Hisa za NMB zimeshuka kwa 50% ndani ya miezi 12

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
BEI YA HISA MOJA YA NMB TAREHE 04/02/2015 ILIKUA NI TSHS. 4,290
JANA TAREHE 04/02/2016 BEI ILIKUA NI TSHS. 2,200
UKIPIGA HESABU HAPA UTAKUTA ZIMESHUKA KWA KARIBIA 50%
TATIZO NI NINI?? AU NI KAWAIDA TU? MAANA BENKI INAFANYA TU VIZURI ILA HISA ZINAPOROMOKA BALAA, UTADHANI UMERUSHA MPIRA PALE MLIMA KITONGA
 
HATA mimi nashangaa mkuu maana kunakipindi ilifika 4000+ leo iko 2150 sielewe tatizo ni nini, nafikiria kuuza hisa zangu kwa kweli!!
 
Watu wengi wanauza hisa zao ndio maana zinashuka.... ila biashara ya hisa nayo mmmmmh
 
Aiseee ukanunua hisa za benki kabisa?inabidi uwe strategic na mtu mfuatiliaji haswa maana mchezo wa kununua hisa unachezwa na wakubwa, mnangojewa tuu vidagaa muanze kuuza hisa zenu halafu zinapanda bei
 
Watu wengi wanakimbilia kununua hisa bila kuelewa kuwa kuna kupata na kukosa katika soko la hisa; soko la hisa sio sawa na SAVINGS ACCOUNT ya benki!! Kuna umuhimu kwa wananchi kuelimishwa zaidi juu ya soko la hisa kwani kuna wajanja wanaweza kulitumia soko hilo kuwaibia wananchi wasiokuwa na uelewa; mfano mzuri ni jinsi wale wazee wa NICO walivyojifanya wazalendo kumbe ndio njia ya kuwadhulumu maskini wadanganyika na serikali imekaa kimya bila kuwasaidia wapate chao kutoka kwa hawa wezi!!!
 
Kuna ishu ya serikali ya kupeleka pesa zao BOT
na vilevile kuna ishu ya Mwalimu bank kuanza

nafikiri hivyo viwili vimeleta fear kuwa bank itayumba
halafu decembe na january watu wana njaa
kwa hiyo wanauza hisa ili wafanye matumizi
nna uhakika hisa by june zitakuwa juu

huu ndo wakati wa kununua
 
sure, walifanya hivyo wakati swala inaingia sokoni. raha ya soko la hisa uwe na pesa nyingi, na info za kutosha
 
huu ndo wakati wa kununua

What factors have you considered to make that determination? Trading in stocks is not palm reading!!!!Hisa haziuzwi au kununuliwa kwa kupiga ramli; unaweza kununua hisa sasa kutegemea zitapanda bei badala yake ndio zikaendelea kushuka,,na ndio utakuwa umeliwa zaidi!
 
Ishu ya mwalimu bank wala haina nguvu hapa ishu ni serikali kutoa pesa zake kwenye mabank ya biashara NMB ikiwemo na bado wasipokuwa wabunifu watayumba sana,wajipange kwakweli.
 
kweli kabisa, hii biashara saa nyingine inaweza ikakuua kwa pressure
 
Ishu ya mwalimu bank wala haina nguvu hapa ishu ni serikali kutoa pesa zake kwenye mabank ya biashara NMB ikiwemo na bado wasipokuwa wabunifu watayumba sana,wajipange kwakweli.
mkuu mbona hizi hisa zske zimeanza kushuka kwa kasi kuanzia mwaka jana kabla ya serikali kufanya huo uamuzi? na kama sababu ni hiyo mbona wenzao wa crdb wapo almost stable?
 
sure, walifanya hivyo wakati swala inaingia sokoni. raha ya soko la hisa uwe na pesa nyingi, na info za kutosha
hizo info utazitoa wapi maana wale ma broker wenyewe wanashindwa kujibu, sijui ni makusudi au ni kukosa uelewa sijui
 
Watu wengi wanakimbilia kununua hisa bila kuelewa kuwa kuna kupata na kukosa katika soko la hisa; soko la hisa sio sawa na SAVINGS ACCOUNT ya benki!! Kuna umuhimu kwa wananchi kuelimishwa zaidi juu ya soko la hisa kwani kuna wajanja wanaweza kulitumia soko hilo kuwaibia wananchi wasiokuwa na uelewa; mfano mzuri ni jinsi wale wazee wa NICO walivyojifanya wazalendo kumbe ndio njia ya kuwadhulumu maskini wadanganyika na serikali imekaa kimya bila kuwasaidia wapate chao kutoka kwa hawa wezi!!!
wanatumia mechanism gani mkuu hebu tuambie
 
HATA mimi nashangaa mkuu maana kunakipindi ilifika 4000+ leo iko 2150 sielewe tatizo ni nini, nafikiria kuuza hisa zangu kwa kweli!!
nakushauri fanya utafiti vizuri ujue tatizo ni nini, maana zinaweza kuja kupanda kwa kasi tena, ukajilaumu
 
hizo info utazitoa wapi maana wale ma broker wenyewe wanashindwa kujibu, sijui ni makusudi au ni kukosa uelewa sijui
info zinapatikana ila kwa taabu sana. soko lenyewe bado lipo nyuma kibiashara. ma-broker wana-hold info wenyewe na ndo maana wanapiga pesa sana, nimeshafanya nao kazi.
 
Mimi hadi Leo najuta kununua hisa CRDB!
Mwaka juzi January nilienda kununua hisa!
Siku hiyo nikakuta bei ni Tshs 435! Nikaona nitoe kiasi kikubwa ili nipate hisa nyingi. Kosa nililofanya ni kwamba ile fomu niliyojaza kununulia nilijaza nanunua kwa market price!
Baada ya wiki moja niliporudi kwa broker ananiambia bei ilipanda hadi tshs 500 kwa hisa. Aisee fikiria tangu mwaka juzi hadi leo hii bei ya hisa haijawahi kurudi tena kwenye hiyo Tshs 500! Inacheza 380 hadi 450!
Loss ni kubwa mno nafikiria kuziuza hivyo hivyo kwa bei ya hasara sasa!
Sitarudia kununua hisa tena!
Mwaka jana nilipata gawio la Tshs 1,800,000/- kwa hela niliyoweka huko naamini ningeifanyia business yoyote nyingine ninge make zaidi ya hiyo!!
 
usiuze kwa sasa, subiri AGM then uangalie bei!
 
info zinapatikana ila kwa taabu sana. soko lenyewe bado lipo nyuma kibiashara. ma-broker wana-hold info wenyewe na ndo maana wanapiga pesa sana, nimeshafanya nao kazi.
ahaaa kumbee? huu upuuzi wa kununua hisa sitakaa nifanye tena, afadhali hata niweke m-pawa
 
Back
Top Bottom