Historia inaonesha amani haiji ila kwa ncha ya upanga

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
793
1,007
Kwa wana historia wanafahamu vema kwamba bila vita ya 2 ya dunia huenda tusingeongea mambo ya uhuru wa mataifa yetu ya Africa leo hii. Ni maveteran wa vita ndio waliorudi na morale na vuguvugu la ukombozi baada ya kuielewa dunia huko walikoenda.

Inavyoonekana ni kwamba bila vita hawa jamaa huwa hawaelewi lugha za kawaida kawaida. Sasa walitupa uhuru wa bendera, uhuru wa kisiasa huku wakiwa bado wanatutawala kiuchumi, na kwa njia hiyo wametutesa sana katika kuiba rasilimali zetu kwa njia mbalimbali kama vile vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Sasa tunapaswa tuifurahie vita hii ambayo ama inafanana na vita ya 3 ya dunia ama ndio itazaa vita ya 3 ya dunia (hatujui) lakini ni vita inayokaribiana sana na ya 3 kwa kuhusisha mataifa yote. Tunapaswa kuifurahia kwa kuwa ndio njia pekee tunakwenda kupata ule " UHURU " uliosalia , ambao hawakuachia, uhuru wa kiuchumi kwa bara la Africa.

Sasa itazaliwa NEW WORLD ORDER, utawala wa upande mmoja tu wa west juu ya dunia nzima utaishia hapo. Wachina na Warussi hawakuwa wamekaa kiboya boya, vile vita vya kibiashara vilivyo vuma sana mpaka leo kati ya U.S na China ndio vilitangulia kuonyesha kuwa sasa muda umefika watu wanataka kuleta mabadiriko ya nguvu duniani. Mmarekani na west wenzie hawataendelea tena kuwa watawala wa ulimwengu baada ya hili.

Unapoona msouth Africa amegoma kuunga mkono west, lazima kuna ndoa ya siri hapo kati ya S.A na Russia, na nilisikia last year wasouth wanadevelop Nuclear technology, za matumizi ya amani, ( kila mtu anasemaga hivyo) , ni dhahiri ukiona mtu anatengeneza technology hizo basi anaemuuzia ni mrussi , hao west ni wachoyo na wasingetaka mtu azijue na kupata ubavu wa kuwasumbua baadae.

WACHA VIPIGANWE BARA LETU NALO JUA LICHOMOZE, TUMEKUWA BARA LA GIZA MUDA MREFU. KUMEKUCHA SASA.

Viva Putin, Viva Russia.
 
Africa tumekiwa bara la giza kwa sababu ya ujinga mwingi na uongozi mbovu sio kwa sababu USA na Ulaya ni superpower wanaoongoza dunia.

Hata Russia au China wakiwa superpower namba moja na namba mbili na USA ikaanguka kabisa Africa itakuwa kama ilivyo sasa tu, hakuna chochote kitakachobadilika kwa mabadiliko hayo, zaidi misaada na mikopo kutoka USA, Ulaya na World Bank itapungua.
 
Wew hujui chochote lofa Sasa Marekani ya nini?
 
Africa Kusini ina vinu vya vya nyuklia vilivyojengwa na makaburu tangu mwaka 1976, Imekuwa ikizalisha umeme wa nyuklia hata kabla USSR haijaanguka.
 
Bado nina machungu ya Waafrika wenzangu waliouawa kwa namna moja ama nyingine Iwe Maradhi,Silaha au chochote ambacho mzungu amekitumia Kumuangamiza Mwafrika...Narudia Tena na Tena Walipuane tu wapungue kama wanavyotupunguza sisi huku Bila Sababu Huenda Hii ni Adhabu ya Mungu Kwao Ikiwezekana wafe wote Tubaki Afrika Pekee yetu!!
 
Toka lini south africa akawa upande wa Urusi. Kwa mujibu wa ufunuo wa Yohana kambi ya west ndo itashinda na kusimika utawala wake kuelekea New world order. Bora mabepari washinde Mrusi na kambi yake anakwenda kuchakaza, kwa ushahidi wa Biblia.
 
Bado nina machungu ya Waafrika wenzangu waliouawa kwa namna moja ama nyingine Iwe Maradhi,Silaha au chochote ambacho mzungu amekitumia Kumuangamiza Mwafrika...Narudia Tena na Tena Walipuane tu wapungue kama wanavyotupunguza sisi huku Bila Sababu Huenda Hii ni Adhabu ya Mungu Kwao Ikiwezekana wafe wote Tubaki Afrika Pekee yetu!!
Ujinga na ubinafsi wetu ndio unatoa nafasi hiyo,mbona mabara mengine wao sio waathirika
 
Baada ya ukoloni wazungu pekee hawaibi rasilimali zetu, Waafrika wenzetu ndio wanaiba rasilimali zetu kwa kushirikiana na Wachina, Waarabu, Wahindi, Wazungu na yeyote ambaye anaweza kufanikisha hilo.
Lakini mali iliyoibiwa ni kijiko tu kwenye bahari still mali bado ni nyingi Sana afrika.
Mfano hapa tza raslimali zilizopo kwenye wilaya moja tu nchini zinafuta deni la taifa,shida hatujawekeza kwenye fikra zaidi.
 
Nakuhakikishia hii Vita Itaisha kimyakimya Na madhara unayoyasikia ya Hii vita sivyo kama Unavyosikia,Hakuna Mzungu wa Kuu Mzungu Mwenzake.
Nakuhakikishia Hii Ukrain Ingekuwa Afrika Saa Hizi Ishatawanyika na Tushasahau.
 
Africa tumekiwa bara la giza kwa sababu ya ujinga mwingi na uongozi mbovu sio kwa sababu USA na Ulaya ni superpower wanaoongoza dunia.

Hata Russia au China wakiwa superpower namba moja na namba mbili na USA ikaanguka kabisa Africa itakuwa kama ilivyo sasa tu, hakuna chochote kitakachobadilika kwa mabadiliko hayo, zaidi misaada na mikopo kutoka USA, Ulaya na World Bank itapungua.
Hujui ni jinsi gani west walitumia vibaraka wao ambao ni viongozi wajinga kuleta ufisadi na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, hawa walikuwa ni wajinga lakini walituzwa na hao west ili wawafanyie matakwa yao.

Na hapa hakuna haja ya kupata superpower mwingine kwa kuwa ujinga utaendelea kivingine ila kinachokuja ni balance of power, ndio maana wanazungumzia kwa sasa mambo ya kubadiri hata baraza la usalama (U.N) , sio ishu ziamuriwe na mataifa matano tena, tunakuja na NEW WORLD ORDER, A balance of power.
 
Baada ya ukoloni wazungu pekee hawaibi rasilimali zetu, Waafrika wenzetu ndio wanaiba rasilimali zetu kwa kushirikiana na Wachina, Waarabu, Wahindi, Wazungu na yeyote ambaye anaweza kufanikisha hilo.
Usiongee kama umekatika kichwa mkuu, angalia maendeleo yalikuwa wapi zaidi kwa muda mrefu halafu ndio utuambie nani alihitaji atuibie zaidi malighafi zetu, mchina kakua kwa kasi kiviwanda baada ya kusomesha watu wake kwa hao west na kuwaruhusu west kuwekeza China kufuatia cheap labor iliyokuwepo huko , na usitudanganye wakati tunajua anaeshikilia soko la dunia ndio mwizi mkubwa kwa miaka mingi.
 
Bado nina machungu ya Waafrika wenzangu waliouawa kwa namna moja ama nyingine Iwe Maradhi,Silaha au chochote ambacho mzungu amekitumia Kumuangamiza Mwafrika...Narudia Tena na Tena Walipuane tu wapungue kama wanavyotupunguza sisi huku Bila Sababu Huenda Hii ni Adhabu ya Mungu Kwao Ikiwezekana wafe wote Tubaki Afrika Pekee yetu!!
Hiyo ndio akili timamu mkuu, lakini ukiona jitu linatetea maharamia ujue hilo linajiandaa kufunga ndoa ya jinsia moja tu.
 
Africa tumekiwa bara la giza kwa sababu ya ujinga mwingi na uongozi mbovu sio kwa sababu USA na Ulaya ni superpower wanaoongoza dunia.

Hata Russia au China wakiwa superpower namba moja na namba mbili na USA ikaanguka kabisa Africa itakuwa kama ilivyo sasa tu, hakuna chochote kitakachobadilika kwa mabadiliko hayo, zaidi misaada na mikopo kutoka USA, Ulaya na World Bank itapungua.

Utumwa wa fikra ni utumwa mbaya sana na ndio unaokutesa
 
Lakini mali iliyoibiwa ni kijiko tu kwenye bahari still mali bado ni nyingi Sana afrika.
Mfano hapa tza raslimali zilizopo kwenye wilaya moja tu nchini zinafuta deni la taifa,shida hatujawekeza kwenye fikra zaidi.
U J I N G A

Tumekuwa watu wa lawama sana na kuzungumzia mambo ya watu,, tunaashindwa kufanya yetu...

Kila saa tunatazama dunia inafanya nini na tunashindwa kujua sisi sio Dunia,, tunatakiwa kuanzia chini ili tufike walikofika wao ndio twende sawa..
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom