Historia halisi ya maisha ya kale.

albuluushiy

JF-Expert Member
Oct 2, 2013
1,405
685
Na.Dr.Omar Ali.
kuna mambo nayafanyia tafiti sasa hivi kuhusu maisha yalivyokuwa zama za kale kabla ya kuzaliwa yesu, vipi teknolojia zilivyokuwa kipindi hicho, historia inaonyesha jamaa walikuwa na teknolojia zaidi ya tulizonazo, sisi tunaona kwamba tuna maendeleo na teknolojia kwa kutumia mashine, nishati kama umeme, gesi, nk.
ukuaji wa viwanda nk.
hawa jamaa walikuwa hatari sana wengi tumeaminishwa kwamba sisi ndio wa kwanza kutumia umeme while wenzetu hawa walikuwa na teknolojia zaidi ya umeme, na walitumia wireless sana kuliko sisi tunavyotumia, hawakuwa na mistimu au minara ya kusafirisha sauti nk.
wao walikuwa wakitegemea zaidi wireless katika kufanya mambo yao mengi hata katika kusafirisha nishati ya kipindi hicho walikuwa wakitumia wireless najua mtakuwa wagumu kunielewa ila ndivyo ilivyo, walikuwa na viwanda vya silaha kali za kivita usifikirie kuwa ni hivi vibunduki mlivyozoea kuviona, wao walitegemea zaidi wireless silaha unaiset hapa inafika unapotaka na inaleta athari kwa wakati huo huo, watu walikuwa na utaalamu wa kuleta kitu kilichopo masafa marefu kwa kupwesa na kupwesua, sio uchawi bali ni teknolojia ya hali ya juu waliokuwa nayo kipindi hicho, mfano wa wazi ni Nabii Suleiman A. s alipotaka kiti cha enzi cha malkia Balqiis jini akasema atakileta kabla hajasimama alipokaa nabii suleiman, ila Quran inaeleza kwamba mtu mwenye elimu kutoka kwenye kitabu, alisema ataleta hicho kiti kupwesa na kupwesua na akaileta hapo hapo, hapa maulamaa wamekhitalifiana kuhusu tafsiri ya hapa ila wote wamekubaliana kwamba huyu mtu alikuwa ni msomi, ni usomi gani hapa ndio kuna ikhtilaaf ila wanasayansi wengi wa karne zilizopita waneleza kwamba huyu alikuwa mwanasayansi aliebobea katika masuala ya sayansi na intelejensia sasa niwaulize wapendwa leo kuna mwanasayansi mwenye nguvu hyo? jibu ni hapana je bado unaamini kwamba sisi ndio wajuvi wa mambo kuliko zama zote zilizopita? sikatai wala sipingi kwamba sisi ndio zama bora na ndio umati bora ila hii haifanyi sisi ndio tuwe tunajua kila kitu au tuwe civilized more than them, kuna mengi ya kuyafafanua siwezi kwa kuwa huu ni usiku mkubwa ila ulimwengu huu una siri kubwa sana ambayo walimwengu wengi hawajui ni kutokana na kuwa wavivu kufanya utafiti, na ukifanya utafiti hapa ndio utajua kuwa Allah ni muweza wa kila jambo, Allah ni mkubwa alikuwepo yupo na atakuwepo milele na milele.
wengi wetu akili zetu zimefungwa minyororo na watu wachache duniani hapa kwa kuficha historia ya kweli ya dunia hii, japo nyengine zinakuwa fix ila hawa kina darwin ambao wanatuaminisha sisi ndio binaadam tulioendelea na babu zetu walikuwa ni manyani etc, na sisi tukaichukua tukaiweka katika mitaala yetu na bado inaendelea kuviza fikra zetu na wakoloni wanalazimisha tuendelee kusomeshwa hii ili tuendelee kuwa watumwa wa fikra kwa wamagharibi, angalia japo sasa hivi tumejua kama huu si ukweli lakini pamoja na hayo hatuna ubabe wa kubadilisha, hichi ndicho kinachofanya waafrika wa sasa waonekane wapumbavu wa kutupwa na kudhalilika duniani, ilhali wao ndio waliobeba ustaarabu wa dunia hii kwa miaka mingi BC yaani kabla hata ya kuzaliwa nabii Isa na mtukufu wa darja Mtume saw, ukiviangalia mabaki ya vitabu vilivyotungwa miaka 2000 kabla ya yesu utajua kama wenzetu walikua mbali sana, na havijaandikwa kwa mkono bali vimechapwa najua mtakuwa wagumu kuamini ila fungua akili yako iweke huru halafu uangalie ulimwengu huu kwa jicho la kielimu zaidi na utafiti akili yako itakubali kidogo kidogo.
nataka niandike mengi ila bado niko kwenye utafiti ila usikose vitabu vyangu ninavyotaraji kuvitoa siku zijazo inshaallah, kikiwemo Uislam na sayansi, vita vya fikra, historia halisi ya maisha ya kale, historia halisi ya muafrika,Historia ya sayansi ulimwenguni, ila pia usisahau kuwa katiba ya kwanza kuandikwa duniani iliandikwa miaka 2000 kabla ya yesu katika bara la afrika katika nchi za mto nile, na sisi afrika mashariki tuna historia adhimu sana jamani ndio maana Dr. Leakey akagundua kuwa mwanaadamu wa kale zaidi aliishi Tanganyika, na visiwa vya Zanzibar kulikaa watu enzi za kale sana ila watu ni wavivu wa utafiti jamani tufanyeni utafiti tusichoke, kwani inasemekana wataalamu wa kale wa astronomy wanatokea Znz, na ndio maana mpaka leo elimu hii wazee wote huko nyumbani ni wataalamu wa hii, ila katika historia ilioandikwa karne ya tano inavitaja kama visiwa vya mbali katika mashariki ya bara la kijani, na hii ni nukuu ya vitabu vya kale sana kabla ya yesu ambavyo vilitaja visiwa ambavyo vina wasomi wengi wa elimu ya astronomy ila wanahistoria wana tafautiana katika kuvitaja hivi visiwa ila idadi iliotajwa ni visiwa 50 vilivyo kwa pamoja mashariki ya bara la kijani, tufanyeni utafiti jamani hiki kizazi cha sasa ni cha kuhoji, sio tuambiwe Mungu hayupo halafu mwanaadamu twaona azaliwa na na anakufa halafu watwambia ni natural howcome? Lazma kuna ambae anaendesha Wenye nguvu, na elimu ya kipekee.
Wakatabahu.
Mdogo wenu Omar Ali Mussa Albuluushiy.
usiki mwema.
 
Hujatoa majibu wala ushahidi katika MADA yako zaidi ya kuomba watu wafanye utafiti...

Tafiti zinafanywa na ndio matokeo ya maendeleo na mabadiriko yanayo tokea Ulimwenguni sasa....

Wakati mitume na Manabii wanamuomba Mungu alete Mvua, leo hii Mwanadamu anaweza kukuambia ni wapi kesho itanyesha Mvua na wapi kitatokea Kimbunga ( kupitia maedeleo ya KITEKINOLOJIA)

Tafiti zinafanyika na mwisho kuja na majibu mbalimbali na sote ni MASHUHUDA.....

Hatuhitaji ubishi wala ushabiki wa KIDINI kubeza juhudi na maendeleo yaliyo letwa na WANASAYANSI zaidi waliofuata baada ya KUFA KRISTO....(Issa mtoto wa MARIAM).
 
Ndio mnavyo danganyana misikitini.
Kupwesa na kupwesua ndio nini?
 
kwanza ncheke sana dah sijapata kuona watu waliokua hawafadhiliki kama wa jamii forum na hii yote inatokana kua kuna mchanganiko wa dini tofauti na ndio maana dharau na kejeli haviadimiki.heshimu dini za watu mkuu sasa nyie makanisani izo pumba za kusameheana zambi na binadam mwenzako mbona hazijadiliwi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom