Historia: Huyu ndiye Mchaga wa kwanza kuwa waziri katika Tanzania huru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Historia: Huyu ndiye Mchaga wa kwanza kuwa waziri katika Tanzania huru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAGAH, Aug 23, 2012.

 1. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Katika mazingira ya kawaida nchini Tanzania, si vyema kutaja makabila ya watu lakini kwa ajili ya kumbukumbu kwa wale wasiofahamu ni kwamba Nsilo Swai alikuwa miongoni mwa mawaziri sita Waafrika waliounda baraza la mawaziri wakati Tanganyika inapata uhuru wake mwaka 1961.Vilevile, Swai alikuwa Mchagga wa kwanza kuwa waziri katika baraza hilo lililokuwa chini ya Waziri Mkuu, Julius Kambarage Nyerere. Jambo hili ni moja ya mambo yaliyotokea miaka ipatayo 51 iliyopita.
  Swai (kwa sasa marehemu), jina lake kamili ni Asanterabi Zephaniah Nsilo Swai, aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35 tu.
  Kwa kifupi, Swai (aliyekuwa akitaniwa na marafiki zake kama ‘Bwana Miwani’ kwa sababu ya kuvaa miwani muda wote), alipata elimu katika Vyuo Vikuu vya Makerere (Uganda), Bombay (India) na Pittsburg (Marekani) ambako alipata stashahada.
  Aidha, mwanasiasa huyo alisoma Chuo Kikuu cha Delhi (India) ambako alipata shahada ya uchumi.
  Mbali na wadhifa wa uwaziri, Swai alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uchumi na Starehe ya chama kilichokuwa kikitawala wakati huo cha Tanganyika African National Union (TANU).
  Kwa ufahamu zaidi, miongoni mwa watu watatu walioshinikiza Tanganyika ipate uhuru wake Desemba 9, 1961 na si Juni 1962 alikuwa ni marehemu Swai.
  Awali, Uingereza ilipendekeza Tanganyika ipate uhuru Juni 1962, lakini kutokana na matatizo ya kiutawala, tarehe hiyo ikasogezwa hadi Desemba 9, 1962 jambo ambalo wawakilishi wa Tanganyika walilikataa na kurudishwa nyuma hadi Desemba 1961.
  Sababu kuu ya Uingereza kusogeza mbele ilikuwa ni mwezi Juni taifa hilo husherehekea ‘bathidei’ ya Malkia Elizabeth wa Pili, hivyo asingeweza kuja Tanganyika kuwa mgeni wa heshima.
  Katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo, Julius Nyerere alimteua Nsilo Swai, Oscar Kambona (marehemu) wakati huo akiwa Waziri wa Elimu na yeye mwenyewe. Walikutana na Waingereza na kuamua Tanganyika ipate uhuru Desemba 9, 1961.


  source: le mutuz blog
   

  Attached Files:

 2. B

  Bumela Senior Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  History again and not photos how?
   
 3. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bumela
  mkuu samahani nilikurupuka.
  picha tayari nimetupia ndugu.
  asante.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ukome kukurupuka
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Good to know...
   
 6. B

  Bumela Senior Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa picha MKuu, nilikumbusha tu usiwe mnyonge sana kawaida tu.
   
 7. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  hebu tupe pia taarifa za hawa wachagga wengine: eliufoo, jacob namfua na israeli elinewinga kama unazo tafadhali
   
 8. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  Nna hamu sana ya kumjua vizuri mtu aitwaye Paul Mareale,msaada please.
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Elinewinga alikuwa mchaga au mpare?

  Tiba
   
 10. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri kujua historia za Wazee wetu wazalendo wa kweli ambao Mungu ameshawita. RIP Nsilo Swai
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Big up wachaga. Huwa nawakubali watu hawa Nyerere alifanya nao kazi na akafanikiwa leo hii eti mnawaweke pembeni na ndiyo maana mambo yanakwenda mrama. Ndiyo maana mwalimu alikataa udini na ukabila, leo hii mlio madarakani mnavikumbatia na sasa vinawageuka!!! Naangalia sakata la sensa na waislam nacheka huku nasema "unavuna unachopanda". Ndicho mlichopanda na msitake kuwakamata na kuwaweka selo na vitisho!!! Si mmewakumbusha watanzania kuwa dini na ukabila vipo? Sasa vumilieni matokeo yake na 26th August mjiandae na mabomu na ffu ili kuwatuliza!!
   
 12. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Habari nilizo nazo ni kuwa israeli Elinewinga alikuwa mchagga wa Lukani /Kyuu Masama
   
 13. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Asante kwa kuweka kumbukumbu zangu sawa.

  Tiba
   
 14. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mwenye habari za Jacob Namfua please!
   
 15. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Mwenye habari za babu yake phd atueleze sababu wazazi wangu walinificha, ila alikuwa chief mkubwa Wakati wa Uhuru
   
 16. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  itakuwa lukani mkuu, kyuu siyo, kama nimekosea wamasama mtanirekebisha
   
Loading...