Hired to be fired: Andre Villas-Boas Sacked by Tottenham Hotspur!

kichwat

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
1,819
587
Kocha wa Tottenham Andre Villas Boas (AVB) amepigwa panga kufuatia matokeo mabaya na mwenendo usioridhisha wa Tottenham. Kipigo cha bao 5-0 nyumbani ni kibaya zaidi katika kipindi cha miaka 16 iliyopita, na kimekuja wiki 3 tu tangu walipochapwa bao 6-0 na ManCity.

Kupigwa panga kwa AVB huenda kukawapa nguvu mashabiki wa Manchester United ambao tayari wameshakata tamaa na kocha wao aliyeonesha kupwaya - David Moyes.
 
uongozi klabu umechukua uamuzi huo kufuatia kipigo cha bao 5-0 dhidi ya Liverpool jana, ikiwa ni wiki tatu tu tangu wapigwe bao 6-0 dhidi ya ManCity tarehe 24/11/2013.
 
Andreas Villas Boas (AVB) amepigwa panga kufuatia matokeo mabaya ndani ya Tottenham

Tottenham dismiss manager Andre Villas-Boas in the wake of the club's 5-0 thrashing by Liverpool-BBC Sports,premier league
 
David Moyes anahitaji vipigo viwili tu naye arudi home.
 
Hatoki yule pale ndo kwanza anapewa fungu la usajili january hii, manchester utd si kama hivyo vitimu vidogo vidogo vibavyotaka umaarufu sasa. Ana mkataba wa miaka sita na ataumaliza tu!
 
Jana nilimuona mwenyekiti wa Spurs Bw Daniel Levy akisikitika wakati wa mechi nikajua tu safari ya AVB imekwiva,the managers are hired to be fired.
 
David Moyes anahitaji vipigo viwili tu naye arudi home.

Kuna tofauti kubwa case ya AVB na Moyes.Moyes ndio kapewa timu while AVB alikuwa katika msimu wake wa pili
AVB ametumia €107 mil kwenye usajili while Moyes ametumia €27 mil
 
DICANIOgoal_2929631.jpg

article-2308074-194926E6000005DC-361_634x501.jpg


article-2308074-1949539C000005DC-351_634x501.jpg
 
mou nae anaweza kufuata siku sio nyingi. sioni uzuri wa huyu mzee zaidi ya kuuwa viwango vya baadhi ya wachezaji tu.

nakubaliana na wewe,mzee anapoteza talanta za vijana,mtu kama zaha ktk timu ya vijna anacheza vizuri na kuipa ushindi timu yake ya under 21,lakini huku ktk timu ya wakubwa anampa dakika 3 hadi 5 za kucheza.
lakini pia mzee hadi sasa bado hajui ipi ni timu yake ya kwanza,kila siku bado anajaribu timu.
 
nakubaliana na wewe,mzee anapoteza talanta za vijana,mtu kama zaha ktk timu ya vijna anacheza vizuri na kuipa ushindi timu yake ya under 21,lakini huku ktk timu ya wakubwa anampa dakika 3 hadi 5 za kucheza.
lakini pia mzee hadi sasa bado hajui ipi ni timu yake ya kwanza,kila siku bado anajaribu timu.

Jose is next!
 
Moyes ana full backing ya Fergie, watampa angalau miaka 3 ya kujiuliza. Kuna tofauti kubwa kati Manchester United, Arsenal na vitimu kama Spurs. Managements za timu hizi zimeshajifunza mengi juu ya kuwapa makocha muda wa kujenga consistences na timu ya nzuri haijengwi kama uyoga. Pia viongozi wa timu kama Arsenal na Utd wanafahamu kuwa mafanikio ya timu si lazima yawepatikane uwanjani tu sio kama timu nyingine.
 
Back
Top Bottom