Hisia za kidini ni ujinga au kuna ajenda ya siri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hisia za kidini ni ujinga au kuna ajenda ya siri?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by JUAN MANUEL, Feb 27, 2011.

 1. JUAN MANUEL

  JUAN MANUEL JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 655
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 80
  Juzi nilibahatika kusikiliza radio moja ya kidini, Radio Imaani, watangazaji waliokuwa studio, walinukuu gazeti moja li kiislam, likihoji suala la DOWANS ni mmliki au kanzu yake.

  Kwa mujibu wa gazeti hilo, ni kwmba hakuna tatizo lolote liloletwa na DOWANS, tatizo lililopo ni kwamba mfumo wa serikali yetu ambao ni wa kikristu ndilo tatizo, watangazaji hao wanadai kwamba mfumo huu hauwapendi waislam, unawashambulia popote walipo na kuharibu sifa yao nzuri.

  Wanadai kwamba DOWANS inashambuliwa na kusakamwa kwa sababu mmiliki wake ni wa imani ya kiislam.

  Suala lingine lililonishangaza, watangazaji hao wanaamini kwamba kinachoendelea katika nchi za kiarabu, ni conspiracy ya nchi za magharibi ambazo zimepania kuuangamiza uislam popote duniani.

  Hivi jamani kinacho endelea kwenye nchi hicho hizo mbona kipo wazi, vyanzo vinafahamika?

  Kama kuna nguvu tofauti nyuma ya yote hayo tufahamishane wakuu,
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Karibu jukwaani ndugu.
  Hizo redio ulizosikiliza watangazaji wake ni nani?
  Tuletee habari za ITV, TBC hizo zengine zisikilize halafu uwaachie wenyewe habari zao, usiwe kipaza sauti chao.
   
 3. Bupilipili

  Bupilipili Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waachie wenyewe ujinga wao.
   
 4. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  as long hawajasoma-siwalaumu-wacha vipofu waongozane wenyewe kwa wenyewe
   
 5. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Kuna aya moja niliisoma kwenye masahafu inasema;
  'Kuna wanafiki wamejenga msikiti kutia udhia na kuimarisha ukafir'
  Hao wanaoandamana wanapiga takbir na kupaza sauti Mungu ni mkuu!
  na wanajinadi wao ni Waislamu.

  Kwa mujibu wa radio imani na basalehe na wenzie watueleze na kutujuza yafuatayo;
  1-Wale ni makaafir si waislamu bali wanashirikiana na wanaafik kumpinga muislamu gadafi ambaye anavunja miskiti ya wanafiki, na kuua makafir.
  2-watueleze uislamu ni dini inayo tetea dhulma na ufisadi bila kificho.
  3-Uislamu na mafundisho yake hayajitoshelezi hadi kuingiliwa na nguvu nyingine za nje.
  Msipo jibu mnajidhihirisha nyie radio imani@company ndio WANAFIKI MLIO JENGA MSIKITI KUTIA UDHIA NA KUIMARISHA UKAAFIR.
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kujua yaliyo vichwani mwa watanzania kama hao ni kazi kubwa. Wpo kama vile wanaishi sayari nyingine wakati wao pia wanashindia mihogo kwa chumvi.
   
 7. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Radio mbao alizosema bwana mkubwa si ndo hizo. Msiamini watangazayo redio mbao.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  ANGALIZO: Kwa kuokoa nafasi, kuna mmoja amedai isitajwe redio imani hapa badala yake zitajwe ITV, TBC. Kumbukumbu zangu ni kuwa hapa imeshahi kuwekwa post inayosema kuwa TBC kuna udini kwa hivyo upo uwezekano pia kuwa hiz TV ulizozitaja hapa zikawa na udini, lakini hili ni angalizo tu, ninarudi kwenye mada.

  Wengine walioko Radio Imani ni waropokaji sana. Huchambua mambo kichwa-nchungwa na jazba bila kufanya utafiti na kusingizia dini katika kila kitu. Kusema kuwa yanayotokea Afrika ya kaskazini na nchi za kiarabu yanachochewa na maadui wa Uislamu sio kweli. Kama walikuwa wanaangalia yaliyokuwa yanatokea Misri kwa mfano, pale watu wa dini zote waliungana kudai heshima na haki zao. Waliwahi hata kusali pamoja.

  Ndugu zangu, Udini ni ujinga. Naomba nieleweke kuwa ninakusudia udini sio dini nisije nikakatiwa fatwa. Hata kama hao wanaotumia udini kwa ajili ya ajenda, bado watakuwa ni wajinga kwa sababu huwezi kuyaingiza mambo yanayohusu jamii katika udini. Mmiliki wa Dowans hata kama angekuwa wa dini, kabila au uraia gani, ni adui wa Watanzania.
   
 9. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hivi huu mgao wa umeme unawaathiri wakristo peke yao au hata waislamu? Jamani watanzania tunachotaka ni reliable source of electricity. Hizo porojo na fikra finyu tuziache. Zina waste time and energy. Hata mpagani akileta umeme wa uhakika kwa bei nzuri kila mtu awe tayari kumpokea. Ila asije kwa kujifichaficha kama huyu mzee.
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni ujinga, wanaanzisha wenyewe, wanalaumu wenyewe! Tumesha washitukia!
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kwa kosa lipi?
   
Loading...