Historia fupi ya makamanda na upambanaji wao dhidi ya Nduli Iddi Amin (Dada)

Ushindi wa Vita ulipatikana Lukaya, ambapo brigade iliyokuwa chini Imran Kombe iliwapa kichapo cha kushtukiza askari wa Amini na wa Libya kilichopelekea kuuwawa kwa kiongozi wa Jeshi la Amini, Sule. Kuuawa kwa Sule na kichapo cha Lukaya km kuliwavunja Moyo sana Askari wa Amini na Mamluki wa Libya na Palestina. Mwalimu Nyerere alimpigia sima Gadafi akamwambia atawasindikiza askari wa Libya kutoka katika mstari wa mbele wa Mapambano kama Libya itakubali kuondoa majeshi yake. Kitu ambacho Gadafi alikubali. Ni aibu kuwa Kombe alikuja kuuwawa kijinga sana.
Kombe, Kombe very sad, nafikiri ni kwa sababu ya uzalendo wake kipindi hicho mkapa anafanya yake kuuza nchi kwa mabeberu madini, Mabenki, etc.
 
Hakika tumetoka mbali , ni fedheha kwa vijana wa kileo kukalia kutukanana mitandaoni bila haya! Hakika hao ndio walikuwa wazalendo wacha kizazi cha leo tutese mitandaoni kwa zamu, ni aibu ni aibu hata hatujifunzi, vijana tunaishia kusengenyana mitandaoni, kutukana viongozi wetu ,madawa ya kulevya na ushoga ndo legacy ya waliowengi, kulia lia na lawama serikalini,

HATARI
 
Uzi huu unatukumbusha kuwa majeshi yetu yalifanya vizuri, na pia wanajeshi na jeshi letu wanapendana sana.

Jee kuna maana maalumu kuletwa wakati huu?
 
Nakumbuka ndugu yangu alikuwa jeshi la anga kazi yake ilikuwa ku plot mwelekeo wa ndege, maandishi wanayaandika kutoka kulia kwenda kushoto, ili aliyeko upande wapili asome kuanzia kushoto kwenda kuliA
 
Uzi huu unatukumbusha kuwa majeshi yetu yalifanya vizuri, na pia wanajeshi na jeshi letu wanapendana sana.

Jee kuna maana maalumu kuletwa wakati huu?
Maana ipo.tunaelekea kuadhimisha siku ya mashujaa wa tanzania.
 
Daah asante sana mkuu!
Siku hizi shujaa wa Taifa ni RC Makonda na akina Riziwani ambao hawajachangia lolote ktk taifa hili
 
Ukweli mchungu ni kuwa vita hii ni miongoni mwa makosa makubwa ya Baba wa taifa. Hakukuwa na sababu za msingi za kuwachokoza waganda kwa kumpa hifadhi Obote na kupanga mapinduzi ya serikali ya Uganda tokea Tz, ikiwemo Ku train wapiganaji wa Obote. Madhara kiuchumi ya vita ile yameathiri nchi hadi leo. Tuliambiwa tufunge mikanda kwa miezi 18, lakini haijawahi kufunguliwa.
 
Makundi na mafungu tunayogawanywa leo kamwe hayawezi kutujengea umoja na mshikamano.
Kuna haja ya kuangalia tumejikwaa wapi, ushabiki wa kisiasa hautusaidii na mechanism zinazotumika kulinda madaraka zinabomoa umoja wetu.
Njia pekee inayomfanya kila mmoja kuwajibika kwa nchi yake ni kuzingatia utawala wa katiba na sheria.
Leo hii mtu anamlazimisha Askari aliyekula kiapo kuilinda katiba inayomkataza kuwa mwanachama wa Chama cha siasa aseme CCM hoyee! Unamtisha kwa kuchukua jina lake na cheo chake ili iweje! Askari anakuelewesha kwamba walioshabikia siasa ni viongozi wakubwa mimi ni Askari mdogo siruhusiwi, unamtisha na cheo chako cha Unec, tunakwenda wapi!
Amani inatoweka watu wanapokata tamaa baada ya kuona utaratibu waliojiwekea kujitawala (Katiba) unapuuzwa. Tuendelee kumuomba Mungu atuepushe.
 
..viko vitabu vimeandikwa na waTz lakini ni vigumu sana kuvipata na havikuandikwa kwa ubora unaotakiwa.

..kipo kitabu kinaitwa " Vita vya Kagera -- Kagera hadi Arua. "

..kitabu kingine kinaitwa, " Kuanguka kwa Fashisti Iddi Amini "
Labda tumcheki mzee Mohamed Said pengine kuna alichoandika kuhusu hii vita!
Eti mzee wangu Mohamed Said wakati wa hii vita ulikuwa wapi? Unaizungumziaje hii vita? Kuna kitabu chochote umeandika?
Wasalaam
 
Back
Top Bottom