STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,770
- 553
Ndugu zangu wana JF naomba niwaletee historia fupi ya Dr. Slaa na Chadema katika wilaya ya karatu tangu 1995 hadi leo hii.
Kwanza kabisa Karatu ni sehemu mambayo imekuwa na historia ya kipekee katika siasa za nchi hii na hii imetokana na ukweli kwamba jamii ya watu wengi walioko karatu wametoka katika wilaya Mbulu. Sehemu ambayo hata mwanzishi wa Taifa hili hataisahau kutokana na kumpinga Nyerere ambaye alikuwa aliataka Dodo awe Mbunge wa mbulu ile hali wananchi wanataka Sarwat ndo awe mbunge wao na hilo likafanikiwa kwani baada ya malumbano Nyerere alikubali Sarwat chaguo la wananchi awe mbunge .
Baada ya kuanza kwa vyama vingi vya siasa, na karatu kuwa jimbu la uchaguzi ndani ya wilaya ya mbulu, historia nyingine inakuja pale ambapo katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kijiji cha Gongali ilipo msimamisha mgombea wa mwenyekiti wa kijiji kupitia Chadema mwaka 1994 na kushinda kwa kura nyingi sana na kuandika katika historia ya nchi kuwa kijiji cha kwanza kuongozwa na upinzani na ndio kijiji ambacho anaishi Dr. W.P.Slaa.
Mwaka 1995 watu wa karatu waliamua kumwondoa madarakani Mbuge wa wakati ule Patric Qorro ambeye alikuwa ni mbabe na asiyejali maendeleo ya wananchi wa Karatu kwa Kumwomba Dr Slaa kurudi nyumbani na kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM. Kwenye kura za maoni alimwacha Qorro kwa mbali sana lakini ccm kwa utawala wao wa kidicteta wakamwengua kule dodoma ndo wananchi walipo mwomba na kumtaka achukue fomu kupitia chadema ili agombee kuwa mbunge.
Ndipo Dr. Slaa alipokubali watu wakaunganisha nguvu zao dhidi ya Pesa za CCM na kumpigia kampeni Slaa akashinda kwa kishindo.
Kuanzia 1995 hadi 2000 Dr Slaa aliweza kutekeleza miradi ya maji hasa kwa vijiji vinavyozunguka wilaya ya karatu ila kwa taabu sana kwa kuwa viongozi wengi walikuwa wa CCM walikuwa hawamungi mkono lakini alipowaambia wananchi wakamwunga mkono na kuanza kuwabana viongozi wa wakati ule.
Kwenye uchaguzi wa 2000 Dr. Slaa aliwaomba wananchi wa karatu jambo maja tu wampe madiwani, hata kura yake hakuwa anaomba, ndipo walipompa madiwani 9 kati ya 12 na wakachukua halimasharuri na kuanza kutekeleza ilani ya chadema kwa karatu ikiwemo kupunguza kudi ya kichwa toka 5000 hadi 2000 ndipo CCM wakafuta kwa nchi nzima 2004. Vile kila diwani aliweza kuhamasisha wananhi kujenga Dispensary kila kijiji na Shule ya sekondari kila kata na kupanua huduma ya maji kwa kila kijiji na yote hayo yakafanikiwa ndani ya miaka mitano.
Mwaka 2005 Dr Slaa alikuwa na agenda ya kutafuta waalimu pamoja na madaktari na manesi, hilo nalo lilifanikiwa kwa kuhamasisha wananchi kushiriki kujenga nyumba za waalimu na madaktari na manesi kwani, kuwa mfanyakazi wa karatu ni dili kwa sababu unapata nyumba ya bure karibu na shule au hospitali/zahanati.
Na kwenye uchaguzi wa 2005 kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha kuna shule za A-level/ Chuo ambazo hadi sasa zipo shule kama nne za A level, Chuo cha manesi na madaktari moja na Chuo kikuu kimoja ambacho kitachukua wanafunzi mwaka kesho.
Hadi sasa halmashauri ya wilaya ya karatu iko chini ya chadema na ina madiwani 10 kati ya 14, kwa hiyo wananchi wa karatu wanajivunia kuwa upinzani.
HITIMISHO:
Si vibaya kwa wabunge wengi wa upinza wakamwomba ushauri wa namna ya kujipanga ili uweze kutimiza majukumu yako vizuri kwa wananchi wako kwani amefanikiwa kwa mambo mengi.
Peoples Power Mabadiliko ya Katiba lazima