Hisia za chuki dhidi ya wayahudi zalaaniwa Ujerumani

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
8,284
8,828
Hisia za chuki dhidi ya wayahudi zalaaniwa Ujerumani
Rais wa Ujerumani Steinmeier ametoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya hisia za chuki kwa wayahudi. Wawakilishi wa makanisa waelezea wasi wasi wao pia huku balozi wa Israel akitoa wito mitindo ya bendera kutiwa moto.




Rais wa shirikisho Steinmeier ameonya vikali dhidi ya kuongezeka hisia za chuki dhidi ya wayahudi nchini Ujerumani."Kwamba katika viwanja vya Ujerumani bendera za Israel zinachomwa moto, ni jambo lililonishitua na la fadhaa kwangu" amesema rais wa shirikisho alipomkaribisha balozi wa Israel, katika kuadhimisha miaka 70 tangu taifa la Israel lilipoundwa, sherehe zinazotarajiwa kuanza mwakani. "Mwenye kuchoma bendera, sio tu anaonyesha chuki dhahiri dhidi ya Israel bali pia haelewi au haheshimu tafsiri ya kuwa mjerumani


Kanisa kuu la kikatoliki la mjini Cologne

Makanisa mawili makuu ya Ujerumani yalaani chuki dhidi ya wayahudi

Wawakilishi wa makanisa yote mawili makuu nchini Ujerumani wameeleza pia wasi wasi wao kutokana na visa vya hivi karibuni vya chuki dhidi ya wayahudi. Katika ripoti yao iliyochapishwa na shirika la habari la KNA, viongozi hao wa makanisa wameonya na kusema visa vya chuki dhidi ya wayahudi vimeongezeka barani ulaya na hasa katika nchi za ulaya ya mashariki.

Nae balozi wa Israel Jeremy Issacharoff akatoa wito ipigwe marufuku mitindo ya bendera kuchomwa moto.

Katika maandamano yaliyoitishwa hivi karibuni, wapalastina na waturuki wanaoishi humu nchini , waliichoma moto bendera ya Israel yenye nyota ya David mbele ya lango la Brandenburg kulalamika dhidi ya uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Miongoni mwao kuna waliokuwa wakipaza sauti kudai "wayahudi wauliwe.


Msemaji wa serikali kuu Steffen Seibert

Serikali kuu pia inalaani chuki dhidi ya wayahudi

"Hakuna hisia yoyote ya chuki , si ndogo si kubwa, si dhaifu na wala si kali inayoweza kuvumiliwa nchini Ujerumani. Ujerumani inaheshimu jukumu lake la kihistoria na kujifunza kutokana na yaliyotokea katika vita vikuu vya pili vya dunia na inapinga aina yyoyote ya ubaguzi na chuki dhidi ya wayahudi" amesisitiza rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier.

Serikali kuu ya Ujerumani pia ilisema imefadhaishwa na maandamano ya mwishoni mwa wiki dhidi ya kutambuliwa mji wa Jerusalem na rais wa Marekani kuwa mji mkuu wa Israel. Msemaji wa serikali Steffen Seifert amewaambia maripota kwamba hata kama Berlin haiungi mkono uamuzi wa raisTrump, hata hivyo serikali inalaani vikali maandamano ya chuki dhidi ya Israel na wayahudi.



Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/epd/KNA(AFP

Mhariri:Yusuf Saumu
 
Vatica
Vatican nayo imekuwa kimya sana kwenye hili suala; sijui kwanini.
Mbona msimamo wao upo wazi! wanaiunga mkono Palestina. Papa mbona kila mara anakaa na viongozi wa Hamas na Fatah kujadili juu ya masuala ya Taifa mfu la Palestina.
 
UKIONA MTU KITU KIUMBE VINACHUKIWA KUPITA KIASI UJUE KINA MATATIZO.
 
alieanzisha hizo chuki ni HITLER
sio huyu
geno2.jpg
 
  • Thanks
Reactions: PNC
HAVIPENDWI VIJAMAA NDIO MAANA HATA KUFUNGUA UBALOZI IMEKUWA ISHU,SALUTE HITLER POPOTE ULIPO.WEWE NDIO ULITHIBITISHA KWAMBA HAO NI VINYAGO KAMA WENGINE,WANATUAMBIA NI TAIFA TEULE WAKATI WA HITLER SIJUI MUNGU ALISAFIRI
 
Hii vita iko mbali sisi tuko nyuma hatuwezi kuona kwa macho ya kawaida mpaka tuwe na bainokla
 
Vatican nayo imekuwa kimya sana kwenye hili suala; sijui kwanini.
Yaani Vatican wawaunge mkono Wayahudi ambao mara kwa mara humkashifu Papa na kusema ni Yesu na Papa wote ni mashetani!

Uzuri ni kwamba, nina access na news za Isreal. Na hata asiye Mkristo, anaweza kujickia vibaya the way Wayahud wanavyomkashifu Papa na Ukatoliki kwa ujumla...
so, what about Wakatoliki wenyewe?!

Kuna gazeti moja la Kiyahudi last year lilitoa a series of articles za kuukashifu Ukatoliki na Papa!

Anyway, wanaweza kutoa tamko kuridhisha umma tu lakini moyoni, wanaweza wasiwe real!!
 
Back
Top Bottom