Hip hop Facts Thread

GadoTz

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
350
566
latest



Album bora ya hiphop ya muda wote ni ipi?

Msanii bora wa hiphop wa muda wote ni nani?

Wimbo bora wa hiphop wa muda wote?

History ya hiphop

Records za hiphop

Tafsri ya hiphop na utamaduni wa hiphop kwa ujumla.


Karibu kwa mjadala!
 
Kwanini uamini Billboard?
Wewe unaamini hiyo list imekamilika?
Kwanini infuential rapper kama 2PAC hawajamweka?
Kwanza hiyo list inaonekana ipo biased sana.
Nilitegemea mtu kama 2pac awepo,nilitegemea NWA wawepo.
Kwa sababu mimi ninaamini kuwa mc mkali lazima uwe CHANGE AGENT. Sasa kwa mtu kama Kendric Lamar ambaye hana hata miaka 5 kwenye peak ya muziki huu unakuja kusema ni mc mkali?
Sikatai kuwa Kendric ni mkali lakini hiyo ya kusema mcs wakali kuwahi kutokea duniani.
 
Album bora za hiphop za muda wote.

1. Ilmatic - Nas

2. The Marshall Mathers LP - Eminem

3. All Eyez on Me - Tupac

4. Ready to Die -Notorious B.I.G.

5. The Chronic - Dr. Dre

6. Reasonable Doubt -Jay-Z

7. Straight Outta Compton - N.W.A

8. The Eminem Show - Eminem

9. Get Rich or Die Tryin - 50 Cent

10. Paid in full - Eric B & Rakim

Hii ni according ya research yangu binafsi
 
[QUOTE"NEW NOEL, post: 15268215, member: 44297"]Kwanini uamini Billboard?
Wewe unaamini hiyo list imekamilika?
Kwanini infuential rapper kama 2PAC hawajamweka?
Kwanza hiyo list inaonekana ipo biased sana.
Nilitegemea mtu kama 2pac awepo,nilitegemea NWA wawepo.
Kwa sababu mimi ninaamini kuwa mc mkali lazima uwe CHANGE AGENT. Sasa kwa mtu kama Kendric Lamar ambaye hana hata miaka 5 kwenye peak ya muziki huu unakuja kusema ni mc mkali?
Sikatai kuwa Kendric ni mkali lakini hiyo ya kusema mcs wakali kuwahi kutokea duniani.[/QUOTE]


Billboard ni source makini ukitaka kupresent data za music, na hakika wamefanya research kabla ya kuja na hiyo list man.
 
VH 1 wametoa nyimbo 20 za muda wote za hiphop kama ifuatavyo.


20 Kanye West ft/ Jamie Foxx – “Gold Digger”
19 Ice T – “Colors”
18 50 Cent – “In Da Club”
17 Sir Mix-A-Lot – “Baby Got Back”
16 Missy Elliott – “Get Ur Freak On”
15 Eminem – “Stan”
14 Tupac – “I Get Around”
13 Wu-Tang Clan – “C.R.E.A.M.”
12 L.L. Cool J – “I Can’t Live Without My Radio”
11 Jay-Z – “Hard Knock Life”
10 Kurtis Blow – “The Breaks”
09 Salt-N-Pepa – “Push It”
08 Snoop Doggy Dogg – “Gin and Juice”
07 Notorious B.I.G. – “Juicy”
06 N.W.A. – “Straight Outta Compton”
05 Grandmaster Flash & the Furious Five – “The
Message”
04 Run-DMC ft/ Aerosmith – “Walk This Way”
03 Dr. Dre – “Nuthin But A ‘G’ Thang”
02 Sugarhill Gang – “Rapper’s Delight”
01 Public Enemy – “Fight The Power”
 
[QUOTE"NEW NOEL, post: 15268215, member: 44297"]Kwanini uamini Billboard?
Wewe unaamini hiyo list imekamilika?
Kwanini infuential rapper kama 2PAC hawajamweka?
Kwanza hiyo list inaonekana ipo biased sana.
Nilitegemea mtu kama 2pac awepo,nilitegemea NWA wawepo.
Kwa sababu mimi ninaamini kuwa mc mkali lazima uwe CHANGE AGENT. Sasa kwa mtu kama Kendric Lamar ambaye hana hata miaka 5 kwenye peak ya muziki huu unakuja kusema ni mc mkali?
Sikatai kuwa Kendric ni mkali lakini hiyo ya kusema mcs wakali kuwahi kutokea duniani.


Billboard ni source makini ukitaka kupresent data za music, na hakika wamefanya research kabla ya kuja na hiyo list man.[/QUOTE]
Billboard wamekurupuka and what do those white folks know bout hip hop....
 
MAANA YA HIP HOP

Mahali ilipozaliwa?

Julai 23 mwaka 2007, Jiji la New York, lilitangaza rasmi kuitambua 1520 sedgwick Ave iliyoko Bronx kuwa sehemu ambayo hip hop ilizaliwa. “1520 sedgwick Avenue ni sehemu ambayo Recreation Room, chumba alichokitumia muasisi wa hip hop, Dj Cool Herc. Taarifa ilisema “ingawa kwa sasa (wakati huo mwaka 2007) umefungwa kwa marekebisho tangu mwaka uliopita, tunawataka wana hip hop na wawezeshaji wengine kutoa zabuni ya kupata uendeshaji wa sehemu hii. Leo hii waratibu watafanya mkutano wa waandishi wa habari katika eneo la kihistoria kutangaza kuwa Jimbo la New York kupitia ofisi ya kuhifadhi makumbusho na utunzaji wa historia wameyakubali maombi yaliyotumwa Julai 2 kuitambua rasmi sehemu hii”.
 
Dj Kool Herc

Ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa Hip Hop anasema “sehemu nilipoanza kupiga muziki ilikuwa ni 1520 Sedgwick Avenue, katika recreation room, chumba kilichokuwepo katika jengo lilipokuwa pango langu, watu walikuja kucheza muziki kutoka maeneo jirani”

Krs One

Anasema “.mwaka 1973, nilikuwa Bronx, katika hii sehemu iliyoitwa 1520 sedgwick Ave, hii ndiyo sehemu ambayo hip hop ilipozaliwa. Mtu anayeitwa Cool Dj Herc alikuwa akifanya maenesho..”

Tarehe ya kuzaliwa

August 11, 1973, ndiyo tarehe ambayo hip hop ilizaliwa kwa mujibu wa Cindy Campbell ambaye ni dada yake na Dj Kool Herc. Onesho la kwanza la hip hop lilifanyika siku hiyo. Onesho hilo liliandaliwa na Dj Kool Herc kwa lengo la kuchangisha pesa ili dada yake (Cindy Campbell) aweze kurudi shule (back to school party). Herc alikodisha recreation room kwa dola ishirini na tano za kimarekani na kiingilio ilikuwa ni thumni (cent) 25 kwa wanawake na thumni 50 kwa wanaume. Herc alikuwa kwenye mashine na msema chochote (mc) wa siku hiyo alikuwa ni dada yake (cindy), tukio hili ndilo linalomfanya cindy Campbell kuwa mwanamke wa kwanza katika hip hop (first lady of hip hop).
 
Charlie Ahearn

Ni mtu ambaye aliyeandaa filamu ya Hip Hop iitwayo “Wild Style” kuanzia mwaka 1980 mpaka 1982 ilipotoka. Anasema “August 11, 1973 imeibadilisha dunia, tunatakiwa kusherekea ubunifu na maajabu ya usiku huo”

Licha ya tarehe hiyo Universal Zulu Nation kupitia tovuti yao wanaitambua tarehe 12 Nov 1973 kama tarehe rasmi ya kuzaliwa hip hop na pia mwezi November kama mwezi rasmi wa hip hop. Wanasema “ kwa kuzingatia tarehe tajwa hakuna kitakachokuwa na umuhimu kama kusherehekea utamaduni wa hip hop na historia yake katika mwezi novemba, hakika ndiyo kitu kilichotufanya Universal Zulu Nation tuwepo kwa zaidi ya miaka ishirini na saba (kwa wakati huo)”
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom