Wakuu nimekua nikisikia 2 hilo neno lakin cjui jinsi ya kufaidika na hzo hisa,mwenye uelewa kuhusu mambo ya hisa anieleweshe bac.na je m2 wa low income unaweza kununua hzo hisa na ukafaidka nazo kwel?
Hisa ni sehemu ya mtaji anayowekeza mtu kwenye biashara. Kwa mfano Kampuni inaweza kuanzisha biashara na mtaji wa Tshs. 100,000.00 na kuwa na hisa 100 zenye thamani ya Sh. 10,000 kila hisa. Hivyo ukinunua hisa 2 utalipa sh. 20,000.00. Biashara ya hisa hufanyika kwenye soko la hisa kupitia kwa wakala. Faida ya kununua hisa ni kupata gawio kutoka katika sehemu ya faida ilioypatikana pia kutokana na kupanda kwa thamani ya hisa wakati wa kuuza. Katika kununua hisa kama katika biashara yoyote unaweza kupata hasara.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.