Hisia za wananchi mtaani: Kilichomfukuzisha Ndugai ni kuhoji kwake kwa nini Pesa nyingi za mkopo kupelekwa Zanzibar licha ya idadi ndogo ya watu

Ndugai amevuruga sana, amesababisha bunge kuwa dhaifu, sababu alikuwa Dili moja na jiwe, uchafuzi, na nchi imekosa upinzani bungeni.
Kwa hiyo mama alivyolinajisi bunge kwa kumchamba Ndugai namna ile ndio ameimarisha bunge?
 
Inawezekana kweli ila kilichomfukuzisha siyo hicho alichohoji bali ni maovu yake nje na ndani ya Bunge. Yaani mioyo ya wale wote ambao wameumizwa na yeye akiwepo aliyepigwa rungu kule ndani ndani Kongwa na wengineo wengi ndani na nje ya chama chake majibu ya maovu yake yamejibiwa kwa kivuli cha mikopo ya serikali na si vingine.

Hiyo hoja yake ingetolewa mtu muadilifu angeungwa mkono na asingeshambuliwa vile.
Ndugai alikuwa shetani kabisa ndani ya bunge
 
Hapo ndipo tunapoonekana wajinga!

Yani huangalii hoja ila unaangalia mtoa hoja.

Tuna safari ndefu bado
Katika sayansi ya jamii haiba ya mtu anaebeba ujumbe ni muhimu sambamba na ujumbe kwa ajili ya usikivu na uchukuliwaji.

Eg. Hoja atakayoitoa babu Tale na hoja ile ile ikatolewa na Mbowe unafikiri uzito wa hoja utakaa wapi🤔

Mlimao hauwezi kuzaa zabibu
 
Katika sayansi ya jamii haiba ya mtu anaebeba ujumbe ni muhimu sambamba na ujumbe kwa ajili ya usikivu na uchukuliwaji.

Eg. Hoja atakayoitoa babu Tale na hoja ile ile ikatolewa na Mbowe unafikiri uzito wa hoja utakaa wapi
Tunaangalia ujumbe hatuangalii sura ya mtoa ujumbe..

Hapo ndipo waafrika ilipo kasoro yetu
 
Tunaangalia ujumbe hatuangalii sura ya mtoa ujumbe..

Hapo ndipo waafrika ilipo kasoro yetu
Sio kweli,labda km haujasomea mambo ya personality na uongozi.

Kichaa au mvuta bangi na muungwana wakibeba ujumbe unaofanana atakaesikilizwa ni muungwana.

Marekani km hauna ukwasi/salio ata kama una ujumbe kutoka kwa Mungu wewe ni fala tu na hautasikilizwa...

Hii ni dunia nzima na ata ngazi za familia km hauna hela usikilizwi mkuu.
 
Ndugai hana uwezo wa kiakili kuweza kuhoji mambo kama hayo. Spika mwenye akili na anayejielewa asingeweza hata kuentertain yale mambo ya "Magufuli atawale milele atake asitake" kule bungeni, sembuse uwezo wa kuhoji mgawanyo wa fedha kati ya bara na Zanzibar?
Na Mungu akasema hivyo hivyo atake asitake.
 
Mkigawana mbao hiyo serikali ya Tz ni ipi tena..
ya Zenj au Tanganyika?
Tanganyika itarudishaje mali zake zilizoenda kujenga zenje?

Ooh una maana ikitokea talaka
Tutahesahiana tu na tutalipana pole pole ila mimi sio mzenji
Ila ni haki yangu kuchangia Boss
 
Hii ni dhana tu.
Kenya mbona haikulipa mali za EAC?

Ila tuligawana fito
Ndege tukazuia wengine mpaka mizigo yetu wakabaki nayo
Hiyo ilikuwa ni funzo ingawa hatujifunzi na kuweka mambo hadharani kuwa likitokea la kutokea itakuwaje

Tatizo kila anaengia Wimbo ni ule ule “ Ntaulinda muungano”
Hapo inaonyesha hautakufa

Lakini tunajua Yemen waliachana mara mbili na kurudiana na kuachana
Mapenzi haya
 
Back
Top Bottom