Hisa Pepe: Je ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hisa Pepe: Je ni nini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mzozo wa Mizozo, Mar 2, 2009.

 1. Mzozo wa Mizozo

  Mzozo wa Mizozo JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 427
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nahitaji kujua zaidi husiana na hawa jamaa wa hisa pepe.. Ni kwamba tangu wameweka website yao hewani na kujitangaza kwa bidii zote huku wakihamasisha watanzania kujiunga kwa wingi ili waweze jipatia kipato kidogo kwa kusoma matangazo na mengineyo hakuna lolote la maana ambalo waweza sema limefanyika katika tovuti hiyo na ni mwezi wa nne sasa.

  Swali ambalo nataka kupatiwa ufahamu wake hapa ni je hawa waheshimiwa walikuwa wanaingia katika hii 'undertaking' wakiwa wanafanya kwa majaribio ama walitaka kuwapotezea muda waTZ? Na je kama imewashinda kwa nini wasikubali matokeo, kuifunga na kuendelea na mengine?

  Salaam.

   
  Last edited: Mar 2, 2009
 2. apakati

  apakati Member

  #2
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi pia nimejiunga na niliwauliza juzijuzi hapa kupitia kituo chao cha huduma kwa mteja...na swali langu lilikuwa hivi
  "Tutegemee lini kufaidika na je ninaweza kupata Tsh Ngapi kwa siku. Mbali na matangazo kuna huduma gani tena au ndio hayo tu?" Nilijibiwa, kwa vile sikuambiwa kama jibu ni siri naona ni haki kushea nawe
  Jibu:
  Ahsante apakatie, mzee wewe nii yule wa chembe ama wa kidevu? Ni kweli ukimya unaonekana, ni rahisi kuuzima ukimya kwa kutuma email kwa wanachama wote, ila kuuzima ukimywa kwa namna hii ni porojo, hakuna anayepende kuwa pleased na maneno ya email, hata mimi sipendi, napenda actions.
  Hisapepe inavyofanya kazi ni kwamba lazima kuwe na watangazaji watakaotoa matangazo na waendesha takwimu au tafiti/dodoso (surveys/questionnaires), matangazo hayatoki kwetu, ila ni jukumu letu kutafuta watangazaji.

  Kwanini kimya? Watangazaji wengi tu wameipenda sana idea na wapo tayari, tuna list ndefu kwa vile bei zetu ndogo, fikiria tangazo la elfu3, elfu10 yani rahisi sana, tatizo ni idadi ndogo ya wanachama, ndo kwanza 400++ kwahiyo wengi wanasema tuzidishe bidii kuongeza wanachama, fikiria giant kama tigo (hatujaongea nao bado) ila kumfuata kwa tangazo la kutuma kwa watu mia4 bado atakushangaa.

  Nini haswa kinafanya idadi ikawa hivyo? Tunashukuru sana wanachama wanaalikana ila mialiko mingi huwa wanaweka maneno matamu na hivyo ujumbe unakwenda spam folder, wabongo wengi tumechunguza wanauliza sana mbona sijapata email tunawajibu angalia spam folder na kweli wanaikuta, kwaio wengi hawana time na spam folder mwaliko wako ukinasa huko basi umeupoteza, najua unajua spam huangalia lugha haswa unapomwambia mtu atapata pesa ama kulipwa, mialiko ya kiswahili walau inapita.
  Kingine ni marketing yetu, haijafanyika zaidi ya blog posts na hiyo mialiko.

  Plan yetu kwa miezi mitatu ya kwanza ni kutotangaza bali kuacha nguvu ya mialiko ya mwanachama kwa mwanachama, ndio maana tukatenga fungu kwa wanaoalika, kisha kinachofuatia sasa ni sisi kutangaza kwa njia nyingine, tumeshaona mialiko pekee haitoshi, sasa tunaingia ground, street kwa street na tutajizatiti.
  Na hii tumeipania wiki ya kwanza ya April hii

  Mwisho wa siku tunaamini sana idea ni nzuri, kwa kweli mtu hana sababu ya msingi kutojiunga na www.hisapepe.com , maana haimgharimu chochote na unaweza kujiunga anonymously ila pia kukiwa kimya panaboa lazima tujitangaze.

  Matangazo yakianza pia usitegemee lazima upate wewe, unaweza kuwa umekaa na mwenzako yeye akapata wewe ukakosa, inategemea kama tangazo ni aina yake, kumbuka ulipojiunga ulichagua haya, na yeye akachagua yale. Kwahiyo basi hata pesa mtapishana, wewe unaweza kujikuta una elfu mbili mwenzako ana elfu ishirini kwa vile tu surveys alizopokea zilikuwa zinalenga criteria zake, kwahiyo kiasi halisi hutegemea na matangazo/surveys/revies ngapi zimekulenga.

  Jiamini, ni kitu kipya, lazima kianze kwa taratiibu na badae ni spree!

  Unaweza pia kuendelea na www.wapi.co.tz ni tovuti yetu pia! karibu pia kwa mambo mengine kama domain names, hosting na website designing, bei zetu poa, buku 80/= tu kwa mwaka na unakuwa hewani daima!"
  Mwisho wa kunukuu
  Nimeamini jibu lao na kwa vile hainikosti kitu kuwa mwanachama nimekaa nasikilizia, binafsi nina tsh 1670/= kama salio langu, hii nimeipata kwa kualika na kuchat, ukichat unajipatia nadhani ni tsh 20 kama sijakosea, so who knows, may be wana mpango mzuri but I can not guarantee.
  ...yours kitaifa zaidi
  Apakati!
   
 3. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Ni utapeli wa hali ya juu. Nashangaa website nyingine wamekubali kuungana na hawa wahuni. Asante JF kwamba hamjaingia mkenge. Jamaa wanachofanya ni usanii tu. Mimi namjua mtu behind this, nitawapa baadhi ya emails alizowahi kunitumia na wizi wake.

  Ni opportunist mzuri sana ukimsikiliza na kuingia kwenye mtego simpo sana. Webmasters ndiyo target yake kubwa.
   
 4. apakati

  apakati Member

  #4
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Love Pimbi maoni ni kitu kizuri na hoja ni nzuri zaidi ya maoni, kwa bahati nzuri nimeshiriki sana get paid to do something nyingi ktk internet, huu mwaka wangu wa nne nadhani, ningefurahi kujua kinagaubaga namna gani naweza kutapeliwa na hisapepe.
  Kwa mfano zaidi ni kwamba nimejiunga na username ya apakati, jina la kwanza beka lapili miki (yote si majina yangu) p. o .box nimeweka 123 anuani nimeandika kijijitz, namba ya simu nimeweka kisha nimejiunga. Anzia hapo unielekeze naweza kutapelika vipi ili nijitoe.

  Kuhusu kuwatarget webmasters sijaelewa pia maana mi sina hata blogu ila nipo ktk websites/forums kama 45 hivi dunia nzima. Ntashukuru sana mchango wako mwana nisije nikajikuta nimelia, katika niliowaalika wakajiunga mmoja ni webmaster ningependa nimwokoe!
  Kuhusu nani owner mi nilichunguza kwanza, hii hisapepe walianza kutambia mwaka jana kule Wapi! - Mkono Kwa Mkono! kisha wakaifungua (hata wapi utaona kuna banner yao maana wapi ni yao pia, kisha wakafungua, so owner wake ni owner wa wapi, ila kama yeye anatumika kama kibaraka kuna owner behind this inapendeza tukijua ukweli toka.

  Nashukuru nasubiria maana walianza februari leo march, mwezi wa pili unakata huo usikute tarehe ya kuumizwa bado
  Wako Kitaifa Zaidi
  Apakati!
   
Loading...