Hilo ‘ Dongo ‘ alilolitoa leo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete linawahusu akina nani hasa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,831
“ Wenye Maoni mseme wenyewe na msitumie Migongo ya wengine “

Naona Mkwere wa Watu tokea jana na leo kuna Watu ‘ wamemchefua ‘ mno kwa Kutaka Kwao ‘ Kumgombanisha ‘ na Mbabe wa Kikatiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa hivyo na Yeye ‘ anajihami ‘ mapema tu.

Kazi kweli kweli hakyanani!
 
JK atulie sisi watu wazima tulishamuelewa haitaji kutupa ufafanuzi zaidi.

Angekuwa ameeleweka sidhani kama kila mara angekuwa anatoa Ufafanuzi wake kwa wale Watu ambao anahisi hawakumuelewa na sijajua labda kama na Wewe ni miongoni mwao Mkuu.
 
Angekuwa ameeleweka sidhani kama kila mara angekuwa anatoa Ufafanuzi wake kwa wale Watu ambao anahisi hawakumuelewa na sijajua labda kama na Wewe ni miongoni mwao Mkuu.
Mimi nilimuelewa maana alikuwa anaongea kwa kiswahili " fasaha" sasa sijui wenzangu hawakuelewa nini.
 
Nyerere ni rais pekee Tanzania aliyeweza kumkosoa rais aliyemfuatia. Kwa kuangalia falsafa.

Hawa wengine wote wanasuasua kwa kuangalia siasa.

Watu walivyosema Kikwete kamsema Magu, nilisema Kikwete mwenyewe kajaa unafiki wa kuangaliana sura sasa hapa anadhihirisha.
 
amejihami kama Mwinyi kwenye ishu ya Makamba.
“ Wenye Maoni mseme wenyewe na msitumie Migongo ya wengine “

Naona Mkwere wa Watu tokea jana na leo kuna Watu ‘ wamemchefua ‘ mno kwa Kutaka Kwao ‘ Kumgombanisha ‘ na Mbabe wa Kikatiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa hivyo na Yeye ‘ anajihami ‘ mapema tu.

Kazi kweli kweli hakyanani!
 
Alikuwa akimzungumzia mwalimu kama kiongozi na rais ndipo akatoa huo msemo wa kujimwambafy.
Angekuwa ameeleweka sidhani kama kila mara angekuwa anatoa Ufafanuzi wake kwa wale Watu ambao anahisi hawakumuelewa na sijajua labda kama na Wewe ni miongoni mwao Mkuu.
 
Jana Mkwere kachokonoa tena Mzinga wa Nyuki Anaejimwambafy

‘Mzee Apson Mwang’onda hakuwa na Kiburi cha Madaraka, tujifunze kwake ‘

Kesho atatoa press release kututaka tusijifiche kwenye hotuba yake

Na Rais Wastaafu wakikaa kimya tunauliza Mbona wako kimya?, wakiongea tunawaambia waufyate

Imebidi watumie style ya kuongea na kukanusa

Yaan kwa style ya siku hizi kwenye Wasap ni kama unamtumia mtu kijembe akishasoma muda ule ule una delete to every one ili tu kumchanganya

Sie Wakwere kwa kuuma na kupuliza Alhamdulillah
 
Back
Top Bottom