Hisia mbaya na uelewa mdogo wa polisi wetu (NBC Meru Branch - Arusha)

Igembe Nsabo

Member
Jun 4, 2010
87
14
Ndugu wana JF, Leo nilikuwa nimekwenda NBC Arusha, (Branch ya Meru), Nimekuwa mteja wa NBC kwa miaka kumi sasa sijawahi kukutana na hii ya leo, mie nilianzia kwenye ATM na rafiki yangu aliingia ndani kutuma pesa kwa familia yake, cha ajabu mie baada ya kuchukua pesa kwenye ATM nikawa pale nje namsubiri huyo jamaa yangu kwani ndani palikuwa hapana hata nafasi ya kuweka mguu, watu wamejaa ile mbaya, nikiwa nimesimaa hapo nje na watu wengine ambao walikuwa either wanasubili jamaa zao waliokuwa wanapata huduma ndani au wanasubiri kupata huduma kwenye ATM, cha kusikitisha kulikuwa na Polisi wawili mmoja yuko ndani ya kijengo cha Polisi alikuwa kavaa uniform na kajifunga nguo ya kimasai kuashiria kujikinga na baridi kari ya Arusha na mwingine yuko nje na SMG yake. Yule askari wa aliyejifunga nguo ya Kimasai akaanza kuniuliza mbona umesimama hapa?. Niko namsubiri jamaa yangu yuko ndani, je unataka niwe wapi?. Toka hapa wewe hujui hili ni eneo la Benki, wewe unaweza kuwa MWIZI au unataka kuchora DIRI uibe Benki, na maneno kibao akaongea, nami nikiwa namsikiliza, mwishowe nikamjibu kwa kumwambia ya kuwa.

Je ni sahihi watu wote walioko hapa kukaa hapa? na huyo Jamaa anaye wauzia Mayai nyie ambae kaweka hapa trei zake hapo na anafanya biashara hapo yuko sahihi?, Je hili ni eneo la kufanyia biashara ya Mayai?. Kama ukiwatoa wote hapa na mie natoka, maanake kama ni kuvunja sheria wote tumevunja, iweje mie kusimama hapa niwe nimekosea!!! au unishuku kuwa nimekuja kuiba Benki? au kuchora DIRI?? kwani mie niko tofauti na wengine?.

Mytake: Si kila mtu aendae BENKI ni mwizi au anachora DIRI la kuibia Benki na isitoshe Tawi hilo ni dogo na haliwezi kuhudumia watu au halina hata sehemu ya watu kupaki magari yao wanapokwenda kupata huduma hapo benki, na hata transaction zake kwa mtazamo wa haraka haraka ni kidogo, hakuna hata mteja anayeweza kuja na pesa zake nyingi kwani Tawi lile limekaa mahala pabaya, hakuna sehemu ya kupaki hata gari, gari lako uliache barabarani, pale palifaa kuwa na ATM tu na si kuwa na Huduma zingine za kibenki kwa mle ndani. Ndugu zetu hawa wao wakiona mtu wanajua ni mwizi, na hata kauri pia zinaweza zikawa si nzuri.
Kama unaona hilo si eneo la kukaa watu, kila mtu anapopata huduma mwambie atoke pale, ni si kwa mtu mmoja tu, uwe fair kwa wote.
 
pole sana.....ni jumatatu haijakukalia vizuri...au labda huyo polisi hakuwa na hela ya kununua mayai...ni vijimamboooo tuuuuu.....mpotezee
 
pole sana.....ni jumatatu haijakukalia vizuri...au labda huyo polisi hakuwa na hela ya kununua mayai...ni vijimamboooo tuuuuu.....mpotezee
Inawezekana Preta, na sometime ni uelewa wa hao ndugu zetu, wengi wanakuwa hawajapelekwa kusoma mind za watu kuwa huyu anafikiria nini na nini anaweza kufanya nini na kwa wakati gani! wezetu, polisi ni lazima awe na uelewa mkubwa na asitumwe na HISIA. Ndio maana unaona watu wanabambikiziwa kesi ya wizi, mauwaji, uzururaji. kwa nchi yetu unyanyasaji unakuwa mkubwa pale tu mtu huyo anaposhindwa kutambua haki yake ya KIKATIBA kwa kutokuelewa.
 
Hii nayo siasa, please pelekeni sehemu husika si kubandika. Habari mchanganyiko, Malalamiko, au biashara
 
Kwani ulikuwa umevaa vaaje? Maana hawa polisi kutokana na kiitelijensia chao wanajua nguo za vibaka, majambazi na walalahoi pia!!
 
Akiwa kazini ana haki ya kutilia mashaka mtu au kitu chochote,
hivyo mashaka yake ni ya kikazi, mwizi au mchora dili hana alama yeyote,
nilichokiona hapa kwa maoni yangu ni kule wewe na yeye kubadilishana maneno ya ujuaji tu
 
Pole aisee mi mwenyewe nshawahi kupata masahibu pale na haohao polisi
 
upolisi mabavu huo, hawa majamaa wasikushangaze wengi div 5 hawajifikirishi kabisa.
 
Back
Top Bottom