HISTORIA FUPI: Ijue Sababu ya Mwanamuziki K'naan Kuimba Nyimbo ya FATIMA

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
0600ec5577b9dd8cc542bd0aa64b559b.jpg

K’naan (KEINAN ABDI WARSAME) ni msanii kutoka CANADA na pia ni mzaliwa wa SOMALIA mjini Mogadishu. Watu wengi wanamtambua kwa nyimbo yake maarufu ya waving flag ambayo aliitunga kwaajili ya kuwaamsha wananchi wa SOMALIA na harakati zao za uhuru/ukombozi na baadae ilitumika kwenye kombe la dunia kama ilivyokuwa kawaida ya wasanii baadhi kupata nafasi ya kutunga au kutumika nyimbo zao pale unapofika msimu wa kombe la dunia (Ilikua south Africa 2010).


Ana nyimbo nyingi lakini tuitazame hii FATIMA, NI nyimbo inayojenga hisia kubwa pale unapopata kutambua chanzo chake. Nyimbo hii ipo kwenye album yake ya TROUBADOUR ambayo ilitoka mwaka 2009 ikiwa na vibao vingine kama waving flag, take a minute na people like me.
Fatima ni hadithi ya msichana mdogo na mrembo ambaye walipendana sana na Knaan wakiwa wadogo huko Somalia (walikua ni majirani). Knaan anasema alikua ni msichana wa ajabu ambaye alimwona ni kama alien kwakua aliweza kuzungumza lugha tatu (Kiswahili, Kiarab na Kingereza) licha ya wote kuwa ni wasomali na wamekua pamoja.

minneapolis-somali-americans_main.jpg


Kwa mikakati ya utoto, walipanga kukimbia Mogadishu pamoja, kwakua kulikua na vita kali sana kipindi hiko na walipanga watakimbilia Newyork Marekani pindi watakapokuwa wakubwa.
Wakati wao wanapanga hivyo, familia ya knaan ilikua tayari kwenye mkakati wa kwenda marekani ambapo baba yake mzazi alikua anaishi.Kwa umri wao wa miaka 12 kipindi hiko, hawakua na la kufanya zaidi ya kuwasikiliza wazazi wao. Kabla hajaondoka kwenda nawyork, Knaan alipatiwa barua kadhaa na FATIMA, barua ambazo aliziandika kwa kingereza ili ampe Knaan chachu ya kujifunza kingereza haraka pindi atakapofika Marekani.


Siku tatu baada ya Knaan kufika marekani, alipata taarifa kuwa FATIMA ameuawa kwa kupigwa risasi kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa inaendelea nchini SOMALIA. Wasomali wengi waliikimbia nchi yao kwakua kulikua na vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilianza mwaka 1986. Knaan aliondoka Somalia mwaka 1990.

eef7a432-00-us-war-in-somalia-kills-civilians.jpeg

Baadae Knaan alielewa kilichoandikwa kwenye barua na rafiki yake FATIMA. Na kumpelekea kuandika nyimbo yake hiyo na kuijumuisha kwenye album yake ya Troubadour, ingawa nyimbo hiyo inaeleza tu jinsi alivyompenda FATIMA na kuonyesha maumivu aliyoyapata pale alipomwacha kwenye vita huko SOMALIA. Nadhani FATIMA sio tu nyimbo ya upendo, bali pia ni nyimbo ya kupinga vita.



HISTORIA FUPI: Ijue Sababu ya Mwanamuziki K'naan Kuimba Nyimbo ya FATIMA
 
Back
Top Bottom