Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Dunia iko kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda (4th Industrial Revolution) ambapo matumizi ya teknolojia ya kisasa yanachukuwa nafasi kubwa kwenye uzalishaji na ubora wakati hasara ya mapinduzi haya ya nne ni rasilimaliwatu kukosa fursa za ajira ambazo zimechukuliwa na teknolojia (mashine na mitambo).
Historia ina Kawaida ya Kujirejeleza (Kujirudia)
Mapinduzi ya viwanda (Industrial Revolution) yalitukia karne ya 18 ambapo matumizi ya mashine yaliondoa rasilimaliwatu (wafanyakazi) nje ya ajira na hawa walioondolewa kujikuta wanakuwa Wamachinga wasio na fursa wala maamuzi kwenye mfumo huo mpya wa maisha ya binadamu ulioibuka duniani nyakati hizo.
Ni hawa Wamachinga ndiyo baadaye wakaja kuwa rasilimali ya kufanikisha mapinduzi ya mfumo kandamizi wa itikadi ya kibepari kwa kusikiliza mafundisho ya Muasisi wa mfumo mbadala wa Ukomunisti Karl Marx ambaye aliwashawishi kwamba ili kuondokana na mfumo dhalili wa Kibepari inawabidi kufanya mapinduzi tena ya moto (siyo ya baridi) ili wawezekuwa huru toka kwenye ukandamizaji.
Machinga hawa wa wakati huo walikosa hata vipande vidogo vya ardhi oevu na za rutuba ambazo zilimilikiwa na mapapa wa ardhi kwa jina la Makabaila na kuwafanya Wamachinga hawa kuwa wapangaji kwenye ardhi ya nchi zao na kushurutishwa kulipa kodi ya pango la kuishi kwenye ardhi zao wenyewe. Karne nne zimepita sasa 17 – 20 bado dunia ya leo inashuhudia jeshi kubwa la Wamachinga likizaliwa na kuzagaa katika mabara yote na nchi zote bila kuwa na mpango maalum wa kuwaratibu.
Tahadhari
Wakati tunatambua umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika uzalishaji mali na utoaji huduma na kwamba matumizi ya mitulinga haina budi kupungua, ni vivyo hivyo kwa pamoja katika mkondo huo wa uelewa tunatambua umuhimu wa Wamachinga walioondolewa na teknolojia ya mapinduzi ya viwanda kuhakikisha usalama wa dunia na mitaji ya wanaonufaika na mfumo huo mpya ili kwamba dunia isije ikajikuta imetengeneza akina Karl Marx wapya ambao wao wataona umuhimu wa kutumia Wamachinga kupindua mfumo mpya uliowafanya kuwa Wamachinga wasio na hatima zao mikononi mwao.
Athari za Siasa Katika Mifumo ya Uchumi Duniani
Maamuzi ya kisiasa duniani ndiyo yanaathiri na kuamua mifumo ya uchumi ambayo hiyo huja na faida na hasara huku kundi dogo ndilo linafaidi faida na kundi kubwa linaangamia kwa hasara. Mzigo wa Wamachinga unaelemea dunia kiasi kwamba kutokuwepo kwao hata kwa siku moja kutaokoa mengi katika mfumo wa maisha ya wanadamu licha ya faida zao zinazojulikana pia kuwepo, kwahiyo hapa ni suala la gharama ya fursa (Opportunity Cost).
If Motorbike commuters in Tanzania stopped using the transport for a day, that will be equivalent to health facilities discharging half of the admissions (hospitalized patients), save approximately 70% of daily traffic accidents across the nation, relieve Traffic Officers of excess routine work by 50%, cut Magistrates’ backlogs by 30%, reduce orphans, desolates, widows and widowers by at least 10% and free Inmate Prisons Cells by 25%, Majwala, D. O. (2021)
Kama abiria wa pikipiki wataacha kutumia usafiri huo kwa siku, hiyo itakuwa sawa na kuruhusu nusu ya wagonjwa toka walikolazwa Tanzania, kuokoa ajali za barabarani kwa 70% kwa siku nchini, kuwapunguzia kazi za ziada za siku Maafisa wa usalama barabarani kwa 50%, kuwapunguzia Mahakimu mlundikano wa kazi kwa 30%, kupunguza yatima, wakiwa, wajane na wagane angalao kwa 10% na kupunguza msongamano kwenye Magereza ya Mahabusu kwa asilimia 25%, Majwala, D. O. (2021)
Historia ina Kawaida ya Kujirejeleza (Kujirudia)
Mapinduzi ya viwanda (Industrial Revolution) yalitukia karne ya 18 ambapo matumizi ya mashine yaliondoa rasilimaliwatu (wafanyakazi) nje ya ajira na hawa walioondolewa kujikuta wanakuwa Wamachinga wasio na fursa wala maamuzi kwenye mfumo huo mpya wa maisha ya binadamu ulioibuka duniani nyakati hizo.
Ni hawa Wamachinga ndiyo baadaye wakaja kuwa rasilimali ya kufanikisha mapinduzi ya mfumo kandamizi wa itikadi ya kibepari kwa kusikiliza mafundisho ya Muasisi wa mfumo mbadala wa Ukomunisti Karl Marx ambaye aliwashawishi kwamba ili kuondokana na mfumo dhalili wa Kibepari inawabidi kufanya mapinduzi tena ya moto (siyo ya baridi) ili wawezekuwa huru toka kwenye ukandamizaji.
Machinga hawa wa wakati huo walikosa hata vipande vidogo vya ardhi oevu na za rutuba ambazo zilimilikiwa na mapapa wa ardhi kwa jina la Makabaila na kuwafanya Wamachinga hawa kuwa wapangaji kwenye ardhi ya nchi zao na kushurutishwa kulipa kodi ya pango la kuishi kwenye ardhi zao wenyewe. Karne nne zimepita sasa 17 – 20 bado dunia ya leo inashuhudia jeshi kubwa la Wamachinga likizaliwa na kuzagaa katika mabara yote na nchi zote bila kuwa na mpango maalum wa kuwaratibu.
Tahadhari
Wakati tunatambua umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika uzalishaji mali na utoaji huduma na kwamba matumizi ya mitulinga haina budi kupungua, ni vivyo hivyo kwa pamoja katika mkondo huo wa uelewa tunatambua umuhimu wa Wamachinga walioondolewa na teknolojia ya mapinduzi ya viwanda kuhakikisha usalama wa dunia na mitaji ya wanaonufaika na mfumo huo mpya ili kwamba dunia isije ikajikuta imetengeneza akina Karl Marx wapya ambao wao wataona umuhimu wa kutumia Wamachinga kupindua mfumo mpya uliowafanya kuwa Wamachinga wasio na hatima zao mikononi mwao.
Athari za Siasa Katika Mifumo ya Uchumi Duniani
Maamuzi ya kisiasa duniani ndiyo yanaathiri na kuamua mifumo ya uchumi ambayo hiyo huja na faida na hasara huku kundi dogo ndilo linafaidi faida na kundi kubwa linaangamia kwa hasara. Mzigo wa Wamachinga unaelemea dunia kiasi kwamba kutokuwepo kwao hata kwa siku moja kutaokoa mengi katika mfumo wa maisha ya wanadamu licha ya faida zao zinazojulikana pia kuwepo, kwahiyo hapa ni suala la gharama ya fursa (Opportunity Cost).
Tafakari hii Modeli (Model) Katika Sura ya Agenda ya Machinga:-If Motorbike commuters in Tanzania stopped using the transport for a day, that will be equivalent to health facilities discharging half of the admissions (hospitalized patients), save approximately 70% of daily traffic accidents across the nation, relieve Traffic Officers of excess routine work by 50%, cut Magistrates’ backlogs by 30%, reduce orphans, desolates, widows and widowers by at least 10% and free Inmate Prisons Cells by 25%, Majwala, D. O. (2021)