HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,303
105,103
Najua wengi ni mashabiki wa wasanii fulani fulani wa mziki pendwa wa hip hop ila leo nataka tuangazie kidogo hawa ma underground hip hop.

Katika tansina ya muziki huu wa hip hop tunaona jinsi gani evolution ilivyobadili ladha ya mziki huu kiasi cha wasanii kuimba nyimbo ambazo hazina lyrical wala critical.

List yangu ni hii hapa na wewe unaweza kuweka yako.

1. Dizasta vina
2. Nala mzalendo
3. Kadgo
4. Boshoo ninja
5. Kinya mistari
6. Shaolin senetor
7. Mbeya boy chuma
8. Hamis mistari
9. Ado gado
10. Nyenza MC

Wapo wengi ila kwasasa nianze na hao halafu chini nitanukuu mistari yao katika baadhi ya nyimbo zao
 
Dizasta vina

Alifika alikaza na kamba, aliweka mizizi ya kukata na panga.../

Alichizika utasema mwehu, moyoni aliacha alama ka ronaldo alivyoacha alama bernabeu.../

Nilikua siufahamu ugoni, kama kufumaniwa ni dhambi na nitapata adhabu motoni,,,,nitaenda na tabasamu usoni.../

Labda wakati ni sasa nimerudi kuenzi nafasi, napenda uhakika silengi bahati.../

Naomba ujue kua mkeo hakupendi kwa dhati, kumlazimisha ni kumuenzi hayati.../

Sasa kwanini usinipige na ulivyojifungia misuli, nivunje mbavu zangu labda utajisikia vizuri.../

Fanya maamuzi sasa maana najitia kiburi, niue leo walimwengu watafukia kaburi.../

Song: kikaoni
 
Nikki Mbishi ni lyricist mkali kwa underground.

“Nipo kwenye mainstream ya underground, Mbishi napanda dau kila round”.
 
Ntendo Boy

Visit YouTube Kuna kipande cha Konekisheni bado ya MOTO

Typed Using KIDOLE
 
Nala mzalendo (diego naladona)

Asubuhi na mapema, nashukuru kwa kila kitu ikifika usiku pakuche tena.../

Niwe mwaminifu niwe mwema, niwe mkamilifu nizidi kumsifu anayenipa neema.../

Nacheka kuanzia asubuhi, utadhani sijui kwamba nala ninaishi na maadui.../

Nimetekwa na roho safi, na ndio maana natengwa na waroho wa nafsi.../

Namuuliza mama mimi nilizaliwa wapi, ananijibu jiji flani la harakati.../

Namuuliza au ni kule kwa gadafi, ananambia kilombelo ila kwenye kizahanati.../

Nilishazaa wanangu wakiume wawili wakike wawili, alifariki kaka yako nikakuzaa wewe ili uzibe pengo hili.../

Hivyo mamako nikawa sina budi, nikakuzaa wewe nikakupa jina na nikakuita sudi.../

Na shule nikafunzwa baba na mama ndio wazazi, nikamuambia mama sijawahi kumuona baba akanambia amesafiri kikazi.../

Niliishi kwa kufurahia sikuwahi kuonesha kiburi, nikashangaa nimekua mkubwa nikaoneshwa kaburi.../

Song: Uhalisia
 
Kadgo

Nimezaliwa naye tumbo moja namuita pacha, mama ananiambia kanizidi dakika tu sio mwaka.../

Yupo hai hajafa hivi navyoongea, amenihasa amenifunza haswa nisije potea.../

Ni identical twins, two kings same blood same color same height and two beings.../

Sasa niende home alipotoka baba, na mama mzazi pia ndio root ya grandfather.../

Kwa raha ndugu yake upendo ndani ya familia, maisha kuongeza mwendo mienendo ikaanza tabia.../

Kufungua ukurasa madarasa yakafuatia, ikafika muda wa kuachana na pacha ambaye namuaminia.../

Siku moja niko stand nasaka mlungula, kosa jinsi niliyovaa nikavishwa misala ya kulwa.../

Kipigo cha mbwa mwitu nikashtuka siku kadhaa, siku muwekea bifu moyoni sikutaka balaa.../

Siku zikapita ikafika siku ya mnada, sokoni napita pembeni yuko siter na father.../

Ghafla mbele yangu akatokea pedeshee, mwenye visanga na kulwa na hakutaka nijitetee.../

Akaanzisha ugomvi mbele ya umati father akaingilia, bwashee si akaitoa risasi dingi akaitoka dunia.../

Kwa macho nikishuhudia najuta kufafana, najua dunia ni njia kulwa acha unachofanya.../

Song: pacha
 
Boshoo ninja

Kila nikifanya wanahanya sio siri, nikichana yanapanda maruani nadhikiri.../

Natumia akili bingwa in dar, wanashangaa ni underground ila na hang ki star.../

Nikiwa bar mi ndo boss uyu mupe yule muluke, nyie matozi mmepandisha bei ndala nyeupe?...?

Eti bongo bahati mbaya halafu unavaa unapendeza, bongo kama ulaya tu uchawi uwe na fedha.../

Skiza nacheza na lugha, ntakutoa udhu wewe usicheze na mbwa.../

Unashangaa nini ndani bikini nje juba, au unashangaa kuona sheria inapindishwa na fuba.../

Fata hii acha ile ni upuuzi uliotukuka, sio bongo ya zaire usi mix na kapuka.../

Shtuka nakupa ujanja chukua kama hujaipata, we kilaza mkono wenye shombo haufukuzi paka.../

Wanaishi na chuki zao ila hawazioneshi, kama wakike kasoro maziwa hawanyonyeshi.../

Song: michano
 
Kinya mistari

Huendi ibada sababu ya uchovu wa nafsi mema umeweka maktaba, maouvu umeyafungulia kurasa.../

Imani haba kwa waganga unatinga, upembe na usinga unarudi unaringa.../

Wakati haujaenda haujaenda ulipoitwa sababu, zakutokwenda unadai kwamba utapitwa ni ajabu

unapuuza sheria za muumba ooh, mgumba usiamini ndumba yesu anakuita njoo.../

Njoo kwenye mwanga achana na giza, njoo ule baraka huu so muda wa baga na piza.../

njoo hizo hanasa na laga zitakuumiza, njoo binadamu hawana maana watakuliza.../

Malengo ya shetani kwa binadamu, ni kuingia nawe jehanamu na anahamu ndo maana kamtegesha chambo mtamu/

Shetani Anakusaka jinsi unavyosaka cash, njoo upesi anakuita bwana wa majeshi.../

Usije ukajilaumu, sauti ukiisikia usifanye moyo kua mgumu.../

Unahangaikia mambo ya dunia unajisahau unachelewa, angaikia ufalme wa mungu na ziada utapewa.../

Song: Njoo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom