hippocratessocrates & JF DOCTORS NISAIDIENI HILI JAMANI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hippocratessocrates & JF DOCTORS NISAIDIENI HILI JAMANI

Discussion in 'JF Doctor' started by Nivea, Oct 11, 2012.

 1. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Naamini ushauri wenu kwa asilimia 100%maana ulishanisaidia several times :
  nina mdogo wangu wa kike ana miaka 22 ,anasumbuliwa na tatizo ambalo kwa kweli tumemtibu na tumeshindwa kuelewa ninini hasa
  akiwa kwenye mkusanyiko wa watu kwenye daladala sokoni stendi huwaanaishiwa nguvu nakuanguka na kupoteza hata fahamu,huwa inaanza na kichwa kuuma sana then hiyo hali inatokea,akiwa katika hiyo hali kichwa huuma sana,jasho jingi,macho pia anakuwa haonikabisa,na hii hitokea within 5min na anakuwa mzima kabisa anaendelea na safari mimi nilishuhudia siku moja nilienda nae sokoni kule karume then alianza kusema anajisikia vibaya tukasimama alilegea akaanguka niwale wauza viatu waliniaidia.imekuwa tena jana alianguak huko mwanza sokoni bahatai nzuri alikuwa na rafiki yake,hawezi kutembea mwenyewe kwani anaogopa sana.
  tulimeleka hospitaliakapata vipimo
  1.moyo
  2.pressure
  3.wingi wa damu
  4.macho ni mgonjwa na anatumia miwani
  Vipimo vyote ni null

  NAOMBA USHAURI WENU JAMANI TATIZO HILO LINAMTESA SANA,NISAIDIENI HATA KUULIZA WATU WENGIME MNIPE USHAURI AFANYAJE
  mkuu hippocratessocrates MziziMkavu na wengine wote nawategemea sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu nivea,..POLE,

  Ni vyema kujua,
  -Tatizo lilianza lini?..yaani lina muda gani sasa,
  -Tatizo hili hutokea kwa frequency gani(how often), interms of wik, mwezi n.k?
  -Je, anatumia dawa zozote za muda mrefu?
  -Je, katika kuzaliwa kwake na ukuaji wake alipata tatizo kama hili?
  -Je, katika familia(upande wa baba+mama mzazi) kuna ndugu mwenye/aliyekuwa na tatizo kama hilo au ugonjwa wa kifafa?


  Tatizo likitokea/linapotokea:
  -Je, tatizo unasema hutokea akiwa mbele ya watu(public) TU?
  -Macho yake huangalia wapi,
  -Je,hutoka povu mdomoni, meno huwaje?
  -Je, hupata haja(ndogo/kubwa) likitokea?
  -Je, mwili hukakamaa /kuishiwa nguvu?
  -Huwa ana kumbukumbu ya jambo/mambo yaliyotokea?
   
 3. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  -tatizo lilianza huu ni mwaka wa pili yaani mwaka jana
  tatizo hilo hutokea akiwa kwenye public tu na sio mwoga wa watu,anaweza akawa public ikatokea au isitokee na imwsababisha hata lecture room akae mbele kabisa au nyuma kabisa na sio katikati ya watu
  -hajatumia dawa zozote zile baada yakutoona tatizo
  -huyu mtoto hajawahi pata tatizo lolote kiafya ni hili tu kitu ambacho huwa kinamsumbua sana ni tumbo la hedhi ambalo anaumwa sana na sio kawaida
  -kwetu hatuna tatizo la kifafa kabisa kwa upande zote mbili
  -macho huwa kawaida ,hakakamai,wala hapati haja na hatokwi mapovu anakuwa amelegea tu jasho jingi na kuishiwa nguvu ukimpa maji anapata ahueni haraka
  -kuhusu kumbukumbu anakuwa anakumbuka na huwa anaelewa kinachoendelea kabisasema ndio hana nguvu kabisa.
  nahitaji msaada wenu wakuu

  hippocratessocrates
   
 4. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mnatakiwa kumuona mtaalamu wa magonjwa ya ubongo (huku wanaita magonjwa ya akili), pamoja na atakayowashauri msiache kufanya kipimo kinaitwaa EEG au kingine cha kisasa zaidi. Kipimo hicho kitaweza kuwapa muenendo wa utendaji wa ubongo. PILI na kubwa zaidi ni kwenda kwa maombezi kwa wachungaji "wanaomuamini Yesu Kristo anayeponya magonjwa yote", watamuombea kwa jina la Kristo Yesunaye atapona kabisa.
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu nivea,
  -anasoma shule gani, kutwa/bweni?
  -akidondoka hudondokea sehemu gani?
  -unatambuaje/unajuaje kuwa haoni?


  Sina uhakika kama ni medical case per se, sounds psychological bse it can be "attention seeking" hasa kwa kina dada, watu wenue umri chini ya miaka 25, n.k...lakini ni vizuri, kufika hospitali yeyote kum-review na kufanya vipimo esp. EEG.
   
 6. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,873
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  Tatizo kama hilo mimi nilikuwa nalo na liliisha mnamo mwaka 2006 nikiwa form 4; binafsi nilikuwa msaidizi wa padre altaren na hapo altaren lilinitokea mara tatu:
  na mara nyingine pia ilinitokea kwenye mikusanyiko mikubwa kama nikutano ambay mara zote sehemu hizo niwe sina mahala pa kuketi hivyo kulazimika kusimama na nilichokuja kugundua kwanini ilikuwa natokewa na hali hiyo ni kuyokana na kuwa na upungufu wa MAJI MWILINI kwani nilikuwa ni mvivu sana wa kunywa maji; pili kuwa na NJAA hii pia ilisababsha kupatwa na hali hiyo:

  kifupi hali hiyo haijawahi kunitokea nikiwa nmeshba vzr au nmekunywa maji ya kutosha .. Baada ya kugundua hilo; nikachukua hatua stahiki na hadi leo hii nmemalza chuo kikuu cjawahi kutokewa na hali hiyo.

  Ushauri azingatie kula vizuri na kunywa maji ya kutosha
   
 7. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  -anasoma SAUT
  -anadondoka popote ndio sababu nikakuambia alidondoka kule karume kwenye wauza viatu
  kuhusu kuona yeye mwenyewe anasema kwa sababu hapotezi ufahamu!ila ni nguvu zinamwishia kabisa
   
 8. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  asante sana mkuu je ilikuwa ni same same kama nilivyoelezea?
   
 9. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Nadhani umeona hapo kwenye RED nilipo-undeline na ku-bold. Nafikiri huwa inamtokea hivyo katika public places kwakuwa anakuwa ametembea muda mrefu juani na yeye hana maji mwilini mwake ndiyo sababu inamtokea kirahisi akiwa maeneo ya watu wengi kwani anakuwa tayari amezunguka masaa kadhaa. Bonyeza link hii: Jitibu kwa kutumia maji | maajabuyamaji.net,

  H
  apo utajifunza namna ya kuyatumia MAJI kujitibu na hilo tatizo la kuanguka na hatimaye baadaye hata macho yatapona ataacha kutumia miwani kabisa maisha yake yote yaliyobaki.
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  asante sana mkuu mungu akubariki bado nasubiri more ushauri wenu wakuu
   
 12. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sina uhakika kama, Bugando Medical Centre (BMC) wanafanya EEG, lakini ni vizuri kufika na kufanya kipimo hicho,
  -Daktari pia ataangalia kama kuna shida yeyote katika moyo(ingawa mlishaangalia mwanzoni)
  -Na kuelezea shida uliyosema mwanzoni tumbo wakati wa hedhi..hasa kama anahisi ongezeko la damu tofauti na ilivyokuwa mwanzoni.
   
 13. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  imekuwa ni tabu sana kwake dr.hilo tumbo linamuuma sana kabla hata wiki mbili na damu haitoki na ikifika siku zake za hedhi inatoka tu kidogo na kuendelea kumuuma hata wiki mbili zaidi ,hii mara ya mwisho juzi aliumwa mpaka akalazwa hospitalini na akachomwa sindano za masaa ,yaani namwonea huruma sana hivi dr.kwa hili afanyaje?nataka nimpigie simu nimwelekeze aende pale bugando afanye hicho kipimo au aje dsm mara moja .it is terrible,mimi pia nilikuwa naumwa sana sana tumbo mpaka nazimia nilijaribu kwenda hospitali wapi sikupata ahueni na mimi huwa sipendi kumeza dawa yyte,kila nilipokwenda wananiambia nikizaa litaacha kweli nikazaa likaacha kabisa mpaka leo du ila ni tabu sana.amekuwa mzigo mpaka kwa marafiki
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Mkuu nivea ninafikiri Wamekutosha sana kukuuliza maswali Wakuu wenzangu pamoja na Mkuu Dr.@hippocratessocrates na wewe kuyajibu ila ninacho kuomba kwanza kamalize vipimo vyote vya Ma Hospitalini na utumie Dawa zote za hospitali ikiwa bado ndugu yako hajapona njoo tena hapa uje utupe Feeedback mimi nitajaribu kukupa Dawa zangu za Tiba Mbadala Mitishamba inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu ndugu yako atapona...
   
 15. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  asante mkuu mzizi mkavu nitashukuru kwa ushauri wako na tiba yako
   
Loading...