Nimesikia Tangazo Moja Kuhusu HISA, naomba ufafanuzi zaidi

zukisa

Member
Feb 8, 2017
47
28
Habarini za sahizi wana JF,
Kuna Tangazo hapa nimelisikia Kuhusu HISA,

Na wanasema kwamba HISA moja unapata kwa 400/=Tsh.

Naombeni ufafanuzi wana JF Kuhusu HISA,

Ipoje??
Nini faida yake??
Ni mtazamo mzuri kununua??
 
Hizo ni hisa za TCCIA wako wanafanya IPO kuanzia tarehe 1 febr hadi 31 March na kweli hisa moja ni shs. 400/=
 
Habar zenu Wadau
Nimesikia redio ya Planet Fm ikitangaza kuhusu Hisa za TCIA kuwa zinauzwa pale CRDB kwa sh 400 kwa hisa moja.

"Nimevutiwa na bei yao"

Plz naomba mwenye kuelewa vizur hawa TCIA maana nataka niwekeze kwao but nahitaji nipate Elimu nijiridhishe nisije nikaingia mkenge kwenye Kampun ambayo ina low performance hivyo uwezekano wakupata Loss ni mkubwa ukilinganisha na kampuni zingine..
 
Kabla yakununua hisa za toleo la awali ni vyema ukosoma kwa makini waraka wa matarajio, waraka wa matarajio unaweza kupata katika mtandao (tovuti yao, ya soko la hisa, ya mamlaka ya mitaji na dhamana, google, n.k). kumiliki hisa ni kumiliki sehemu ya kampuni na sio kumiliki kipande cha karatasi hivyo ni vyema kujua shughuli ya kampuni unayotoka kuwekeza. Kokotoa thamani ya hisa na linganisha na bei ya hisa, soma kuhusu sera ya gawio, soma kuhusu taarifa ya mwanasheria huru, angalika kamakuna uongozi na utawala bora, kwa ujumla jifunze kila kitu kuhusu kampuni unayotaka kuwekeza.
TIC ni kampuni inayojishughulishana masuala ya uwekezaji, inamiliki hisa za kampuni nane zilizoorodheshwa katika soko la hisa la Dar es salaam ( TBL, NMB, TCC, DCB, CRDB, SIMBA, SWISSPORT, TWIGA). Ina ufanisi mzuri, haina madeni, inamiliki blue chip stocks, ina historia nzuri, ina maeneo mengi mapya mazuri inayoweza kuwekeza ( Hatifungani, hisa za makampuni ya simu yatakayojiorodhesha, hisa za Benki zitakazijiorodhesha, kuwekeza katika nyumba, microfinance, dalali wa soko la hisa, n.k)
Mapungufu yake:
1. Bei ya hisa ni kubwa kuliko thamani halisi ya hisa, hisa moja wanauza 400 lakini ukiingia sokoni leo tarehe 21/2/2017 ukanunua hisa zilezile na idadi wanayomiliki utanunua kwabei rahisi zaidi. Bei ya hisa ingetakiwa iwe 350 (NAV is 356 according to my calculation )
2.Ukisoma waraka wa toleo la awali utaona kuwa kuna kesi mahakamani, endapo kampuni itashindwa itaathiri sana thamani ya kampuni
3.Sera ya gawio, 50% ya faida itatolewakama gawio, kama unawekeza kwa ajili ya kukua kwa mtaji hili sio jambo zuri kwa maana litaathiri ukuaji wa thamani ya kampuni (intrinsic value). ila kama lengo lako ni kupata gawio hili ni jambo nzuri.
4. Inatarajia kuanza kufanya shughuli ambazo haina uzoefu nazo (Microfinance, investment in agri business etc), hivyo inaweza isifikie malengo yake.
5.Uchache wa wafanyakazi, pia inabidi ufanye utafiti wa makini kuhusu uongozi na utawala bora wa kampuni. kuna uhusiano mkubwa kati ya ufanisii wa kampuni na utendaji wa viongozi
Ushauri:
Nunua, lakini tumia kiasi ambacho hatakama utapoteza hakitakuathiri sana.
Hayo ni mawazo yangu na sio mawazo ya kitaalamu, hivyo sitakuwa na dhima kama utafuata ushauri wangu na ukapata hasara.
 
Great!! I observed the same thing, bei za hisa walizotumia kukokotoa hiyo IPO price ya 400 ni za mwaka jana wakat bei ziko juu, wakati sasa hivi bei zimeshuka sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom