Hisia na hamasa za Maandamano nchini: Mapokeo, Mitazamo na Uhalisia (Viongozi na Wananchi)

Unafurahia watu waendelee kuwa mafukara ili watawaliwe kijinga ba kibabe! Tunataka Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake waondoke maana hawafai. Hata PM hatuna shida naye kabisa! Shida iko kwa Magufuli pekee na baadhi ya watendaji wake ambao wamelewa madaraka!
Huwezi kusema unataka aondoke na akaondoka, kumbuka kuwa huyu alizunguka nchi nzima akiomba kura, kapigwa jua kanyeshewa mvua akitafuta kura. Kusema aondoke abakie fulani na fulani ni akili za kitoto sana.

Huamui ukiwa umekaa nyuma ya laptop yako, ni mchakato halali uliomuweka pale ikulu. Na bora uishie kwenye laptop yako, ukitoka nje na kuanza vurugu utaumia. Huyu sio JK aliyeweza kucheka na kila mtu.
 
Hawa sijashikiwa akili na wala siwazi kuandama ila mawazo yako ya cheap politics kama alizofanya pale magufuli kwa huyo mama eti ndo unatumia kuaminisha kwamba magu ni kiongozi bora lazima uwe na matatizo katika sakiti yako ya kichwa
Mkuu JPM anakwenda moja kwa moja kwa watu wa hali ya chini, hao ndio wapiga kura tofauti na hawa wasomi wanaoishi nje ya nchi.

Usidanganyike ukadhani kuwa hawa wapiga kelele humu JF wanao uwezo wa kuamua hatima ya urais, kinamama wauza magenge, wakulima na watu wa aina hiyo ndio wenye kuamua hatima ya kiongozi mkuu wa nchi.
 
Akishatukana frustrations zinaisha, nadhani wewe ndio una frustration
Mange hawezi kuheshimiwa na wanaojiheshimu, huwezi ukatoa maoni yako kwa kumtukana mkuu wa nchi, tena yale matusi ya mtaani yasiyokuwa na staha.

Jamii ya vijana wa facebook wenye kutumia matusi ya hovyo ndio wenye kumuunga mkono huyu dada.
 
Mkuu JPM anakwenda moja kwa moja kwa watu wa hali ya chini, hao ndio wapiga kura tofauti na hawa wasomi wanaoishi nje ya nchi.

Usidanganyike ukadhani kuwa hawa wapiga kelele humu JF wanao uwezo wa kuamua hatima ya urais, kinamama wauza magenge, wakulima na watu wa aina hiyo ndio wenye kuamua hatima ya kiongozi mkuu wa nchi.
Unafiri sijui kwamba hawana uwezo ila haribatirishi msimamo wangu juu ya baadhi ya mapungufu ya jpm

Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
 
Hello pipoz

Wanaanza kuyaongelea maandamano ya tarehe 26/4 na kutoa vitisho kwa kutumia jeshi la polisi, hivi bado hawajajifunza saikolojia ya watanzania??????

Hiyo tarehe 26/4 hakutakuwa namaandamano yoyote, na hata yakiwepo hayatokuwa na effect yoyote, hiyo tarehe 26/4 itapita kama siku ingine..

Mm ndo ningekuwa raisi/kiongozi wa ngazi ingine serikalini hlf nasikia maandamano yanaanzishwa kwenye mitandao, ndo kwanza ningepunga upepo na kunywa juisi, UKWELI NI KWAMBA WATANZANIA HATUNA UBAVU WA KUANDAMANA, WATANZANIA SISI NI WAOGA SANA, kwamfano hata raisi leo aseme anapandisha kodi mara 5000, im 100% sure hakuna mtanzania atakayeandamana tarehe 26/4

Kama mnabisha sisi si tupo? tutajionea wenyewe hiyo siku ikifika...
 
Unajua kilichomuangusha Madarakani Keneth Kaunda Rais wa Kwanza wa Zambia dhidi ya Fredrick Chiluba 1991?

Alimdharau Chiluba Kwa kuwa alimuona Mtu WA kawaida sana kumuangusha

CCM haiwezi kufanya kosa la Chiluba, alikuwa anacheza Table tennis wenzie wanamwambia Mzee Hali ngumu Yeye anajibu wa kuniangusha Zambia Hata Wazazi wao hawajagusanisha Vitovu
 
Hello pipoz

Wanaanza kuyaongelea maandamano ya tarehe 26/4 na kutoa vitisho kwa kutumia jeshi la polisi, hivi bado hawajajifunza saikolojia ya watanzania??????

Hiyo tarehe 26/4 hakutakuwa namaandamano yoyote, na hata yakiwepo hayatokuwa na effect yoyote, hiyo tarehe 26/4 itapita kama siku ingine..

Mm ndo ningekuwa raisi/kiongozi wa ngazi ingine serikalini hlf nasikia maandamano yanaanzishwa kwenye mitandao, ndo kwanza ningepunga upepo na kunywa juisi, UKWELI NI KWAMBA WATANZANIA HATUNA UBAVU WA KUANDAMANA, WATANZANIA SISI NI WAOGA SANA, kwamfano hata raisi leo aseme anapandisha kodi mara 5000, im 100% sure hakuna mtanzania atakayeandamana tarehe 26/4

Kama mnabisha sisi si tupo? tutajionea wenyewe hiyo siku ikifika...
Yaani huu waitwa uhamasishaji maandamano kwa kutumia "mlango wa nyuma" ... sie yetu macho na "mashikio"
 
I mean hata mtu mmoja akionewa tunapaswa kipaza sauti. uko sahihi sana

unapazaje sauti? unawaambiaje watu waelewe? wana utayari kwa kiasi gani? wanalazimishwa au wana hiyari?

huyo mmoja anayeonewa anaonewa na nani hasa with tangible evidences?

- Chama tawala kinapaswa kuwa cha kwanza kupaza sauti kwa ajili ya hao wachache wanaoonewa. Hii ni pamoja na viongozi wengine waliopo madarakani (katika serikali iliyopo)

- Viongozi wa asasi nyingine (tofauti na serikali) pamoja na wale wa vyama vya upinzani ndio wa pili kupaza sauti baada ya .kuna chama kimeshindwa kuwajibisha wawakilishi wake waliopo madarakani. Watumishi wengine wa serikali pia ama kwa kuwa wanafaidika au kwa hofu nao wameshindwa kupaza sauti.

- Hakuna muda maalumu wala tukio maalumu la kusema watu wapo tayari. Wafaransa walifikia kikomo baada ya malkia kuwaambia wale keki kama hakuna mikate. Sehemu nyingine ni tukio kubwa zaidi. Sasa hivi huko Marekani ni vijana wadogo wa sekondari ndio wanaoonekana kufanikiwa kwenye kampeni ya gun control. In short hakuna formula ya utayari au tukio.

- Huyu mmoja anaonewa na raisi na wawakilishi wake wote. Anaonewa na matamko ya raisi yaliyo na double standard. anaonewa na matamko ya sishauriki. Nayo yanaigwa na watumishi wengine wa kuteliwa na kuchaguliwa. Hapo kabla maneno ya watu yalikuwa 'tusubiri baada ya miaka mitano tutamtoa huyu' lakini jinsi hali inavyozidi kwenda hiyo sentensi inazidi kupotea. It is just a matter of time watu watapata more courage...only time!
 
Maandamano ni haki yetu watanzania kikatiba na wanaopinga maandamano, na maneno mengi, ni kuvunja katiba, na kwa sababu watanzania ni watu wa Amani tunaburuzwa.
 
Mimi ninacho ona kwa sasa ni kushilikiana kujenga Tanzania moja na kusubili uchaguzi ujao haya mambo ya maandamano HUSABABISHA amani kupotea kuna vijana wengi wanategemewa kwenye familia zao sioni kama ni haki kwenda kuandamana na kufanya uhaini si DHANI kama mange yupo sahihi
 
  1. Kushambuliwa Tundu Lissu
  2. Kukamatwa kwa Nondo Abdul
  3. Kupotea kwa Ben Saa nane
  4. Kutetewa/kulindwa kwa DAB
  5. Kufukuzwa wafanyakazi 10000+ na kunyimwa mafao yao
  6. Kufutwa/kuungwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii
  7. Kushuka kwa bei za mazao
  8. Kuliwa ambirambi za luck vincent
  9. Bomoa bomoa mbezi kimara
  10. Kuliwa kwa fedha za misaada ya tetemeko Bukoba
  11. Kutishiwa kwa watu wanaohoji serikali
  12. Kupungua madawa hospitalini
  13. Kunyanyaswa kwa watu wasio na hatia
  14. Kupanda kwa bei za bidhaa muhimu
  15. Kifo cha Akwilina
  16. Gharama za kurudia uchaguzi kutokana na hama hama ya viongozi kwenda CCM
  17. Kudhulumiwa katiba yetu
  18. Viongozi wa dini wa kukandamizwa
  19. Viongozi wa kisiasa kukandamizwa
  20. Teuzi za madaraka za upendeleo na ukabila
  21. Kupendelewa kwa Chato bila kuwa na ulazima
  22. Matumizi mabaya ya pesa
  23. Matumizi mabaya ya madaraka
  24. Kuachiwa kwa walawiti wa watoto kwa msamaha wa rais
  25. Kunyima wanafunzi wa kike wenye mimba kusoma na kuwafunga baba zao kwa miaka 30
  26. Rushwa na unyanyashaji Jeshi la Polisi
  27. Mishahara kutokupanda kwa miaka zaidi ya 3
  28. Walimu kuhamishiwa shule za msingi bila kufuata taratibu
  29. Unyanyasaji wafanya biashara kwa kutozwa kodi kubwa na TRA
  30. Dhuluma ya waziwazi dhidi ya wanyonge
  31. Kuminywa uhuru wa habari
  32. Kuminywa uhuru wa bunge
  33. Kuminywa uhuru wa mahakama
Kama hizi sababu hazikupi sababu ya kushiriki basi uzalendo wako ni wa mashaka

Wasalam

PBK
 
Ina maana hamtaenda makazini? Maana inasemekana ni nonstop. Mkinusurika kuvunjwa miguu basi mjiandae kukosa kazi baada ya kumaliza maandamano.
Nahisi kama waandamanaji wengi ni wanafunzi na majobless, mtu mwenye ajira ya maana sidhani kama ataandamana!
 
Kwani jobless nani kasababusha? Unemployment ni moja ya sababu ya kuandamana
 
Kwani jobless nani kasababusha? Unemployment ni moja ya sababu ya kuandamana
Sikatai madai ya msingi mnayo, ila ukweli ni kwamba asilimia 99.9999 ya watakaoandamana ni majobless na wanafunzi. Point yangu ni hiyo tu mkuu...sipingani na madai yenu.
 
Back
Top Bottom