Hili Tatizo la kuweka "L" badala ya "R" katika uandishi ni Janga la Kitaifa

Aiseee au mimi siyajui majanga,tena majanga ya kitaifa...

Kweli matumizi yasiyo sahihi ya R na L tunayaita majanga ya kitaifa.

Ni tatizo ila sio janga la kitaifa,nadhani hii huchangiwa na kutotiliwa mkazo sana mashuleni,kutoelewa kwa wanafunzi , na baadhi ya makabila hii ni kama kilema kwao.
 
Unakuta mtu kaandika
Kalibuni badala ya Karibuni, Selikali -Serikali etc Je ni moja ya viashiria vya kuporomoka kwa Elimu yetu ama ni nini?
Ukifuatilia zaidi utangundua kuwa ni generation flani ndio imekumbwa na hili janga,maana hata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu nao wamo walio kwenye hili janga,ukiachilia wale ambao kutokana na lafudhi za lugha zao ambapo hili kwao haliepukiki..
 
073d93ed4f1736b8a6e4a8860326e727.jpg

Hili ni janga la kitaifa.
 
Wataalamu watusaidie kufafanua hili jambo, kuna watu nawajua ni wasomi wazuri na ni akili za kazi haswaaa lakini bado wana hili tatizo
 
Alafu watu wa dar wanaona ndo fasheni, mi ukiongea ivo nakublock. Wat a waste.
 
Tatizo hilo li na nyie wanyamwezi sisi hatuna hilo tatizo huku kwetu.Mkija mnatusumbua mnatuharibia jina la vyakula vyetu badala ya UROJO mnasema ULOJO.
 
Back
Top Bottom