribia vita kubwa sana kuwahi kutokea katika historia.
ARMAGEDDON!
Kabla ya vita hiyo haki zitavunjwa sana na mambo ya kutisha,ubinadamu ukiwekwa kando kwa muda!Ndio tunaelekea huko.
 
Hahahaaa... mkuu, wewe kweli mfuasi wa Marxism.
Vita vya tatu vya dunia ni muhimu Sana katika kubalance nguvu za kiuchumi, kisiasa na kijeshi ili angalau tujikwamue. Afrika na mataifa ya Asia yamekuwa yakijiendea bila visions, wahuni wachache wanafaidi rasilimali za nchi kwa kigezo Cha usomi na exposure. We have to fight in order to determine our fated future.
 
Eti wamachinga wako dunia nzima! Machinga wasioratibiwa wako nchi masikini tu. Nchi zilizoendelea na zinazotumia teknolojia ya juu zinatumia taratibu za kieletroniki, uharibifu wa rasilimali kidogo, kuzalisha zaidi kuliko sisi na zina mifumo thabiti ya kukusanya kodi. Zina mifumo ya afya ya jamii inayohakikisha jamii inalindwa!!

Hakuna kitu kitatokea bila wanufaika wa machinga kutaka! Unachodhani watafanya hawataweza kufanya kwa kujiita ni kundi muhimu la wapiga kura!! Labda wasubiri kuadhibu wanasiasa - hawawezi kuleta vita!!

Zaidi. Hatuwezi kuwa na taifa ambalo kila pembe ya barabara ni kijiwe cha mama/baba lishe, banda la mitumba, wachoma mahindi, chai nk. Juu ya mitaro ya maji machafu!!

Point yangu ni kuwa turuhusu umaching huku ukiratibiwa!! Haiwezi kuwa kila machinga aamue anataka kufanya nini wapi na iwe hivo tu!
 
Mkuu THE LOST,
Hawa jamaa wako smart, kwasababu wanajuwa yanayoweza kuwakuta kwa mfumo walioujenga ambao siyo rafiki kwa wanyonge ambao ndiyo wengi, tayari waliishajiandaa zamani kwa kutengeneza mfumo mwingine (wameuficha kwenye madroo) ambao utatumika endapo Wamachinga watafanya mapinduzi ya pili ya Marxism. Mfumo huo mpya wameutambulisha kwa jina la NEW WORLD ORDER, wewe unadhihirisha kwa mchango wako huo kuwa ni Mwanazuoni mzuri sana, hivyo fuatilia hiyo New World Order, ni hatari kuliko mfumo tulio nao hivi sasa ambao wanyonge hawana chao wala sauti. Wakati fulani nakubaliana na wewe kuwa dawa inaweza kuwa ni WW tu.
Yaani ukiweka haya ma new world order napuza hata kusoma andiko lako
 
Eti wamachinga wako dunia nzima! Machinga wasioratibiwa wako nchi masikini tu. Nchi zilizoendelea na zinazotumia teknolojia ya juu zinatumia taratibu za kieletroniki, uharibifu wa rasilimali kidogo, kuzalisha zaidi kuliko sisi na zina mifumo thabiti ya kukusanya kodi. Zina mifumo ya afya ya jamii inayohakikisha jamii inalindwa!!

Hakuna kitu kitatokea bila wanufaika wa machinga kutaka! Unachodhani watafanya hawataweza kufanya kwa kujiita ni kundi muhimu la wapiga kura!! Labda wasubiri kuadhibu wanasiasa - hawawezi kuleta vita!!

Zaidi. Hatuwezi kuwa na taifa ambalo kila pembe ya barabara ni kijiwe cha mama/baba lishe, banda la mitumba, wachoma mahindi, chai nk. Juu ya mitaro ya maji machafu!!

Point yangu ni kuwa turuhusu umaching huku ukiratibiwa!! Haiwezi kuwa kila machinga aamue anataka kufanya nini wapi na iwe hivo tu!

Revise post yangu upya uone kama sikuongelea kwa msisitizo juu ya kuwaratibu, tena nikarudiarudia kusema waratibiwe kwa sera, sheria, kanuni, miongozo badala ya matamko ya dharura tu wakati tatizo lenyewe siyo dharura lipo nasi tangu 1985 nk, tena nikatoa timeframe ambapo mara kadhaa waliondolewa lakini wakarudi. Aidha, kwenye msitari wako wa kwanza wa para ya kwanza unakubaliana nami kwamba wapo bila kuratibiwa kwenye nchi masikini.

Lakini nilitoa mfano wa Korea Kusini ambayo kimsingi haijapishana sana na Tz kiumri (1950 kwa 1961 miaka 11) Wamachinga wake waliokimbilia nje ya mipaka wanaiingizia 30% ya GDP. Kenya 16% ya GDP. China ambayo haijapishana sana na Tz kwa umri (1949 kwa 1961 miaka 12) ina mitaa kama ya mtaa wa Congo Kariakoo kibao tu, kwa sababu China imewekeza kwenye idadi ya watu hivyo wako wengi kiasi kwamba serikali haiwezi kuwapa ajira wote hivyo wengi wao kujikuta Umachinga (kujiajiri) ni mojawapo ya mikakati ya kujikwamua bila kuhitaji mkono wa serikali na leo kama South Korea, China ina Wamachinga Afrika wanaochoma mishikaki tu na kazi zingine zinazoweza kuwapa riziki zinazoweza kufanywa na Watz, na hapa tunahitaji mkono wa serikali unaowaelemea Wamachinga wetu nao kwa usawa huo huo uwaelemee Wamachinga wa Kichina na Kinigeria pia waliopo nchini, watafutwe washughulikiwe maana hawafanyi Umachinga directly bali kwa kujificha nyuma ya Wamachinga wetu. Sasa, South Korea, China, Nigeria nguvu zao unazilinganisheje na nguvu za Tz?

South Africa Xenophobia mara kwa mara inaendeshwa na Wamachinga na South Africa bajeti yake ya 2021-2022 imefika ZA R1.95tr sisi Tz bajeti ya 2021-2022 ni Tzs.34.88tr, sasa South Africa na Tz ipi ni masikini kuliko mwenzie? Je, Wamachinga wao wanaratibiwa? Kama wa South Africa wanaratibiwa Xenophobia inatoka wapi karibu kila awamu ukiacha ya Mandela? Tz Wamachinga wanaondolewa kila awamu kasoro ya Mwl. Nyerere (hawakuwepo maana serikali ilikuwa inabeba ustawi wa wananchi wote ktk nyanja zote) na Magufuli (ambaye walikuwepo siku zote za uchaguzi na zisizo za uchaguzi), hapo chini angalia takwimu za kibajeti za South Africa vs za Tanzania uone masikini ni nani na kwanini bado kote kote uko Wamachinga hawaratibiwi hadi SADC na AU walipozichagiza South Africa kuweka mfumo imara wa kuratibu Wamachinga wa ndani na Wahamiaji ili kuondokana na janga la Xenophobia linalohujumu diplomasia kati yake na mataifa mengine, ZA R1.95tr in 2020-2021 ni equivalent na Tzs.296,258,768,511,301.63 (Exchange rate: Tzs.1 = ZA R0.0064), nadhani kama South Africa ingekuwa masikini Wamachinga wa Ethiopia ambao nchi yao ni tajiri pia wasingekuwa wanahamia South Africa. Aidha, Zambia Wamachinga ndiyo wamepiga kura za malipizi kumuondoa Edgar Lungu Ikulu kwasababu aliwapa Wachina Micro-economy yote ambayo hiyo ndiyo ilibeba Wamachinga weusi. Aya hii na ya pili inajibu hoja yako kwenye msitari wa kwanza kwamba "Wamachinga wasioratibiwa wako nchi masikini"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom