Hisa za ACACIA zaendelea Kuporomoka kutoka sh.13,070 Siku ya Jumanne Leo zinauzwa kwa sh.8,800

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Wawekezaji wameendelea kutokua na Imani na Kampuni ya Acacia Mara baada ya Kuvuliwa Nguo na Ripoti ya Rais John Magufuli kuhusu Kiasi cha Madini kilichomo katika Mchanga unaosafirishwa Nje ya Nchi kwenda Kuchenjuliwa.

Hisa za Acacia zilizokua zimeporomoka kwa 15.91℅ hazijaonesha kuimarika tena ambapo Jana Kampuni ya Acacia iliendelea Kudondokea pua kwa kushuka zaidi kwa 19.47%.

Hisa hizi za Kampuni inayochimba dhahabu ziliuzwa kwa sh. 10,990 Siku ya Jumatano lakini Jana Ziliendelea Kuelekea Kusini zaidi kwa kufikia Sh. 8,800 kwa hisa hii inaonesha ni Jinsi wawekezaji walivyokosa Imani kwa Kampuni yao.

Siku ya Jumatano Rais Magufuli alitangaza kuendelea Kusitisha Ushafirishaji wa Mchanga wa Madini kufuatia Ripoti aliyoiunda kugundua kuwa Acacia waliokua wanadanganya Kiasi cha Madini yalikua yamo hivyo Kulikosesha Taifa Mapato ya Kodi.

Vilevile hisa za Acacia ziliendelea Kuangukia Pua katika Soko la hisa la Londoni (LSE)

Majira ya Saa 15:30 (Saa za UK) hisa za Acacia ziliuzwa kwa £261.50 wakati hili lilikua anguko la 14.36℅ kutoka Bei ya £308.36 Bei waliyofungulia nayo Jana asubuhi 8:00 (Saa za Uingereza). Siku ya Jumanne hisa zilifungwa na Bei ya £427.6

Pamoja na Kampuni Kutokuabaliana na Taarifa ya Tume ya Magufuli bado wawekezaji wanaonekana hawajasikia la Mhadhini swala wala Mteka maji msikitini kwa kukosa Imani na Kampuni ya Acacia.

Wanahisa Ni wakati wa Kuwawajibisha viongozi wa juu wa Kampuni yenu kwa Kufanya Ujinga kwa miaka Mingi.
 
Napenda kuuliza, hivi wanaochejua ni ACACIA tu hapa nchini? nikiwa na maana migodi mingine haichejui maana sijasikia kashkash kwa migodi mingine, au ndo step at a time. Kama vipi serikali iyanunue hayo makontena kwa bei laghai ya ACACIA then wakayauze tupige mpunga huku wakiwaburuza mahakamani. Am i dreaming?
 
5-Stars-Colonization.png
Magufuli kashtuka.
 
Hivi mbona katika hili ni ACACIA tu ndo wanasikika sana, kulikoni hapa?
 
Hizi ndizo habari ambazo watu flani wanapenda. Ni kusikia fulani kafilisika, fulani nyumba yake inapigwa mnada, fulani kafunga biashara.
Haswaa ndio zimewatawala watu fulan haswa kipindi hiki. Ukiwa tu tajiri ni kosa... watakuandama kwelikweli
 
Hizi ndizo habari ambazo watu flani wanapenda. Ni kusikia fulani kafilisika, fulani nyumba yake inapigwa mnada, fulani kafunga biashara.
Mkuu Mbona Comment yako ya Kijinga sana nakushauri ifute haina haja ya wewe kuchangia.
 
Back
Top Bottom