Historia fupi ya vita ya Kagera 1978-1979

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
150
HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79
MAJESHI YA UGANDA YALIVYOINGIA KAGERA

TUONE KWA UFUPI.

MWAKA 1978, Majeshi dhalimu ya Nduli Idi Amin Dadaa wa Uganga, yalivamia Ardhi ya Tanzania, eneo la Mto Kagera, katika mkoa wa Ziwa Magharibi na kufanya uharibifu mkubwa wa mali na kuua wananchi wa mkoa huo, NYAKASAGANI MASENZA anasimulia kupitia vyanzo mbali mbali vya habari jinsi majeshi hayo yalivyoingia Tanzania na Amin kutangaza rasmi kuwa eneo hilo la Mto Kagera ni sehemu ya Uganda.

DAIMA Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa ukombozi wa Bara la Afrika, ikiwa miongoni mwa mataifa masikini zaidi duniani, lakini iliyojariwa viongozi wenye hekima, kuanzia muasisi wake Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

Busara za viongozi wa Tanzania zilianza kuonekana mwaka 1961, baada ya Mwalimu Nyerere kuwanasua watanzania kutoka mikononi mwa utawala kandamizi wa wakoloni, wakati huo pia akiwa tayari kuchelewesha Uhuru wa Tanganyika ili nchi zingine zilizokuwa kwenye mchakato wa uhuru zipate Uhuru siku moja na Tanganyika.

Msimamo dhabiti Mwalimu Nyerere, uliweza kujenga Tanzania imara na kuifanya kuwa Taifa kimbilio la vikundi na vyama vya wapigania uhuru Kusini mwa Afrika, ambao walipewa hifadhi ya kudumu na kutumia ardhi ya Tanzania kuwa sehemu ya mapambano ya kudai uhuru wao, ambao waliupata kupitia mgongo wa Tanzania.

Viongozi kama Hayati Edward Mondolane, Samora Macheli wa Msumbiji, Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Yoweri Mseveni wa Uganda, ni sehemu ya viongozi waliopitia mikononi mwa Mwalimu Nyerere wakati wakipigana nchi zao zikombolewe.

Watanzania walianza kuingiwa na wasiwasi mwaka 1971, wakati Nduli Idi Amin Dada alivyoasi na kuchukuwa madaraka ya Uganda kwa nguvu baada kuungusha utawala halali wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hayati Milton Obote na kutangaza kuitawala nchi hiyo kijeshi.

Mwanzo wa utawala wake waganda pamoja na mataifa mengine walidanganyika, wakawa na matumaini makubwa juu ya kiongozi huyo wa kijeshi, kutokana na ahadi zake nyingi kwamba yeye ataitala uganda na kuhakikisha eneo lililoko Tanzania, sehemu ya mto kagera, katika mkoa wa Ziwa Magharibi litakuwa sehemu ya Uganda.

Mwaka huo huo, Idi Amin alijaribu kutimiza madai yake kwa kuishambulia sehemu hiyo ya Mto Kagera, lakini watanzania walikuwa imara katika kulinda ardhi yao sehemu hiyo akashindwa, baada ya majeshi yake kurudishwa nyuma na majeshi hodari ya Tanzania.

Pamoja na majeshi yake kurudishwa nyuma, Fashiti huyo aliyejitangaza kuwa Rais wa maisha wa Uganda, akiwapongeza wapiganaji wake kwa kurudishwa nyuma huku akiwasifia kupata jeraha kidogo kutoka kwa majeshi ya Tanzania.

Baada ya wapiganaji wake kurudishwa nyuma Idi Amin alisema huo ni mwanzo tu, awamu nyingine atatumia silaha nzito zaidi ikiwa pamoja na makombola ya kurushwa kwa ndege na kuwaongezea nguvu askari wa miguu, jambo ambalo liliwafanya waganda kuingiwa na hofu kutokana na utawala huo wa mabavu, baada ya Amin kuanza kuwatilia shaka wananchi na kuwaua hovyo.

Mauaji ya kinyama yakawa kitu cha kawaida katika Uganda, wananchi wengi wasiokuwa na hatia walipoteza maisha, watu mashuhuri kama Jaji Mkuu Benedicti Kiwanuka na Askofu Mkuu Jamal Luwumu, waliteswa na kuuawa chini ya utawala wake.

Aitoa amri kuwa watu wote wanaopinga utawala wake, wapigwe risasi hadhalani, katika kutekeleza moja ya ndoto zake alizodai kuwa ni mazungumzo baina yake na Mwenyezi Mungu, aliwafukuza kutoka Uganda, Waasia wote waliokuwa na pasi za kusafiria za Uingereza na kuwanyanganya mali zao zote.

Baada ya shutuma nyingi za uongo dhidi ya Tanzania, mnamo tarehe 30 )ktoba 1978 Idi Amin aliyaamuru majeshi yake kuvuka mpaka na kulivamia eneo la Tanzania, ambapo watanzania zaidi ya 10,000 wasiokuwa na hatia yaliangamizwa na eneo la kilomita za mraba 1850 zilichukuliwa na majeshi ya Uganda.

Majeshi hayo ya Amin yalilikalia eneo la mto Kagera sehemu ya kyaka na kufanya vitendo vya kinyama kwa kuua wananchi wa mkoa wa Ziwa Magharibi hovyo, kuchoma nyumba, viwanda, kupora mali nyingi na kuzipeleka Uganda.

Itaendeleaaaaa.....
a249d3b4ff1db656ef386afa199e94a1.jpg
fa03aec141a0d9727bbdbe97e5f90c3e.jpg
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,130
2,000
Mleta mada kuna baadhi ya mambo hayapo sawa, au labda kwa sababu source yako ni vitabu vya Tanzania tulivyojiandikia wenyewe... one sided history!!

So, kama mtu ana shida ya kumeza historia inayotu-favor sisi then, uliyoandika yote ni sahihi lakini kama mtu angependa kupata historia ya ukweli isiyoegemea upande, basi kuna walakini kwa maandiko yako!

Ingawaje ni kweli kwamba, by 1978 Tanzania haikuwa na budi zaidi ya kuingia Uganda na kwenda kumchapa Amin, lakini ukiangalia choko choko ya Vita Vya Kagera ni sisi wenyewe!!!

Inawezekana kabisa kwamba hata kama tusingeanza sisi uchokozi huenda Amin angeanza lakini ukweli unabaki pale pale kwamba sisi ndio tulianza!!!

Ikumbukwe kwamba, Dk Milton Obote alikuwa rafiki mkubwa wa Hayati Baba wa Taifa! Hivyo basi, Obote alipoenda kwenye mkutano Singapore kisha akapigwa biti na Amin kwamba asirudi Uganda; Obote akatii amri na kurudia Dar es salaam Tanzania.

Baada ya Obote kuja Dar es salaam, wafuasi wake kadhaa wakavuka mpaka na kuingia Tanzania.

Kama ambavyo Maswahiba wengi wanavyofanya, Mwalimu akaandaa coverty operation ili kwenda kumng'oa Amin madarakani ili swahiba wake Obote akachukue Ikulu yake!!

Hili lilifanyika baada ya wafuasi kadhaa wa Uganda People's Congress, UPC kupelekwa Kambi ya Handeni kupata mafunzo ya kijeshi ili hatimae warudi Uganda kumpindua Amin.

Na kweli, walipoamini wamekwiva, wakavuka mpaka kurejea Uganda na kufanya jaribio la kwanza la kumpindua Amin. Kwa bahati mbaya; walifyekwa vibaya mno!! Hiyo ilikuwa ni 1972 na hapo ndipo Amin alipopata sababu!!!
 
Mwanah

JF-Expert Member
May 7, 2013
353
225

URAFIKI BINAFSI WA NYERERE NA MILTONI OBOTE NDIYO CHANZO CHA VITA VYA KAGERA.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,250

Una ushahidi wa picha?
 
dabaga6

JF-Expert Member
Jun 11, 2017
244
500
Toa kiini sio historia. Kiini hutolewa na waliokuwepo au kushuhudia mambo flani na kupasi generation to generation. Historia inawezatolewa kwa malengo flani inaweza hata badilishwa uhalali wake. Soma historia ya Mkwawa kwenye vitabu na uje karenga tukupe yetu. Try to be different. Bring New things kaka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom