HISA za kampuni ya Acacia PLC inayojihusisha na uchimbaji madini nchini zimepanda bei kufikia TZS 7,000

Jan 3, 2017
11
38
HISA za kampuni ya Acacia PLC inayojihusisha na uchimbaji madini nchini zimepanda bei kufikia TZS 7,000 kwa hisa moja baada ya kushuka wiki iliyopita ambapo zilishuka hadi kufikia TZS 6,750 kwa hisa moja Jumanne ya wiki hiyo kabla ya Jumanne ya wiki kupanda tena. Kampuni hiyo iliyoorodheshwa kwenye masoko ya hisa matatu, Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE), Soko la Hisa la Nairobi (NSE) na Soko la Hisa la London (LSE) inamiliki migodi mitatu ya dhahabu hapa nchini.

Kampuni hiyo ambayo hivi karibuni iliingia kwenye mgogoro na serikali ya Tanzania juu ya ukwepaji kodi ambayo ilidaiwa kuwa nk $ 190 billioni (Zaidi ya TZS 400 trillioni) inamiliki migodi ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu.

Kupanda kwa bei ya hisa za kampuni hiyo kulipelekea mtaji wake kuongezeka na kufikia TZS 2.8 trillioni kutoka TZS 2.7 trillioni kwa wiki iliyopita. Hata hivyo, bei ya hisa za kampuni hiyo zimepanda licha ya kutokuwepo kwa hisa zozote zilizouzwa ama kununuliwa, lakini hiyo imechangia baada ya taarifa za kampuni ya Barrick Gold Corporation inayomiliki hisa 63% za Acacia PLC kutaka kununua hisa zilizobaki na kuimiliki kampuni hiyo kwa asimia zote!

Pia hisa za kampuni ya Jubilee Holdings PLC wiki hii zilipanda kutoka TZS 7,750 hadi TZS 8,200 kwa hisa moja. Kupanda huko kwa hisa za kampuni hizo mbili zenye mtaji mkubwa ndani ya DSE pia kulifanya soko kufanya vizuri kwa wiki hii tofauti na wiki iliyopita.

Kuongezeka kwa mtaji wa kampuni hizo zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE) kulifanya pia mtaji wa soko hilo (Market Capitalization) kuongezeka kutoka TZS 19.155 trillioni hadi kufikia TZS 19.178 kama ilivyorekodiwa mapema Jumatatu ya wiki hii.

Licha ya hisa za kampuni hizo mbili ambazo pia zimeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Kenya (NSE) kupanda bila ya hisa yoyote kuzwa na kununuliwa, pia ripoti za DSE zinaonesha kuwa siku ya Jumanne ya wiki ilifanyaka biashara yenye mauzo ya thamani ya TZS 53 millioni kutokana na mauzo ya hisa zipatazo 338,395 za hisa zote za kampuni zilizoorodheshwa ndani ya soko hilo.

Mauzo ya hisa za Benki ya CRDB yalikuwa ni TZS 32 millioni, huku mauzo ya hisa za kampuni ya TPCC yakiwa ni TZS 20.2 millioni na mauzo ya hisa za TCCL wakiwa ni TZS 704,440 na vilevile mauzo ya hisa za kampuni ya Vodacom yakiwa ni TZS 266,000 katika mauzo ya miamala miwili pekee ya hisa za kampuni hiyo kubwa ya mawasiliano nchini ambapo hisa moja ya Vodacom iliuzwa TZS 760, huku mauzo ya DSE Plc yakiwa ni TZS 118,800 baada ya mauzo ya hisa 110 za kampuni hiyo katika miamala miwili tofauti!



#Mwenda ND,

Source: Gazeti la THE CITIZEN, Toleo Namba 5060 la Tarehe 22 Agosti 2019 Ukurasa wa 19.

FB_IMG_1566540724413.jpeg
 
DSE kuna siku hapa katikati walivunja records kwa kufunga siku na mauzo ya Tsh elfu(40,000) kwa siku.
 
Hisa hazijauzwa wala kununuliwa zinapandaje thamani???
Unajiita "Econometrician" halafu hujui hata mambo haya madogo yanavyokwenda Mzee! Listen, "The share price can increase for different reasons, it might be because the overall performance of the industry sector is increasing or the research and development of products or services itself may influence the price of shares to increase, also even the increase of the price of product or service of a certain a company can make price of shares to increase despite of having no counter made. TUMEELEWANA?
 
Back
Top Bottom