ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati Maalumu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kupitia na kupendekeza maboresho ya sekta ya madini nchini, Jaji Mark Bomani, amesema hatua ya kampuni ya African Barrick Gold kuuza hisa zake haina uhusiano wowote na pendekezo lililotolewa na kamati yake kwa serikali juu ya uuzwaji wa hisa za makampuni ya madini.
Kauli hiyo ya Jaji Bomani inapingana na ile ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, aliyekaririwa na gazeti hili Jumatano iliyopita akiielezea hatua hiyo ya Barrick imetokana na pendekezo la kamati hiyo lililotaka kampuni za madini ziuze hisa zao. Zitto alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
Vyanzo mbalimbali vya kuaminika ndani na nje ya nchi, hivi karibuni vilithibitisha kuwa kampuni hiyo inayomiliki migodi kadhaa ya dhahabu ndani ya ardhi ya Tanzania, imeamua kuuza asilimia 25 ya hisa zake katika soko la hisa la London kuanzia Machi 29 mwaka huu, chini ya ufadhili wa benki kubwa ya kimataifa ya JP Morgan.
Akizungumza kwa simu na Tanzania Daima, jana, Jaji Bomani, alisema kamati yake ilipendekeza kila kampuni ya madini itoe asilimia 10 ya hisa zake bure kwa serikali na asilimia 15 ya hisa hizo ziuzwe katika soko la hisa nchini ili kutoa fursa kwa wananchi nao kuwa sehemu ya wamiliki wa migodi hiyo, mambo ambayo bado hayajatekelezwa.
Sisi tulipendekeza asilimia 10 ya hisa za kampuni za madini zitolewe bure kwa serikali na asilimia 15 ziuzwe kwa wananchi hapa nchini. Sasa hiyo hatua ya Barrick kuuza hisa zake kwenye soko la London sijaelewa maana yake nini. Haina uhusiano na pendekezo letu, tulichopendekeza bado hakijatekelezwa, alisema Jaji Bomani.
Alipoulizwa kwa nini mapendekezo hayo ya kamati yake iliyopewa nguvu na Rais Kikwete hayajatekelezwa mpaka leo huku Barrick ikiuza hisa zake kwenye soko la hisa la London badala ya Dar es Salaam, alisema: Kwa kweli mimi sielewi uamuzi huo wa Barrick kuuza hisa zake una maana gani......lakini kazi yetu ilikuwa ni kutoa mapendekezo tu. Uamuzi wa kuyatekeleza au kutoyatekeleza bado ni wa serikali.
Kwa upande wake Zitto aliisifu Barrick kwa kuamua kuuza hisa zake na kuielezea hatua hiyo kuwa itatoa fursa kwa wananchi kumiliki uchumi wao.
Baada ya kuona kuwa serikali imelazimisha kampuni za simu kuuza hisa soko la hisa wao wameamua kuuza bila kusubiri kusukumwa, wamesalimu amri.
Hatua hii ni muhimu sana kwani itawafanya Watanzania wamiliki sehemu ya utajiri wao na sasa ni wakati wa serikali kuweka mkakati maalumu wa kuhakikisha kuwa taasisi za Tanzania na Watanzania wengi zaidi wanamiliki hisa hizi, alisema Zitto.
Hata hivyo, Zitto alitaka hisa za Barrick katika soko la Dar es Salaam ziuzwe sambamba na zile za soko la hisa la London ili kutoa fursa kwa Watanzania.
Aidha, alimtaka Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuruhusu mashirika ya Tanzania kama mifuko ya hifadhi ya jamii kununua kwa wingi hisa za Barrick huko London kwa manufaa ya taifa.
Mwaka 1999 serikali ilikuwa inamiliki asilimia 15 ya hisa za mgodi wa Bulyanhulu na kuziuza kwa bei ya kutupwa. Madhara yake sasa ni kununua hisa hizo tena pamoja na za migodi mingine kwa bei kubwa zaidi, alisema Zitto.
Alisema hatua hiyo ya Barrick itaiweka katika mtego kampuni ya Anglo Gold Ashanti ambayo hisa zake zinauzwa katika soko la Johannesburg hivyo itailazimisha kampuni hiyo nayo kuweka hisa zake katika soko la Dar es Salaan.
Kwa hatua hizi, soko la Dar es Salaam litachangamka sana kwa kuwa na mtaji mkubwa zaidi. Hii itafanya makampuni mengi zaidi na hasa ya binafsi nayo kuorodhesha hisa katika soko hili na hivyo kuwafanya Watanzania wengi zaidi washiriki katika uchumi, alisema Zitto.
Kampuni ya African Barrick Gold ina thamani ya dola za marekani bilioni 4 ambazo ni sawa na robo ya uchumi wa Tanzania kwani pato la taifa la hadi kufikia mwaka jana lilikuwa dola za marekani bilioni 16.
Taarifa nyingine za kuaminika zimelithibitishia gazeti hili kuwa tayari kampuni hiyo inayomiliki migodi kadhaa ya dhahabu nchini, imeshaanza kulipa kodi ya mapato ya mgodi wa Tulawaka, hatua ambayo Zitto alisema pia inatekeleza mapendekezo ya kamati yao yaliyotaka kila mgodi utozwe kodi yake badala ya utaratibu wa awali ambapo kampuni za madini zilikuwa zinalundika gharama kwa kuchanganya migodi na hivyo kukwepa kulipa kodi.
Mbali ya Jaji Bomani na Zitto, wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM) na mwanasiasa mkongwe Iddi Simba.
Wengine ni Peter Machunde anayetoka Soko la Hisa, Dar es Salaam na David Tarimo, Kutoka Kampuni ya Price Water Coopers.
Alikuwemo pia Maria Kejo, ambaye ni Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa.
Hadidu za rejea za kamati hiyo zilikuwa ni kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini.
Aidha, mengine yalikuwa ni kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, kuchambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na mwenye rasilimali (serikali), na kukutana na wadau wa madini.