Hints za January Makamba kuhusu mafuta na Gesi Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Contents za Mh. Waziri Makamba

1. Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia nchini ulianza mwanzoni mwa miaka ya 1950. Mafanikio makubwa yalipatikana yakiwemo ugunduzi wa gesi asilia katika kisiwa cha Songo Songo mwaka 1974 na Mnazi Bay mwaka 1982. Aidha, Katika miaka ya 2010 na 2012 utafiti uliendelea katika maeneo ya kina kirefu cha Bahari ya Hindi. Hadi kufikia mwezi Mei 2022, jumla ya Futi za Ujazo Trilioni (TCF) 57.54 za gesi asilia ziligunduliwa katika maeneo ya nchi kavu na kina kirefu cha bahari. Kati ya kiasi hicho Futi za Ujazo Trilioni 47.13 zimegundulika katika Vitalu vilivyopo katika kina kirefu cha bahari ya Hindi, na Futi za Ujazo Trilioni 10.41 zimegundulika kutoka maeneo ya nchi kavu.

2. kutokana na ugunduzi huo wa kiasi kingi cha gesi asilia, Serikali ilifanya maamuzi ya uanzishwaji wa Mradi wa Kusindika na Kuchakata Gesi Asilia (Liquefied Natural Gas -LNG) kama njia bora ya kuendeleza rasilimali hiyo kwa ajili ya kuuzwa katika masoko ya Kimataifa na sehemu nyingine ya gesi hiyo kutengwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi

3. Serikali kupitia TPDC itashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huu. Ushiriki, katika ubia na ushirika wa uendeshaji wa mradi, utasaidia kujenga uwezo wa Shirika hili ili miaka ijayo liweze kufanya shughuli hizi lenyewe na kwa tija na ufanisi kwa manufaa makubwa zaidi kwa taifa. Safari ya kuisuka upya TPDC kama Shirika mahiri na la kimkakati imeanza kwa wewe kutupatia Mwenyekiti wa Bodi mzito na sisi tumeunda Bodi mpya yenye kutoa mwelekeo wa dira mpya tunayoitaka kwa TPDC.

4. Manufaa yatakayopatikana katika utekelezaji wa mradi huu ni pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi; kujenga uzoefu wa TPDC kupitia ushiriki wake; kuongeza mapato ya Serikali yatakayotokana na mauzo ya gesi; upatikanaji wa gesi asilia iliyochakatwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi; ushiriki wa watanzania katika uuzaji wa bidhaa na utoaji huduma; na fursa nyingi za ajira kwa watanzania hususan katika kipindi cha ujenzi na hata katika kipindi cha uendeshaji wa mradi.

5. pia tumefanya uamuzi wa kuanzisha Eneo Maalum la Kiuchumi (Special Economic Zone) kwenye eneo la mradi ambapo kutakuwa na vivutio mbalimbali, ikiwemo bei nafuu ya umeme, ili kuvutia viwanda na shughuli za kiuchumi katika mikoa ya Kusini.
 
Hii gesi asili nmeona inawekwe kwenye mitungi na kufungwa kwenye magari kama nishati mbadala wa petroli,kwa ufahamu wangu mdogo niliju gesi asili sio raisi kuwekwe kwenye mitungi ndio maana yanatumka mabomba kwa ajili kuisambaza kwa wahitaji,kama hilo limewezekana kwenye magari ni kwa nini isijziwe kwenye mitungi kwa ajili ya matumizi ya majumbani?
 
Katika ku summarise speech ya kiazi yule umeacha hoja ya msingi kwenye maeneo ya majadiliano.

Anadai wanatumia consultant kwenye key four areas kwa ushauri;
Kifedha (commercial)
Biashara (economic)
Kiufundi (technical)

Sheria (hii sio technical issue ya kibiashara).

Hizo tatu za juu kweli ni key issues lakini sio hizo tu zipo sita.
Mazingira (hii ni key issue kwenye dunia ya leo katika majadiliano).

Mbili zingine za jamii na siasa wameparaza paraza tu lakini sijasikia emphasis katika majadiliano hayo mambo yanatakiwa kuwa kwenye maandishi pia especially ushiriki wa jamii.

Ushauri wa kisheria ni muhimu lakin unakuja kivingine sio key issue ya namna mradi utakavyoendeshwa kila siku.

Sheria ni muhimu katika kukadhia makubaliano; sasa makubaliano yenyewe bado ushauri wa sheria wa nini at this stage unless hao negotiators are clueless ata kwenye basic issues za majadiliano ya awali.

Mambo yenyewe awayaelewi halafu wanayakimbiza.

Huo mradi eleweni wanaenda kutoa mali za Tanzania sandakalawe wao wanachofikiria ni hizo $30 za uwekezaji wa awali not sure even those sums are justifiable, let alone wanajua madhara ya interest kubwa kwenye kugawana mapato huko mbeleni bila kuuliza source za hizo funds.

Yaani chief negotiator anampigia simu waziri kwa ushauri, Makamba huyu huyu ambae ukimsikiliza akiongelea hayo mambo hajui lolote; sasa sijui ana mshauri nini.

Hakuna shughuli hapo zaidi ya kugawa maliasili kwa mabeberu kwa bei chee.
 
Nini kifanyike sasa ndugu mtaalam ?
Au ndio "iache ikae hukohuko chini maana haiozi" ?
Kilatha
At least they should seek local input kwanza by poking ideas on what direction the government should pursue.

Kama wanaweza anzisha zoom meetings kila siku za kumsifia raisi; kipi kinawashinda kuanzisha mjadala wa mikataba ya mafuta na gesi wadau wachangie kushauri serikali ijikite na mambo gani kupata mawazo ya watu mbali mbali.
 
Nadhani waziri na timu yake ni wasikivu, ukitumia njia sahihi ya kuwasilisha mawazo yenye kujenga, naamini watayazingatia.
 
Katika ku summarise speech ya kiazi yule umeacha hoja ya msingi kwenye maeneo ya majadiliano.

Anadai wanatumia consultant kwenye key four areas kwa ushauri;
Kifedha (commercial)
Biashara (economic)
Kiufundi (technical)

Sheria (hii sio technical issue ya kibiashara).

Hizo tatu za juu kweli ni key issues lakini sio hizo tu zipo sita.
Mazingira (hii ni key issue kwenye dunia ya leo katika majadiliano).

Mbili zingine za jamii na siasa wameparaza paraza tu lakini sijasikia emphasis katika majadiliano hayo mambo yanatakiwa kuwa kwenye maandishi pia especially ushiriki wa jamii.

Ushauri wa kisheria ni muhimu lakin unakuja kivingine sio key issue ya namna mradi utakavyoendeshwa kila siku.

Sheria ni muhimu katika kukadhia makubaliano; sasa makubaliano yenyewe bado ushauri wa sheria wa nini at this stage unless hao negotiators are clueless ata kwenye basic issues za majadiliano ya awali.

Mambo yenyewe awayaelewi halafu wanayakimbiza.

Huo mradi eleweni wanaenda kutoa mali za Tanzania sandakalawe wao wanachofikiria ni hizo $30 za uwekezaji wa awali not sure even those sums are justifiable, let alone wanajua madhara ya interest kubwa kwenye kugawana mapato huko mbeleni bila kuuliza source za hizo funds.

Yaani chief negotiator anampigia simu waziri kwa ushauri, Makamba huyu huyu ambae ukimsikiliza akiongelea hayo mambo hajui lolote; sasa sijui ana mshauri nini.

Hakuna shughuli hapo zaidi ya kugawa maliasili kwa mabeberu kwa bei chee.
Uko sahihi kabisa, je wabia wetu katika mradi huo ni kina Nani kutoka wapi? Naanza kuona mwelekeo wa kuweka mayai yetu yote katika kikapu kimoja tu Marekani?
 
Nadhani waziri na timu yake ni wasikivu, ukitumia njia sahihi ya kuwasilisha mawazo yenye kujenga, naamini watayazingatia.
Mawazo ndio hayo aandae zoom meeting ya kujadili aspects za mikataba ya mafuta at least serikalini wawe na ideas za kutosha.

For starters sidhani kama engineer ni mtu sahihi wa kuongoza majadiliano anao umuhimu katika kufafanua technical process za mradi which require engineering expiations. Lakini ideal kwenye negotiators wanahitaji watu wenye finance skills na watu wenye uelewa mpana how the industry work on the business side.
 
Contents za Mh. Waziri Makamba

1. Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia nchini ulianza mwanzoni mwa miaka ya 1950. Mafanikio makubwa yalipatikana yakiwemo ugunduzi wa gesi asilia katika kisiwa cha Songo Songo mwaka 1974 na Mnazi Bay mwaka 1982. Aidha, Katika miaka ya 2010 na 2012 utafiti uliendelea katika maeneo ya kina kirefu cha Bahari ya Hindi. Hadi kufikia mwezi Mei 2022, jumla ya Futi za Ujazo Trilioni (TCF) 57.54 za gesi asilia ziligunduliwa katika maeneo ya nchi kavu na kina kirefu cha bahari. Kati ya kiasi hicho Futi za Ujazo Trilioni 47.13 zimegundulika katika Vitalu vilivyopo katika kina kirefu cha bahari ya Hindi, na Futi za Ujazo Trilioni 10.41 zimegundulika kutoka maeneo ya nchi kavu.

2. kutokana na ugunduzi huo wa kiasi kingi cha gesi asilia, Serikali ilifanya maamuzi ya uanzishwaji wa Mradi wa Kusindika na Kuchakata Gesi Asilia (Liquefied Natural Gas -LNG) kama njia bora ya kuendeleza rasilimali hiyo kwa ajili ya kuuzwa katika masoko ya Kimataifa na sehemu nyingine ya gesi hiyo kutengwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi

3. Serikali kupitia TPDC itashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huu. Ushiriki, katika ubia na ushirika wa uendeshaji wa mradi, utasaidia kujenga uwezo wa Shirika hili ili miaka ijayo liweze kufanya shughuli hizi lenyewe na kwa tija na ufanisi kwa manufaa makubwa zaidi kwa taifa. Safari ya kuisuka upya TPDC kama Shirika mahiri na la kimkakati imeanza kwa wewe kutupatia Mwenyekiti wa Bodi mzito na sisi tumeunda Bodi mpya yenye kutoa mwelekeo wa dira mpya tunayoitaka kwa TPDC.

4. Manufaa yatakayopatikana katika utekelezaji wa mradi huu ni pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi; kujenga uzoefu wa TPDC kupitia ushiriki wake; kuongeza mapato ya Serikali yatakayotokana na mauzo ya gesi; upatikanaji wa gesi asilia iliyochakatwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi; ushiriki wa watanzania katika uuzaji wa bidhaa na utoaji huduma; na fursa nyingi za ajira kwa watanzania hususan katika kipindi cha ujenzi na hata katika kipindi cha uendeshaji wa mradi.

5. pia tumefanya uamuzi wa kuanzisha Eneo Maalum la Kiuchumi (Special Economic Zone) kwenye eneo la mradi ambapo kutakuwa na vivutio mbalimbali, ikiwemo bei nafuu ya umeme, ili kuvutia viwanda na shughuli za kiuchumi katika mikoa ya Kusini.
Ni jambo jema,waharakishe kujenga Ili tuwapige BAO Msumbiji.
 
Uko sahihi kabisa, je wabia wetu katika mradi huo ni kina Nani kutoka wapi? Naanza kuona mwelekeo wa kuweka mayai yetu yote katika kikapu kimoja tu Marekani?
Wabia ni Shell, Equinox, Exxon Mobil na mwingine mimesahau jina that is not the issue.

Swala la msingi hapo tunaingia mkataba wa aina gani sheria yetu inaagiza framework ya kufuata ni PSA je itaheshimika.

Maana aina ya mkataba unao ingia unaamua pia kwenye pipa mgawanyo wenu upoje.

Zinaanza fixed distribution ambazo kuna royalities, recovery costs za investment (hizo $30 billioni lazima sirudi kwanza), gharama za ziada zikijitokeza.

Halafu mnakuja kwenye variable distributions kwenye pipa ambazo ni faida na zenyewe zinakanuni zake serikali inapata nini na wawekezaji wanapata nini na kodi inalipwaje.

Concession contract inakanuni za kwa pipa na service contract inakanuni zake.

Ni hivi kuna mambo ya msingi kwanza negotiators wanatakiwa kuyajua and some are basic legal matters; kabla ya kuwaza kufikia hatua za kukadhia mkataba which is pretty much ADR and understanding of international business law.

Good afternoon
 
Hii gesi asili nmeona inawekwe kwenye mitungi na kufungwa kwenye magari kama nishati mbadala wa petroli,kwa ufahamu wangu mdogo niliju gesi asili sio raisi kuwekwe kwenye mitungi ndio maana yanatumka mabomba kwa ajili kuisambaza kwa wahitaji,kama hilo limewezekana kwenye magari ni kwa nini isijziwe kwenye mitungi kwa ajili ya matumizi ya majumbani?

Mbona kwenye matumizi ya majumbani inatumika muda mrefu? Gasi majumbani mbona wengine wameingiziwa?
 
Mkataba huu wa awali sijui kama ulikuwa sahihi kuukimbiza kwa haraka kwetu wananchi Na kuhudhuriwa Na mheshimiwa rais kwani bado haujaweka manufaa ya moja kwa moja kwa serikali yetu ukiacha qualitative information kama vile Ajira Na gharama ya uwekezaji iliyotajwa.

Watanzania wanahitaji kuelezwa faida za Ziana za mkataba ikiwemo hisa za serikali na gawiwo kutokana Na projections za Mauzo Na kodi..

Naamini bado watarudi tena kwetu Na kuweka hadharani manufaa ya mradi kwa taifa letu ukiacha Ajira kwa watu wetu pekee ambayo ndo imetajwa leo.
 
Mbona kwenye matumizi ya majumbani inatumika muda mrefu? Gasi majumbani mbona wengine wameingiziwa?
Nafaham ya kwamba imekuwa ikitumika kwa matumizi ya nyumbani lkn kwa njia ya mabomba,hoja yangu ni kama imeweza kusindikwa kwenye mitungi na kutumika kwenye magari,je inashindakana nini kujazwa kwenye mitugi hii tunayotumia majumbani?
 
Nadhani ile ya magari sio LPG kama ya mitungi ya kupikia
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom