Hisia za Ng'wanangwa: Sahara Communications Waunganishe Live Show ya Tuongee Asubuhi na RFA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hisia za Ng'wanangwa: Sahara Communications Waunganishe Live Show ya Tuongee Asubuhi na RFA.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanangwa, Oct 7, 2012.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  mara nyingi Star TV imekuwa ni moja ya vituo vya TV vinavonikuna sana hasa show zao za masuala ya Siasa, Elimu, Uchumi na hata Michezo. Sabaubkubwa ni kwamba hawako biased. Thumbs Up! hapa nazungumzia show zinazorushwa moja kwa moja na kuruhusu watizamaji kupiga simu kuchangia katika mada mbali mbali zinazokuwa mezani, au hata kuchangia kupitia mitandao ya kijamii na ujumbe wa maandishi SMS.

  shaka yangu ni moja tu. watanzania wengi hasa wa maeneo ya vijijini hawana access na matangazo ya TV. wengi wana access na matangazo ya redio, na kikweli, RFA, kama moja ya radio zinazorusha matangazo kupitia njia ya satellite, wanasikika sehemu nyingi sana za nchi yetu. kwa kuzingatia ukweli huo, napenda kuwashauri Sahara Communications Ltd kuangalia uwezekano wa kuunganisha show za Star TV, hasa ile ya Tuongee Asubuhi, waiunganishe na RFA ili wakati sisi wachache tunapojinoma na runinga zetu, ndugu zangu pia kule bonde la Songwe wakiwa wanakula ugali wa asubuhi na maziwa mabichi (yaliyotoka kukamuliwa sasa hivi) tayari kwenda malishoni wawe wanapata matangazo haya muhimu.

  lazima tujenge taifa lenye watu wanaopata taarifa sahihi kwa muda sahihi. kwa kuwa Sahara Communications mmejipambanua kuitumikia jamii kwa kuipatia huduma muhimu ya habari, basi ninaomba sana muhakikishe jamii yote inapata habari, bila kubagua kuwa hawa wa mujini, hawa wa shamba.

  IPP media wanafanya hivyo sasa kwa kuunganisha Kipimajoto cha ITV na Radio One na Capital Radio.

  TBCCM wanafanya hivyo katika show ya Tuambie

  BBC wanafanya hivyo katika show yao ya BBC Have Your Say.

  You can add to that list too.

  Hisia zangu.
   
 2. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hili ni wazo murua kabisa na pendekezo hili linaweza kusaidia kushirikisha watanzania wengi zaidi kuwadhoesha mijadala.Mimi naamini kwenye mijadala ya wazi na staha inaweza kusaidia wananchi kujenga uvumilivu wa mawazo yanayotolewa na mtu mwenye mtazamo tofauti.
   
 3. a

  adolay JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,577
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  I agree,should it be implemented is a good idea and will do more better as not all the time an opportunity to avail TV sets

  exists, with radios everywhere the program can be accessed.
   
Loading...