HISIA ZANGU.................nini sheria wakati uliopo na uliopita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HISIA ZANGU.................nini sheria wakati uliopo na uliopita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Masanja, Jan 28, 2011.

 1. C

  Chief Masanja Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wajukuu zangu nipo mbele ya tv naangalia. ni mengi yamezungumzwa na mengi tumeyaona.

  nimepata jambo moja ambalo nafikiri ndilo la msingi sana pamoja na mengine mengi yaaliyojitokeza....NINI MAANA YA SHERIA KATIKA WAKATI ULIOPO NA ILE YA WAKATI ULIOPITA.

  swali langu nimeuliza hasa nikiangalia hizi kauli za kwamba ''..... haiwezekani raisi aunde tume ,.....haitokuwa tume huru na kwamba hapaswi kuchagua yeye........'' pamoja na mengine nataka tujiuliuze na hasa ndg zangu wanasheria wakina msando mtusaidie. nini sheria inazungumza juu ya
  1. nani mwenye mamlaka ya kuanzisha mchakato wa katiba kwa mujibu wa sheria
  2. anaanzishaje mchakato huu?
  3. na nini maana ya mawazo ya watu?
  4. je kama sheria inatamka jambo, katika muda gani mtu anaweza tamka vyengine?

  naomba tujibiane haya ili tuanze mjadala vizuri.

  naomba kutoa hoja.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  cha muhimu tufikie muafaka kama taifa na si kikundi fulani kwa manufaa yao ya kujiundia tume! nimependa maoni ya kibanda wa tz daima japo hata majina ya wanaounda tume yakipelekwa bungeni bado yanaweza kuchakachuliwa!
   
 3. F

  Fenento JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu mimi nitakujibu hoja yako kisiasa kwa vile si Mwanasheria. Mosi, nani mwenye mamlaka na ataanzishaje mchakato?. Kwa ujumla hilo ni tatizo mojawapo la Katiba yetu kwa vile haijafafanua mchakato mzima wa kuandika katiba mpya. Katiba tuliyonayo imefafanua juu ya kufanya marekebisho au kuweka viraka kwenye sheria mama(katiba). Kwa mantiki hiyo basi katiba yetu haijafafanua nani na kwa namna ipi mchakato wa kuandika Katiba ufanyike.

  Kwa kuwa katiba yetu haizungumzi lolote kuhusianan na mchakato wa katiba ndo maana serikali imehusika moja kwa moja kuanzisha mchakato lakini pia kuna nafasi ya Bunge letu kuongeza hivyo vipengele kwenye katiba kwa utaratibu wa kisheria. Baada ya hapo katiba hiyo sasa itafafanua namna ya kuandaa katiba mpya na utaratibu utafuatwa kisheria.

  Pili, Mawazo ya watu kwenye suala la katiba ni muhimu sana,kwani ukitaka kupata katiba ya watu ni lazima wananchi washirikishwe kutunga katiba yao, ndiyo maana hata hii katiba tuliyonayo haikuwa shirikishi kwa vile watanzania hawakuipigia kura. Mfano Kenya etc.
   
Loading...